Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Mayala, wakati ukikosoa kurugenzi ya mawasiliano, kosoa vyombo vyote vya habari. Ninasikiliza vyombo vingi vya habari kwa siku mbili sasa. Wengi wanapiga miziki ya furaha tu, bila kujali tangazo la msiba huu. Mawasiliano ikulu ni sehemu ya waandishi wa habari wetu nchini ambao huenda mafunzo yao, hayatoshi kuleta hisia za msiba.
Wanapitia mafunzo duni. Hata ktk TV hawawezi kuonesha hisia za taarifa wanazosoma. Mtu anasoma mapigano kwa furaha ya michezo. Anasimulia mtoto aliyebakwa bila hata hisia usoni. Waandishi habari ni habari na hawaoni kama wana wajibu wa kuibadirisha jamii.
 
Hivi kama Hayari baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere tulijulishwa amefariki hospitali ya Mt. Thomas Uingereza alikokuwa amelazwa, Mzee wetu Mkapa kulikoni hatuelezwi alilazwa hospitali ipi! Ni muhimu kuelewa kuwa viongozi ni mali ya Taifa hivyo mali ya Wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wamepewa jukumu la kumshauri Rais katika kitu lakin naona kama hawatekelezi majukumu yao sasa sijui wanamuogopa au ni nni.

Mkuu jibu la swali lako liko ndani ya swali lenyewe! [emoji3]

Anayetakiwa ashauriwe anashaurika? Hapo ndipo issue ilipo!
 
Mkuu Pascal Mayalla
Kwa jinsi taarifa ilivyokua hakuna shaka yoyote kua ilikosa vigezo vya msingi vya ku-qualify kua imepitia kwa wabobezi wa habari, either kwa maksudi au kwa kutokujua ila haikua SMART!
 
Watanzania watamsamehe BWM kwa mabaya yake aliyotenda wakati wa uhai wake. Mwenyezi Mungu mwenye rehema amewaleta waovu na wenye mema duniani ili kuangalia matendo yetu. Ni vyema kuwa na huruma kwa waovu wengi hapa duniani ambao hawafahamu yale wanayoyatenda, maovu hayana nafasi hapa duniani.

Watanzania tuchape kazi tuondokane na umasikini wetu, tusitegemee uncle kutoka nje ya Tanzania.
 
Nimelazimika kurudia uzi huu baada ya kuona ikulu ya Chamwino haikuomba radhi baada ya andiko zuri la lenye ujumbe wa maslahi mapana ya Taifa kutoka kwa niliyemtaja hapo juu baada ya Rais wetu kuutubia taifa letu paspo kuzingatia sheria za matangazo ya vifo ya viongozi wetu wa kitaifa.

Kiukweli, Mh. Rais alitangaza kifo cha raisi wetu wa Awamu ya Tatu tatu ndivyosivyo hata Wimbo Taifa tu haukupigwa, hakuvaa vazi rasmi na mengineyo mengi.

Kimsingi, tangazo la kifo lilikuwa kama tangazo la uapisho wa viongozi au kufungua majengo fulani jambo ambalo sio kabsa.

Ikulu ya Chamwino iombe radhi watanzania kukengeuka kwa namna hii ni ishara ya kuzalilisha tunu za Taifa, ikiwemo Wimbo wa Taifa.
 
Wasamehe! tumsamehe! tuwasamehe! Msiba uliowapata alioupata tuliopata ni mkubwa in short tulivurugwa alivurugwa walivurugwa imeondoka ni nguzo muhimu
 
Hajawahi kusikika kuwa Benjamin Mkapa anasumbuliwa na maradhi yoyote, hivyo taarifa kuwa amefariki hospitali ni shocking, hospitali gani na ameumwa nini, ni maswali ambayo taarifa ya rais ilikosa.

Hata mimi bado sijui nishike lipi

  • Msaidizi wa Marehemu alisema aliondoka nyumbani kwa Mkapa na alipofika nyumbani alipata habari kuwa Mkapa amefariki
  • Msemaji wa familia anasema Marehemu alitaka kusimama kwenye kiti baada ya kutazama taarifa ya habari lakini alishindwa akakaa na kuinama, alipopimwa alionekana ameshafariki.
  • Kiongozi Mkuu anasema aliongea na Marehemu akiwa hospitali na akamwambia Yohana usiwe na wasiwasi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mambo ni vululu tyuuuuuuh.
 
Angalia hio mistake tena ni YouTube chanel ya ikulu badala ya Urais wameandika Uraiz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…