Tangazo la Kupotea kwa Members wengine wa JF

malaria Sugu
hivi huyu Malaria Sugu alikua na udugu na FaizaFoxy?

Naam, Tena kabisa. Msome Bi Fatma anauelezea undugu wetu kwa kina:

Waislamu wote ni ndugu

Na Fatma Mussa

KATIKA maisha yake, mwanadamu analazimika kuwa na mahusiano baina yake na watu wengine. Mahusiano hayo kwa lugha rahisi yanaitiwa Udugu. Udugu umegawanyika katika sehemu nne. Udugu wa kuzaliwa (damu), udugu wa ndoa, udugu wa ubinadamu na udugu wa imani.

Udugu wa damu una mipaka yake, ndoa hata ubinadamu pia una mipiaka yake. Lakini udugu wenye nguvu na unaotiliwa mkazo sana na Uislamu ni udugu wa imani. Udugu huu ni ule unaotokana na watu kuwa na imani moja.

Udugu huu ndio ambao IshaAllah tutautizama katika mada yetu hii. Allah (s.w.) anatupa khabari katika Qur'an tukufu sura ya 49:10: "Kwa hakika Waislamu wote ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu (msipuuze jambo la kupatanisha) ili mrehemewe".

Kwa mujibu wa aya hii tunafahamishwa kuwa Waislamu wote ni ndugu moja, ummah mmoja na ni sawa na mwili mmoja ambao kidole kimoja tu kikipata maumivu mwili wote unakosa raha na amani.

Vile vile aya hii inatuonesha kuwa Uislamu hauna mipaka ya jiografia ya mtaa kwa mtaa, wilaya kwa wilaya, mkoa kwa mkoa, nchi kwa nchi na kadhalika. Bali Waislamu wote kokote waliko ni ndugu moja na ummah mmoja ni sawa na ndugu wa baba mmoja na mama mmoja au hata zaidi ya hapo, tatizo la mmoja wao linakuwa ni tatizo la Waislamu wote kote duniani bila kujali tofauti za kabila, rangi, hadhi nafasi na kadhalika kama tufahamishavyo katika Qur'an 49:13:

"Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja, Adamu) na yule mwanamke (mmoja, Hawwa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbalimbali) ili mjuane. Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi..." (49:13)

Kama nilivyokwishaeleza hapo juu, kuwa Uislamu ni ummah mmoja na hatuna mipaka ya jiografia. Ummah huu mmoja wa Kiislamu unaitwa "Ummat l-Islam" yaani Ummah wa Kiislamu.

Mipaka hii ya kijiografia tunayoiona leo iliwekwa na wakoloni kwa lengo la kutaka kututawala kwa kuanza kutugawa, ili kurahisisha utawala wao.

Waislamu kote ulimwenguni ni sawa na mwili mmoja, hivyo raha ya Muislamu mmoja ni raha ya wote na tatizo la Muislamu mmoja ni tatizo la wote.

Yanayotokea leo ulimwenguni dhidi ya Uislamu kama vile Chechnya, Bosnia, Cossovo, Kashmir, Afghanistan, Palestina na kadhalika yanatakiwa yamguse kila Muislamu popote alipo hapa duniani na tatizo hilo lishughulikishe hasa vichwa vya Waislamu na kuangalia jinsi ya kulipatia ufumbuzi stahiki.

Namna gani Mtume aliweza kuimarisha udugu wa Kiislamu

Miongoni mwa mambo ya muhimu ya kwanza kabisa ambayo Mtume (s.a.w.) aliyaanzisha na kuyahimiza ni kuunganisha udugu.

Ikumbukwe wakati Mtume (s.a.w.) amehama toka Makkah kwenda Madina alikuta kuna ugomvi kati ya makabila mawili ya Aus na Hazraj, ambayo kwa muda mrefu sana yalikuwa na ugomvi wa kudumu, lakini Mtume (s.a.w.) aliweza kuondoa mzozo huo na watu hao wakaishi kwa pamoja kama ndugu wa imani.

Haikuishia hapo bali aliwafundisha watu wake na kuwaelimisha juu ya dhana nzima ya udugu katika Uislamu.

Hii inathibitishwa na mapokezi waliyoyapata Muhajiriin toka kwa An-swar. Kila mmoja alimpokea mwenzake kama ndugu yake khasa alikuwa tayari kutoa kila kilicho chake kwa ajili ya ndugu yake. Ilifikia baadhi ya Answar kuacha hata wake zao ili wapate kuolewa na wenzao Muhajirin, kwani waliwacha wake zao Makkah.

Undugu kama huu ndio uliojengeka na ndio ulisaidia kuimarisha na kufanikisha dola ya Kiislamu iweze kusimama Madina. Kila mmoja alikuwa anashirikiana na mwenzake kama ndugu moja katika kuhakikisha Uislamu unakwenda mbele.

Vile vile undugu uliojengeka wa Waislamu ndio uliopelekea kufungwa kwa Baia (Baiatul Ridhwan) ambapo Waislamu walikuwa tayari kufa wote kwa kulipa kisasi baada ya kupata tetesi za kuuliwa Uthman (r.a.). Hili tunafahamishwa katika Qur'an 48:18.

"Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waislamu, walipofungamana nawe chini ya mti na alijua yaliyomo nyoyoni mwao, Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawapa kushinda kwa zama za karibu".

Ushindi huo wa karibu uliweza kupatikana kutokana na imani thabiti waliyokuwa nayo na kutokana na ule udugu wa kweli waliokuwa nao.

Tujiulize ni kitu gani kilichowafanya Waislamu wale kula kiapo cha utii cha kuwa tayari wote kufa kwa tetesi ya kuuawa Muislamu mwenzao. Hiyo inatokana na ule udugu wa kweli wa Kiislamu uliojengeka ndani ya nafsi zao.

Je, sisi Waislamu wa leo tukoje, je, tumefikia hatua hii, kama hatujafikia tunangoja nini, je, tatizo la mmoja wetu linatushughulisha sote? Ni miaka miwili sasa tokea ndugu zetu Waislamu wauawe Mwembechai ni hatua gani tumechukua? Je, tumekuwa tayari kujitoa muhanga nafsi zetu kwa ajili yao?

Mfano mwingine wa udugu wa kweli wa Kiislamu, ni kile kitendo cha Abubakar (r.a.) kumnunua Bilal na kumuacha huru kutokana na utumwa, kilichomfanya Abubakar afanye vile si kingine bali ule uchungu aliokuwa akiupata alipoona ndugu yake Muislamu anateswa naye anaouwezo wa kumkomboa.

Sambamba na hilo iliwahi kutokea mwanamke wa Kiislamu kuvuliwa hijabu yake na Mayahudi Madina, Muislamu aliyeliona tukio lile hakuweza kuvumilia, bali alichukua hatua ya kumuua mtu yule kwa kitendo chake cha kumdhalilisha mama wa Kiislamu.

Jambo lililopelekea Mayahudi nao kumuua yule kaka wa Kiislamu na Mtume (s.a.w.) kuamrisha kuandaliwa jeshi kwenda kupambana na Mayahudi.

Lakini katika wakati wetu tulio nao mara kwa mara watoto wa Kiislamu wamekuwa wakidhalilishwa kwa kuvuliwa hijab zao lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na Waislamu. Huu ni udhalili mkubwa kwa Ummah wa Kiislamu.

Waislamu Chechnya wanauawa, kuteswa, kudhalilishwa na manyanyaso ya kila aina na wanashindwa kujitetea ipasavyo kwa vile hawana silaha, hawana chakula cha kutosha. Japokuwa zipo nchi zenye uwezo huo lakini hazijatoa msaada stahiki kwao.

Hiyo ndiyo hali tuliyonayo Waislamu wa leo kote duniani, mipaka ya jiografia tuliyowekewa na makafiri imetupagaranyisha na kutuondoa katika ule ummah mmoja wa Kiislamu. Hatushughulishwi na madhila yanayowakuta ndugu zetu kisha tunakaa Misikitini kusoma surat Hujurat kuwa Waislamu wote ni ndugu, udugu gani tulionao katika hali kama hii, udugu gani tulionao ilhali hatupendani, hatusaidiani na hatuhurumiani. Tusitaraji kupata pepo ya Allah (s.w.) katika hali kama hii.

Tatizo la Muislamu mmoja liwe letu sote ifikie mahali ikisikiwa tu Muislamu wa sehemu fulani amepatwa na tatizo lishughulishe Waislamu wote.

Chanzo: An-nuur Na. 241
 
Mr President, Ocampo four, chamviga na Mkandara mkerewe anayeishi Canada
 
niliwafananisha coz avatar zinafanana kwa kiac flan anyway arudi bhas jf jaman pla namiss michango yake walah da FaizaFoxy fanya hima umhimize,arudi
 
Game theory hata katika list ya members jayumo tena. Labda alibadili ID na kuwa verified.
 
Back
Top Bottom