Tangu Deception aanze kampeni yake kuhusu UKIMWI, kuna yeyote humu ndani ambaye amemuamini?


Mkuu vipimo vinavyopima anti-bodies sio hivyo tu,

Almost karibu kila kipimo kinachopima damu kinachohusisha Micro-organism kinaweza kupimwa kwa anti-bodies tunaweza kupima parasites(malaria ,filariasis kwa antibodies,tunaweza kupima kaswende kwa antibodies tunaweza kupima magonjwa mengi mengi mengi sana kwa mtindo wa antibody

Na kipimo cha antibody kinakuwa ni specific kwa asilimia kubwa na mdudu anayehusika

Mfano kama ni malaria basi vile vipimo vipo coated na material ya antibody ambayo yanazalishwa baada ya mwili kushambuliwa na mdudu

Sasa naomba tukae hapo hapo kwenye antibodies je kwanini baadhi wapimwe wakutwe nazo na wengine hapana je hii ni genotype kwa maana ya wengine ni genetic make up ya baadhi ya protein zili-undergo transcription au vipi?

Nadharia ya HIV/AIDS ngumu sana na mm huwa sikai upande wowote napenda kujadili haya mambo kwa upana
 
Mzingo
Kutokana Na maelezo yako, nataka nikufahamishe sio kila ukifanya mapenzi Na mwanamke au mwanamme mwenye ukimwi kwa mara moja utapata ukimwi, unaweza ukafanya mapenzi na mtu yoyote mwenye ukimwi na usipate maradhi ila isipokuwa kama utapata michubuko tuu hakuna kingine, na kama ukimwi ungekuwa unaambukizwa kama wewe unavyodhani basi huku kwetu africa hasingwbaki mtuu.
 
Mkuu sasa kwa nini huo ukimwi kama haupo,kwa nini ukishasex na mtu mwenye ukimwi na wewe unaupata???,i mean kwa nini unapungukiwa kinga?? na kwa nini hii peke yake ndio iwe na upungufu mwilini??? kwa nini ukisex na mwenye cancer hupati cancer ???nini kinakua kimeambukizwa??? ndugu hapo ulipo una ndugu wewe ushapoteza kwa ukimwi.....watu wafanye ngono zembe waukwae...eti ukiweza kujipatia kinga hautadhurika...hivi unajua Aids imechukua matajiri,wale wa mboga saba,wenye uwezo wa kula vizuri ,una utani eeh?
 
Yeah unawezamua sahihi kwakuwa sina background ya sayansi japo napenda sana kujifunza tena with open mind.

Moja ya Changamoto inayojitokeza ktk hili dudu hiv ni like kusingiziwa. Maana mtu ataugua malaria kuharisha neumonia nk. Ila antivodies zikionekana hasemwi anaumwa neumonia wanasema aids complication. But unakuta mtu soecifically anaumwa neumonia.

Hata tiba za watu hao mara nyingi ni lishe nzuri kuliko arv ili kuimarisha mfumo wa kinga.

Lkn pia inaonekana hakuna tofauti ya antibodies mfano wa TB na hao wanaonekna kuhusishwa na HIV
 
Endeleeni Kuota tu Na Ndoto Zenu Za Mchana Lakini Hapa Hamumshawishi Mtu Kukubaliana Na Mtazamo Wenu! Kila Siku Tunawazika Kwa Ngoma Wakaidi Kama Nyinyi.
Keep Dreaming boys.....
"Kila Siku mnawazika watu kwa Ngoma " unaweza weka tangazo LA kifo ambalo DR kaandika mfu wako kafa kwa Ngoma ?
Kama hakuna jiulize nini kilichomuua angawa laymen mnasema ni Ngoma
 
Virus visivyo na sifa kama virus wengine eeh ?
 

Mwili una mfumo wa kujikinga na magonjwa ambao uko katika aina mbili specific na non specific. Non specific, hii hushambulia vitu vigeni mara tu vinapoingia mwilini. Specific, hii inafanya kazi pale ambapo Kitu kigeni (antigen ) kipo kwenye mfumo wa damu. Kitu kigeni kinaweza kuwa kirusi, bakteria, seli ya mtu mwingine n.k. Inaitwa specific kwa sababu yenyewe inashambulia kila antigen kwa namna ya kipekee kwa kutengeneza antibodies. Antibodies dhidi ya antigen ya surua ni tofauti na Ile dhidi ya tetekuwanga na ndio maana inaitwa specific body response. Kwa point hiyohiyo HIV inapoingia mwili unajibu kwa kutengeneza antibodies ambazo tungetegemea zishambulie hivyo virusi lakini zenyewe zinashindwa. Ndio maana basi katika kupima kama una HIV wanapima hizo antibodies kwa sababu zinakuwa tayari zimeshazalishwa na cells za mwili ulio na HIV.

HIV inashambulia cells aina ya T helper (cd4) ambazo zinafanya kazi ya kupresent taarifa za antigens na kuactivate killer cells na plasma cells ili zitengeneze antibodies. Mtu mwenye VVU anakua na cd4 chache Kwahiyo uwezo wake wa kupigana na magonjwa kwa kutengeneza antibodies au kuactivate killer cells ni mdogo. Hii husababisha kushambuliwa na magonjwa mbalimbali kwa kuwa kinga ni ndogo na ndio maana mwenye VVU akipata TB wanasema ni HIV/AIDS complication

HIV denialists wengi wanapinga wakitumia point ya kuwa process za kumuisolate huyo kirusi hazikufuatwa kama ambavyo zimeainishwa na pia katika Koch postulates ili kutambua kisababishi cha ugonjwa lazima uweze kumcultivate huyo microbe Kitu ambacho wao hawaamini kama kimefanyika katika kuthibitisha kama HIV inasababisha UKIMWI. Sawa unaweza kukubaliana nao lakini mpaka hapa tulipofikia nadharia ya HIV ni bora kuliko zote kwa sababu imetupa njia bora ya kukabiliana na adui. Unaposema AIDS inasababishwa na lishe mbovu inatakiwa uwe tayari kuthibitisha hilo kwa watu wote wenye AIDS. Mimi najiuliza sana maswali haya

Antibodies zinazoonekana kwa wenye UKIMWI huwa ni dhidi ya nini kama si HIV?

ARVs zinafanyaje kazi kuboost CD4 count kama hakuna HIV?

Usisahau kwamba hizo ARVs ni effective dhidi ya hepatitis B ambayo haina ubishi kuwa ni retrovirus Kwahiyo target ya hizo dawa ni Reverse transcriptase lakini inatoka wapi kwa wenye AIDS ikiwa kisababishi sio retrovirus?

Samahani kwa reply hii ndefu
 

Sasa naomba nikushauri kitu kimoja mkuu,

Inaonekana kabisa huna elimu kuhusu huyu mdudu hata ile ya kawaida tu.

Kwa ulivyo ni rahisi sana kuwa defeated hebu acha u-bias halafu kaa chink soma vitabu vya kawaida vinasemaje na denialist wnasemaje pia

Ukimaliza njoo ujenge hoja usiokoteleze ya mwenzako deception ambaye hajafanya cha ziada tofauti na kusoma na kuangalia documentaries you tube
 

Kijibabu, kwa akili yako naomba ubadili jina. Badili kuwa lijibabu. hahahaha

Tunataka hoja kama hizi. Point zako ni very clear na umetoa hitimisho kama swali kwa wale denialist.

Wengi wa hawa denialist wanapenda kupiga kavu nje, sasa wanataka justification ya kujipa moyo. hahahha
 
Huyo jamaa viroba vikimuisha atajua anachikiandika ni pumba au la

Daud1990, huna hoja yoyote, kazi ni kutukana. Ndivyo ilivyo mtu akiishiwa hoja.

Nenda kaelewe mada husika. For the time being, tulia walio naufahamu wa ukilaza wajenge hoja. Wewe uliye na akili nyingi hapa hupawezi.
 

Ngozi Joram, Ikigundukila leo hii upo HIV positive, utapewa counselling ili uanze kutumia dawa. Kama hautaki, naomba nirudie hili, KAMA HAUTAKI! haulazimishwi kutumia dawa.

WORST CASE SCENARIO: Kumbuka utapewa dawa za mwezi mmoja au zaidi. Binadamu mwenye akili nzuri kama amelazimishwa kunywa dawa na amepewa za mwezi mzima, akienda nyumbani hatazimeza hizo dawa kama hataki, bali atazitupa.

Tulete argument zilizo na mshiko.
 
Kwani mwaka jana mwanzoni kurudi nyuma mtu alikua anaanzishiwa dawa CD4 zikifika 250 na ss hata ziwe 900 maadam umegundulika +ve unaanzishiwa. Virusi vimeadvance au?
 
[emoji2] [emoji2] niache tu nitumie hilohilo tu kwa sababu kwangu lina maana kubwa sana. Inabidi tujiulize kama Kweli UKIMWI ni lishe duni sasa kwanini balaa lake lianzie 1980s na sio kabla ya hapo, je ni kwa sababu watu walikua na lishe bora?. Na kwanini watu wenye lishe sawa mmoja apate na mwingine asipate?

Kule sauzi Thabo Mbeki aliingizwa mkenge na hawa denialists akashawishi watu waachane na ARV ila mwisho wake maelfu ya watu walikufa mpaka Mbeki akajuta kuwafahamu
 
Kwani mwaka jana mwanzoni kurudi nyuma mtu alikua anaanzishiwa dawa CD4 zikifika 250 na ss hata ziwe 900 maadam umegundulika +ve unaanzishiwa. Virusi vimeadvance au?

1. Mama mjamzito anashauriwa aanze dawa mara moja anapogundulika yupo positive ili mtoto asipate maambukizi.
2. Unapotumia dawa za ART unapunguza uwezekano wa kuambukiza mtu mwingine.
3.Unapotumia ART, unapunguza kupata magonjwa nyemelezi.
4. Utafiti uliofanywa unaonyesha kuanza dawa mapema kunampa mwathirika maisha marefu zaidi, kuliko aliye anza dawa akiwa na CD4 chini ya 200.
 

Kaka unanikosha. Natamani Deception aje. Sijui alipotelea wapi huyu ndugu. Kuna mtu mmoja anaitwa DAUD1990, akija hapa hachangii, yeye anatoa neno moja tu " kilaza" hahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…