- Mkuu SHY, heshima mbele sana na matokeo ya utaalamu wako ambao ninauheshimu sana, kama nilivyosema kule nyuma baada ya kufika huko bondeni mwenyewe nilijionea makenge yaliyomo kwenye msafara wa mamba, kama ilivyo humu ndani, nilijionea part ya makenge on the deal yaani the scam na part ambayo ni genuine na ndiyo ninayoifanyia kazi hadi sasa,
- Infact, Jumatatu ya next week jamaa zangu watatu watakuwa na the first interview kuhusiana na na hii deal ya kwenda majuu, wengine wote ninawashukuru sana kwa utabiri wenu mzuri sana nafikiri na nyinyi mmewahi kukutana na makenge ndani ya haya ma-deal, siku zote katika maisha panapokuwa na uongo, lazima pawepo na ukweli japo kidogo, shetani hawezi ku-create uongo kwa 100% bila kuwepo ukweli haijawahi kutokea katika masiha ya hapa duniani,
- Again Mkuu wangu SHY shukrani kwa your findings, ambazo originally ndio zilinifanya nishuke mwenyewe bondeni na bado ninaheshimu sana utaalamu wako kwa sababu bila ya wewe ningeupanda mkenge, kwa wengine wote ujumbe wangu bado ni ule ule, kwamba akili ni kama parachute ina-function better ikifunguka na sio kweli kwamba google ina majibu ya maswali yote duniani mengine haina ndugu zangu.
Sasa kama nilivyoahidi, ni kwamba jamaa zangu watatu wakishafinikiwa, nitaanza kwanza kuwafahamisha ndugu zangu wengi wa-Tanzania walionitafuta na wenye shida toka bongo kwanza, ma baadaye ndio ikibidi nitaweka hapa, unajua JF ni demokrasia makini sana hapa tunaheshimu sana mawazo ya kila mwananchi, kwa hiyo ndugu zangu mnaweza kuendelea na hizo ngonjera na taarabu, ila kinachonisshangaza ni kwamba watu wanaomini hii ni scam wanavyolala macho na hii thread ambayo inazidi kukua kwa kasi ya ajabu sana, saafi wakuu tupo pamoja na tuendelee kujadili! ila next weekend nitashuka tena huko bondeni, kama kuan wana-JF huko bondeni tuwasiliane ili tuweze kuonyeshana njia namna ya kusaidia ndugu zetu!
Na wakuu nitaendela kuwafahamisha yanayojiri na hii deal.
Respect.
Field Marshall Es!