Tangazo la Kondomu au Pedi likirushwa nikiwa karibu na binti yangu huwa napata tabu sana

Tangazo la Kondomu au Pedi likirushwa nikiwa karibu na binti yangu huwa napata tabu sana

bob nasta

Senior Member
Joined
Apr 25, 2011
Posts
145
Reaction score
118
Jamani, ni kweli tuko kwenye utandawazi lakini haya matangazo yamezidi ukali utasikia Kondomu ina vidoti inanukia inaongeza utamu au yule binti yuko chooni analia damu zimemtoka ghafla hana Pedi mambo hayo yanatia ukakasi au ni ushamba wangu tu ndo unanisumbua.
 
Aibu ya nini? Ni muda wa kukaa na watoto wenu na kuwapa elimu juu ya afya ya uzazi kama wewe baba au mama hutazungumza na mwanao, nani azungumze nae? Tv?
"Condom inavipele vinavyo kuna vizuri, hivyo itakufanya kuongeza radha ya tendo" mixer brah brah nyingine kibao

Aah babu! Kuna maneno mengine kwenye matangazo yanaleta ukakasi sana, hii ikinikutaga na washua huwa natamani ardhi ipasuke niingie kujificha.....

Labda ni ushamba wetu mimi na mtoa mada
 
Matangazo yamekuwa too graphic
Kuna hawa madkt wa tiba asili yaani ukiwa na mdada pembeni unaona aibu wewe

Dkt anadai anatibu magonjwa mbalimbali lakini ukisikiliza matangzo kila siku ni yeye na nyeti za watu tu humsikii akizungumzia kisukari, BP
 
Hivi yule dkt Ndodi alifiaga wapi maana anakamba balaa
 
Matangazo Pendwaaa[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
[emoji23][emoji23] ndio maana wazazi wengine hununua tv mbili nyengine anaweka chumbani kwake kuepuka Mambo kama hayo..
Kwahiyo mzazi ukiwa na tv chumbani utakuwa hukai sebuleni? Au ukiwa sebuleni inazimwa? Na redio je, mbona matangazo ni hayohayo siku hizi?
 
Back
Top Bottom