Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Uzi uliotukuka
 
Wimbo wa taifa hauna kazi mbali na mpira.

Anyways wanasema acha wafu waliokufa katika Bwana maana matendo yao yaambatana nao,

hayo tuseme ndiyo matendo ya marehemu Ben yameambatana naye,

Na pengine wakaandika lililoandikwa limeandikwa, Ben aliisha andikiwa iwe hivyo according to his life performance,

Let God be God.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku ndo kunakokufaa PASKALI UNAONA SASA UNAVYOTOA NONDO uharaka rule hata mm niliuona una walakini any way ishatokea KWA UPANDE MWINGINE ALITAKA TUAMKE NALO WAKULIA WALIE.......
 
Ile alisema kujipendekeza ndio kama hivi
Alipashwa na mpokea taarifa kuchukua muda kutafakari namna ya kufikisha ujumbe kwa WaTz
Huyu alikuwa ni Rais Kiongozi wa WaTz
Alipashwa kuhakiki Taarifa : Aliugua toka lini , Alilazwa wapi, chanzo cha kifo,

**Bado wanao muda wa kurekebisha mapungufu haya kabla ya siku ya mazishi Pascal Mayalla

Taarifa ilitolewa kama mjumbe wa kura za maoni ameaga
 
Yaaani like tangazo ni kama yale ya matangazo ya vifo radio one au RTD ya zamani full stop
 
Taasisi ni watu, lazima wafuate miiko, tamaduni na sheria za nchi.
 
Kama usivyotaka kuwekewa maneno na mimi usiniwekee maneno japo kuwa hitimisho langu kwao ilikuwa unaashiria usichosema.

Sijasema mkusanyiko wa watu unaweza sababisha watu kuondoka na maiti.

Nimesema moja ya sababu inaweza kuwa hakuna ulinzi wa crowd control, hospitali wagonjwa wa kila aina wanaingia 24 hours uwezi wacha umati ujae hadi getini ata mtu anaekimbizwa mahututi iwe tabu kumfikisha A&E akafia getini kisa waombolezaji; achilia usumbufu mwingine watakaopata wagonjwa waliolazwa watu wakiamua kuanza kuimba usiku wa manane.

Mambo kama hayo yanataka kupangiwa utaratibu kwanza.
 
Timing
Kwa vile msiba umetokea usiku, kutoa tangazo saa 6:30 usiku was not the right timing kwa Watanzania, news ya msiba ingekuwa held, halafu Wahariri wakaitwa Ikulu usiku ule, halafu Tangazo litolewe live saa 12:00 asubuhi, rais akiwa na VP na PM.


Kwenye zama za teknohama, huwezi kuchelewesha taarifa hadi asubuhi, ingekuwa ni aibu kwa Rais kuwahiwa kutoa taarifa na akina Kigogo.
 
Taasisi ni watu, lazima wafuate miiko, tamaduni na sheria za nchi.
Kuna kitu kinaitwa institutional reporting and narrative taratibu sio kigezo vile isipokuwa interface kati ya active institutional na audience.

Kwa ivyo kwa mtazamo wa Ikulu walichokifanya ni kuonyesha kiasi gani msiba umewagusa na ulimwengu utawaelewa kwa sababu habari yenyewe sio for local audience only but international too.

Hayo ndio kama malalamiko ya Ulimwengu kuhusu udikteta wa Mkapa uwezi kufanya kazi magazeti ya serikali kama unataka kuwa critic wa serikali; similarly uwezi kuandika kwenye gazette la WHO kama wewe unataka ku-promote mitishamba. Unapozuiwa kufanya ivyo na mhariri sio udikteta ni kwamba kazi yako aiendani na institutional narrative.
 
Kwenye zama za teknohama, huwezi kuchelewesha taarifa hadi asubuhi, ingekuwa ni aibu kwa Rais kuwahiwa kutoa taarifa na akina Kigogo.
Good point.

Ila, walau basi Rais angeisoma taarifa kwenye teleprompter.

Kwa nilivyoona, alichokitangaza kilikuwa kinatoka kichwani mwake. Hakuwa anasoma sehemu...

Na pia angeweza kuwa attired appropriately.
 
Kuhusu kifo cha Karume, nilikuwa mdogo lakini kichwani kiliingia kila kitu. Aliawa saa 12 jioni. Kifo chake kilitangazwa subuhi kesho yake saa 2.

Usiku ule kulikuwa na tangazo tu la hali ya dharula. Wazanzibari hawakuruhusiwa kutembea kuanzia saa 2 usiku. Vyombo vya usafiri vya anga na majini vilizuiwa kuingia au kutoka nje ya Zanzibar.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha kama kawaida yenu watanzania wajuvi wa kuongea na kuandika!

Eti dressing code hahaha
Mara hajaandaliwa mara ooh sijui nini
Yote haya mtafute vya kukosoa hahah
Mnapenda misiba ya maigizo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…