bishankara
Senior Member
- Feb 21, 2012
- 140
- 8
Salam kwa nyinyi nyote wana jf. Jina langu naitwa Rwehumbiza. Nimemaliza chuo kikuu mwaka 2011 katika fani ya biashara nikijikita zaidi katika masuala ya ununuzi (materials management) na kufaulu vizuri masomo yangu, pia kabla ya hapo ufaulu wangu katika ngazi ya kidato cha nne na sita ni mzuri kwani nilipata daraja la kwanza (division one) kwa hvyo vidato vyote. Mpaka sasa nina uzoefu wa zaidi ya mwaka mmoja katika masuala ya manunuzi na ugavi. Pia nimesajiliwa kwenye bodi ya wataalamu wa manunuzi na ugavi. Lengo la kuandika haya yote ni kujitangaza kwa makampuni na mashirika mbalimbali yaliyotayari kuniajiri ili nifanye kazi pamoja nayo. Kuanzia july mwaka huu mpaka sasa nimeajiriwa na kampuni flani hapa mjini dar es salaam lakini maslahi niyapatayo hayalingani na kazi nizifanyazo, na pia mwanzilishi wa kampuni analenga zaidi kuinua familia yake kwani ndo malengo yake makuu ya kuanzisha hii kampuni. Hivyo basi kwa kampuni au shirika lolote lililotayari kufanya kazi na mtu ambaye ni mchapa kazi, mpenda maendeleo, mwenye kujituma, na mwenye uzoefu katika vitendo, mawasiliano yangu ni 0684073794. Natumaini ya kuwa nitapata majibu chanya kutoka kwa waajiri.