Tangazo la Kondomu au Pedi likirushwa nikiwa karibu na binti yangu huwa napata tabu sana

Kumbe tupo wengi,Ila mi naataga shida nipo na wazazi Mara ghafla wimbo msanii wakike kaupiga uyupi tuu anawageuzia choo anaanza kutetema aisee huwa inakuwa shidaaa
 
mm kwanza huwa nakosa amani,kabisa kwanza sipendag hata mchumba azungumzie kuwa sujui period
 
Jamani, ni kweli tuko kwenye utandawazi lakini haya matangazo yamezidi ukali utasikia Kondomu ina vidoti inanukia inaongeza utamu au yule binti yuko chooni analia damu zimemtoka ghafla hana Pedi mambo hayo yanatia ukakasi au ni ushamba wangu tu ndo unanisumbua.
mimi kama mwanamke sioni ubaya wake kwa sababu zifuatazo kwa sasa watoto wanaanza mapenzi mapema mno jamani hakuna kipya leo hii unakutana na katoto kamepaka lipstic kanavaa bikini kanaenda kuogelea kwa wale wa mjini, huko kijijini ni wapo na mafuta ya midomoni na poda zile za baby , unafikiri mtoto anajipodoa amuoneshe nani kuwa ni mzuri kama sio mwanaume? haya ukisema matangazo yana nia mbaya je huko mashuleni wanapopewa elimu hiyo kwa undani hali ipoje? wanavyosema yana harufu nzuri ni kwamba kutoa hamasa watu kutumia kwa wingi kulipo kuenda kavu na kujipatia magonjwa zaidi...... ifike mahali tusiseme sana utamaduni utamaduni tuangalie na kizazi chenyewe, kingine matangazo ya pedi yamesaidia sana watu kuona hedhi ni kitu cha kawaida kulipo ilivyokuwa mwanzo ilikuwa ni aibu kabisa ukikutwa na siku zako lakini leo hii kuna wanaume wananunulia watoto au wake zao pedi maana wanaelewa hali halisi ilivyo, mimi naona yangeoneshwa muda wote tuokoe vijana zaidi ni juzi tu tumetoka kusoma hapa #jamiiforum kuwa maambukizi kwa vijana 15-24 yameongezeka kwa 40% je tuyazuie kabisa huku tukijidanganya hawafanyi kumbe tunazidi poteza nguvu kazi ya kesho au tuendelee kutangaza zitumike ili watu waone umuhimu wake au vipi
 
Sawa lakini kuwe na staa jinsi ya kuelimishana mbona haya mambo yapo toka zamani lakini kulikua kuna utaratibu nyie nani aliwafundisha kuvaa pedi si mabibi shangazi na wamama kwa siku izi basi bora wafundishwe mashuleni sio mmekaa sebuleni mara condom pedi mwisho litakuja tangazo lakufundisha kukata mauno kitandani ndo tunakoenda uko lakini nimekuelewa
 
Ni kudhalilishana tu miaka nenda miaka rudi watu wametumia na kufundishana kimya kimya tu
 
Pia na bongomuvi, kuna maneno hayana stara kuyatamka kwenye kadamnasi km neno malaya. Inabidi wahariri wa hizi muvi wajiongeze.
 
Kwa tulipifikia tu ndugu zanguni tuwe wapole Dunia imeharibika haswaaaa
 
Back
Top Bottom