Tangu Ahmed Ally aje Msimbazi timu yetu haijawahi kuifunga timu ya Yanga

Nasema Uongo Ndugu Zangu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
279
Reaction score
779
Mara yamwisho tumeifunga Yanga kule kigoma kwenye FA goli 1 bila, wiki hiyo mgogoro wa Manara na Barbra ulikuwa kwenye peak. Baada ya Manara kwenda Yanga, kijana machachari Ahmed Ally akaja Simba.

Sasa tangu aje Simba hatujawahi kuifunga Yanga mara 5 mfululizo, binafsi nahisi huyu mwamba ana gundu.

Tumtafute hata Masau Bwire tuone kama atakuwa na bahati nayeye, Matola hahusiki kabisa kwenye hili.
 
Toka mzungu poli aje yanga timu yetu haijawahi kufika makundi caf [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Simba kuifunga yanga kwenye league ni ngumu kwasababu kuna makundi kwenye team ya simba wanaotaka babra afeli na moja ya kitu wanachojaribu kufanya ni kuhakikisha wanatoa siri ya kambi kwa mpinzani ili iwe sababu ndio maana manara alionekana kwenye hotel siku chache kabla ya mechi ya yanga na simba na matola ndio muuza ramani mkuu kwa manara na ndio maana huwezi kuta manara amemdhihaki au kumtania matola iwe bahati mbaya au kusudi kwasababu wanajua wanachokifanya ngoja niishie hapo.
 
duh! aisee kweli Simba mbumbumbu FC. yani magoli yote ya Yanga kwa Simba ni yenye kuonesha quality ya juu wachezaji wa Yanga we unasema mnafungwa kwa sababu ya makundi tena wapi na wapi? Makundi ndo yanacheza uwanjani?Goli la Feisal ni kutoka kundi la mpira pesa au mpira biashara?

Simba haina uwezo wa kuifunga Yanga chukua hiyo itakusaidia , mkiendeleza imani hiyo sijui tunawaua nje ya uwanja basi tutawafunga karne nzima maan hamtaboresha timu yenu, kumbuka asiekubali kushindwa si mshindani!
 
Malengo ya Simba hayajawahi kuwa kuifunga yanga ndio yamefikiwa. Tuna target kubwa zaidi. Nyie mmeshatimiza Lengo kuu lenu la kuifunga Simba msimu huu, hayo mengine ni ziada tu.
 
Wenye akili huko Yanga na Jk na Manara sr

Kwani Ahmed Ally anacheza mpira au anafundisha?
akili nini?
Wewe akili zako unazipimaje?
Akili za watu wengine unapimaje?
nani anawapima watu akili?
Yeye mpimaji ana akili kiasi gani?
Je mpimaji akili kwa wanayanga alipewa mamlaka na chuo kikuu gani kupima akili wanayanga?
Mpimaji anatumia akili ipi kuwapima watu akili?
Je lini mashabiki wa Yanga walipimwa akili?
Kilitumika kipimo gani?
Mtihani wa kupima akili ulifanyika wapi , maswali yalikuwa yapi?
Nani alitunga maswali kuwapima akili wanayanga?
Nani alisahihisha majibu ya maswali ya mtihani wa akili?
Msahishaji alitumia akili ipi kusahihisha mitihani ya akili ya wanayanga?

Je huko Kolokoloni kwenu Msimbazi mtu taahira akiropoka baada ya kushiba chipsi zege ndio mnahesabu ana akili?

Kweli Simba wengi hamna akili binafsi bali mnatumia akili za Msemaji wa Yanga kuzungumza na kutenda!
 
Mpira sio bahati ni ufundi acha uchawi kijana
 
Muulize msemaji wenu ndio alisema hayo, maana hata yeye pia hana akili. NB: aliyesema ni yeye, mi sihusiki
 
Kweli Simba wengi hamna akili binafsi bali mnatumia akili za Msemaji wa Yanga aliepumzishwa!
Sasa maswali yako yoote ya juu hapa chini we umewapima na nini mashabiki wa Simba 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣, hapa sasa ndio inaonesha HAUNA AKILI
 
Kipimo cha kumbaini mtopolo asiye na akili ni kumwangalia kisogo tu. Huwa Wanavisogo vilivyochongoka na wengine wanaomba kubadilishwa jinsi ili wamzalie Mayele

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Uyo Ahmed mnamuonea tu kwani yeye ndo anayecheza uwanjani? tatizo mna timu mboovu
 
Nyamambichi ndiyo umekuja na staili hii leo?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kwa bandiko lako hili wewe huna akili kabisaaa! Una kibuyu cha kufugia nywele na kuhifadhia makamasi mwenyewe unakiita kichwa.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…