Tangazo la Kondomu au Pedi likirushwa nikiwa karibu na binti yangu huwa napata tabu sana

Tangazo la Kondomu au Pedi likirushwa nikiwa karibu na binti yangu huwa napata tabu sana

Kwahiyo mzazi ukiwa na tv chumbani utakuwa hukai sebuleni? Au ukiwa sebuleni inazimwa? Na redio je, mbona matangazo ni hayohayo siku hizi?
Nisaidie kujibu hayo maswali mi nipo busy nakunywa juisi kola hapa.. tusitiane stress bure..😅
 
Matangazo yanahitaji ubunifu.
Watayarishaji wa matangazo wanakosa ubunifu.

Ukiangalia hata Sanaa za zamani nyingi zilikua na ubunifu mwingi.

Kuna nyimbo za zamani ambazo zilikua zikiongelea topic za kiutu uzima Kama maswala ya mapenzi. Lakini hata mtoto alikua akiweza kuusikiliza, ama kuuimba na asijue anaongelea au anaimba nini. Maana ujumbe ulikua umejificha.

Hata baadhi ya matangazo yalikua yanasema hoja wazi bila hata ya kuweka manjonjo ambayo yanaleta shida katika kutoa taarifa husika kiasi kwamba walengwa walikua wakifikiwa bila kuleta shida kwa wengine. Au Rika lisilo husika.

Matangazo ya siku hizi Mengi ni hovyo. Hayana ubunifu. Hawajui jinsi ya kuyatayarisha waelewa Rika husika tu.

Nadhani watayarishaji huwa wanapuuzia jinsi yatakavyopokelewa na shida yatakayoleta.
 
Matangazo yamekuwa too graphic
Kuna hawa madkt wa tiba asili yaani ukiwa na mdada pembeni unaona aibu wewe

Dkt anadai anatibu magonjwa mbalimbali lakini ukisikiliza matangzo kila siku ni yeye na nyeti za watu tu humsikii akizungumzia kisukari, BP

Eti yeye na nyeti za watu tu😀😀😀
 
Jamani, ni kweli tuko kwenye utandawazi lakini haya matangazo yamezidi ukali utasikia Kondomu ina vidoti inanukia inaongeza utamu au yule binti yuko chooni analia damu zimemtoka ghafla hana Pedi mambo hayo yanatia ukakasi au ni ushamba wangu tu ndo unanisumbua.
kuna lile tangazo la Free styl sijui,yuko Mobeto anajibinua binua tule tutako chake,linanudhi sana,halina heshima kwa wazazi na watoto
 
"Condom inavipele vinavyo kuna vizuri, hivyo itakufanya kuongeza radha ya tendo" mixer brah brah nyingine kibao

Aah babu! Kuna maneno mengine kwenye matangazo yanaleta ukakasi sana, hii ikinikutaga na washua huwa natamani ardhi ipasuke niingie kujifisha.....

Labda ni ushamba wetu mimi na mtoa mada
Yan nimeangusha bonge moja la cheko 😆😆😆
 
Jamani, ni kweli tuko kwenye utandawazi lakini haya matangazo yamezidi ukali utasikia Kondomu ina vidoti inanukia inaongeza utamu au yule binti yuko chooni analia damu zimemtoka ghafla hana Pedi mambo hayo yanatia ukakasi au ni ushamba wangu tu ndo unanisumbua.

mimi juzi nilikuwa nyumbani kwa maza akawa anatazama channel ya sinema zetu,ghafla wakaanza kuongea matusi na mambo ya kitandani nikanyanyuka nikaondoka,leo pia nimekuta imewekwa channel ya sinema zetu wanasifiana kukatika mauno kitandani nikabadili channel
 
Na wanarusha muda wa taarifa ya habari, familia yote iko hapo inaangalia.

babe mimi kuna Bongo movie tulikua tunatizama na maza,jamaa anamsifia demu wake mambo ya kitandani
hata wazungu tu wana maadili ndio mana wana viewers Guidelines.
 
Aibu ya nini? Ni muda wa kukaa na watoto wenu na kuwapa elimu juu ya afya ya uzazi kama wewe baba au mama hutazungumza na mwanao, nani azungumze nae? Tv?

kwa tamaduni za mtanzania mambo ya hedhi ni mama na mtoto wa kike ndio wanafaa kuongea
Baba anafaa ku deal na watoto wa kiume.japo ulichosema ni sahihi ila umekosea kuona kwamba ni sawa baba kuongea na binti mambo ya uzazi hiyo sio sawa. nimemkumbuka baba yake na rafiki yangu alikuwa anamwambia jamaa akumbukd condom kila siku anamsisitiza
 
mimi juzi nilikuwa nyumbani kwa maza akawa anatazama channel ya sinema zetu,ghafla wakaanza kuongea matusi na mambo ya kitandani nikanyanyuka nikaondoka,leo pia nimekuta imewekwa channel ya sinema zetu wanasifiana kukatika mauno kitandani nikabadili channel
Bongo movie hutukana matusi, na maswala ya ngono hadharani, Hadi aibu
 
Bongo movie hutukana matusi, na maswala ya ngono hadharani, Hadi aibu

wanakwama sana aise hapa nafikilia kum convince maza abadili king’amuzi aweke Dstv. maana mambo ya sinema zetu ni aibu ule sio uigizaji ni uasherati
 
babe mimi kuna Bongo movie tulikua tunatizama na maza,jamaa anamsifia demu wake mambo ya kitandani
hata wazungu tu wana maadili ndio mana wana viewers Guidelines.
Hivi hizo bongo movies ni mamlaka gani inawajibikwa kuwaweka kwenye mstari?
 
Hili swala nashindwa nikae upande upi maana Kama Ni swala la kuvutia ngozi kwa muwamba Ngoma basi kila mmoja naona yukk sahihi.

Ngoja niendelee kusubiria wenye kutoa point nyingi nilale huko huko[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom