Samahani wakuu wangu JF, ni kwamba sina access ya mtandao, hapa nimeazima tu laptop ya mtu, ni kwamba:-
1. Sherehe zinaendelea kama zilivyopangwa, jana ilikuwa siku ya watoto wa yatima, leo zimehamia nyumbani Sea View, kuna wana JF waliojitokeza hapa saafi sana.
2. Pia naomba kugusa kidogo huu ujumbe wa ndugu mmoja hapo juu kuhusu watoto wa Mzee Malecela, ni ishu ambayo imekwua ikisemwa kwa muda mrefu sana, lakini cha muhimu ni kwamba ukweli uko wazi na Tanzania kama kawaida huwa tunasumbuliwa sana na waandishi makanjanja ambao huandika bila kuuuliza maswali muhimu sana ya kiandishi na hivyo kuishia kuupotosha umma, ni kwamba Mzee Malecela ana watoto wafuatao:-
- Waliotangulia mbele ya haki ni watatu, wawili wa kiume na mmoja wa kike, na sio wawili kama Michuzi alivyoandika, nao ni wakiume Senyagwa Malecela, Mkwawi Ippy Malecela, na wa kike ni DK. Irene Malecela.
- Waliobaki ni saba, sio watatu kama ilivyosemwa na Michuzi, nao ni kwa umri:-
1. Wiiliam Malecela.
2. DK. Mwele Malecela.
3. DK. Secelela Malecela.
4. Mwendwa Malecela Bisendo.
5. Tully Malecela Mwaipopo (Adapted)
6. Samweli Malecela.
7. Nyagwa Malecela.
3. Sasa kati ya hawa watoto wakiume ni wawili, na wengine ni wa kike, sasa ukichanganya na watoto wanne wa mkewe ambaye alimuoa hivi karibuni
wanakuwa ni watoto 11, kwa sababu ukioa mke si na watoto wanakuwa wako!
- Kwa hiyo hii habari ya Michuzi ndio hasa bongo tunaouita uandishi wa ukanjanja.
Kwaherini na tutaonana tena soon, hapa uwanjani.
William.