Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,490
- 38,302
Heshima sana wanajamvi,
Barua kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Mkaazi ya tarehe 12/08/2025 kuhusu uuzaji wa viwanja eneo OLMOT karibu na uwanja wa mpira wa AFCON.
Tarehe 12/08/2025 naijongelea ofisi ya Mkuu wa Wilaya Arusha kwaajili ya kulipia na kujaza form.Ninapoulizia utaratibu naambiwa tayari ugawaji wa number za waombaji 60 zimeshamalizika.
Naambiwa nisubiri hadi waombaji 60 wakimalizika number nyingine 60 zitatolewa,tunaamua kusubiri lakini majibu tunayopewa na wale waliopewa number za mwanzo yanakatisha tamaa.
Kwanza tunaambiwa viwanja vya watu wadogo yaani kuanzia sqm 320 hadi 600 vimekwisha vimebaki low density sqm 2500 hadi 4000.Ukizingatia sqm 1 ni tsh 32,000 viwanja vya biashara na makaazi 27,000.
Baada ya muda tunapenyezewa taarifa kwamba viwanja vimerejesha Dodoma na vingine vimetengwa kwaajili ya Wazanzibar kwakuwa wao kisheria wanaruhusiwa kumiliki ardhi Tanganyika.
Baada ya siku mbili tatu tunapewa mchongo kwamba viwanja vingi wamejigawiya wenyewe maafisa ardhi
Hiki kitengo cha ardhi Arusha yafaa kichunguzwe na hatua stahiki zichukuliwe.
Ngongo kwasasa Monduli.