Tangu Deception aanze kampeni yake kuhusu UKIMWI, kuna yeyote humu ndani ambaye amemuamini?

HIV virus Images - TEM

Sijui unataka nini zaidi mkuu deception. Ni kwanini ukiugua mafua huwa unaenda kutafuta dawa fasta. Ulishawahi kuviona virusi vinavyosababisha mafua?

Wewe sikiliza...virusi vya mafua vilishawahi kuonekana na vimefanyiwa isolation na purification.Isolation na purification hiyo imetumika kukifanyia kirusi hicho uchunguzi kuanzia Observation,Hypothesis,Experimention na Conlusion kwamba kirusi hicho kweli kinasababisha mafua.

Katika sayansi lazima upitie hatua hizo ili hiyo iitwe sayansi ya kweli.Sasa unaniuliza mimi kama nikiumwa eti lazima nikione kirusi hicho ndio nile dawa?Mbona swali hili halina mantiki kabisa...hiko kirusi kimeshathibitika tayari...na ndio maana wanapokipima na kukiona wanajua ndio hicho,mimi kama mgonjwa sihitaji kukiona,lakini ukweli ni kwamba kiliwashawahi kuonekana kwa kupitia procedure zote za kisayansi.

Sasa niambie,huyo HIV wenu ambaye hizo picha mlizoleta ndizo mnaziamini kwamba ni zake,amefanyiwa wapi Isolation na purification ili kujua kwamba yeye ndiye anayehusika?

Hypothesis na Conlusion ya HIV kwamba anasababisha AIDS havirandani kabisa....sasa hiyo ni sayansi ya wapi?Wewe umeona wapi katika sayansi Hypothesis na Conclusion vinapingana halafu bado watu wanang'ang'ania kuikubali tu?

Eti mwenyewe umeleta picha za HIV,halafu unajiamini kabisa kama umeleta picha za HIV!!!...he he heeeee...ama kweli suala hili ni gumu sana kueleweka...lakini ninachoshukuru ni kwamba,tayari kuna watu wengi sana wameshaelewa na nimeshawaachisha ARVs na wapo wengi ambao hawatumii kabisa ARVs..wote hao wana miaka kadhaa na hawaugui kijinga...

Hivyo basi kama wewe na jamaa zako hamtaki kuelewa ni sawa tu,si lazima niwaeleweshe watu wote....wewe unafikiri kama wote wakielewa tutapunguaje duniani?Mwisho wa siku lazima tupungue..huu ni msaada wangu kwa wengine tu ili wasije kufa kwa kusingiziwa kitu ambacho hakipo.Sasa ni hiari yako kufuatilia na kujifunza,sio lazima ujifunze.
 
Mkuu Deception, hizi findings for HIV possible cure ni gharama kubwa, kama hawa watu hawajui wanachokifanya, kwanini wapoteze pesa zote hizo? Juzi tumeambiwa Gilead ya Wadanish wamegundua orgasims zinazotoka kwenye udongo na wameona kabisa kuwa zinaweza kuungana na Lymphocytes na kuua virusi vya HIV. Kwa kuendeleza research hii dili ya 2 billion Euro ilisainiwa. Hawa watu watakuwa wanacheza pata potea na pesa zote hizo?
 
Mkuu wewe ni ignorant sana.

Unafikiri unajua lakini hujui.

Unacheza tu na maneno wala huprove chochote. Umekalia tu ulichoaminishwa na you tube.

Watu wamekuacha wee, ukaona upo sahihi kukalia you tube.

Umekalia tu isolation na purification.

Ukienda maabara kucheck ugonjwa huwa unawaambia wafanye isolation na purification?

Acha kupotosha jamii.

Credible researchers hawawezi kukaa hapa na kubishana na wewe. Ndiyo maana watu wapo kimya. Sio kwamba upo right.

Nipe credible researchers wa 2016 anayesema HIV haipo. Achana na scientist wako wa miaka ya themanini.
 


Gilead licenses Danish Bispecific antibodies for the next HIV Cure
 
Mtoa mada mbona kama huna hoja ya kutuaminisha kuwa Deception anakudanganya? Mbona humkanushi Deception kwa hoja? Kama ukimfutilia Deception kwa umakini na kuhoji jinsi hili swala la Vvu/ Ukimwi lilivyokaa Ki-ujanjaujanja basi utajua ana nia njema. Mimi nimemuelewa na nimemwamini baada ya kwenda field mitaani na kujaribu kuhoji Madaktari kuhusu Hiv/AIDS nimejifunza mambo makubwa sana. Haya mambo matatu nimeyazingatia , LIFESTYLE, MALNUTRITION, na MSONGO WA MAWAZO ndio vyanzo vya UKIMWI.
 
Mbona unapaniki mkuu.... HIV ipo bana whether you like or not, virus vya HIV vipo na vinasababisha UKIMWI. Kitu cha ku argue labda ni kwanini wanasema hakuna kinga wala tiba!? Hapo ndo penye mjadala lakini kuhusu uwepo wake kataa tu ili kubishana kwani hata walioshiriki kuvitengeneza wameshaanza kukiri! Unawasikiliza sana madaktari wa YouTube ambao nao wanamsilahi na hii kitu. Ungeingia maabara ukatest mwenyewe huenda ungesikilizwa
 
Bushman10.

Usikubali kuaminishwa fikra za mtu bila utetezi.

Hujamwelewa Deception. Anasema HIV haipo. Nimemwonyesha under electron microscope anasema hivo sio HIV.

AIDS ni ugonjwa unaosababishwa na upungufu wa Kinga mwilini. Hilo sina ubishi.

HIV ikiingia kwenye mwili matokeo yake huvamia askari wanaopambana na magonjwa yaani CD4.

Ila kama utapata virusi vya HIV ukawa unakula lishe vizuri na unameza dawa vizuri na kwa utaratibu mzuri basi utaishi vizuri.

Ila kuna wakati dawa za ARV huwa zinafeli baada ya kutumia kwa muda mrefu. Zikifeli kama utakuwa hukupata second line treatment basi uwezekano wa kupata AIDS ni mkubwa sana. Kwa maana dawa zitakuwa hazisaidii Kinga yako iwe imara.

Kwa hiyo virusi vya HIV vipo, na ukimwi upo.

Usiende peku peku kwa sababu Deception kasema hakuna HIV. Jali afya yako.

Dawa zozote sio ARV tu zina madhara. Kumbuka Tanzania tunatumia generic ARV na ni gharama nafuu. Ila kuna dawa kwa wenzetu huko ni nzuri zaidi ambazo ni brand names lakini ni bei kubwa sana ila less toxic.
 
Ukishaanza wewe jamaa ni ignorant hapo ni dalili ya kuishiwa na hoja.
Time theory.

Sina haja ya kuonekana Nina hoja.

Amesema huwezi kuviona virusi vya HIV. Nimempa andiko na picha.

Yeye anasema sio. Sasa huyo sio ignorant. Au neno ignorant unalichukuliaje mkuu?
 
Time theory.

Sina haja ya kuonekana Nina hoja.

Amesema huwezi kuviona virusi vya HIV. Nimempa andiko na picha.

Yeye anasema sio. Sasa huyo sio ignorant. Au neno ignorant unalichukuliaje mkuu?
Mjadala ulikuwa mzuri na kila upande ulikuwa ukishusha nondo,ila mkianza name calling mtaibua hisia na kuharibu utamu wote.

Japo kubainisha upande niliopo mi niko upande wa deception. Hili limetokana na tafakari ndogo tu niliyoifanya kuhusiana na jinsi mataifa makubwa yanavyohangaika kila kukicha kuhakikisha hatuamki.
 

Wewe unadharau scientist wa miaka ya themanini? Old is gold
 
Time Theory.

Umeeleweka mkuu.

Naomba nikutoe upande wa deception.

Naomba nikukumbushe. Wakati wamarekani walipopiga Bomu la nuclear pale hiroshima baadaye wali feel guilty sana. Walisaidia japan kurudi tena kwenye uchumi wao. Japo marekani haijawahi kukiri kumpa compensation mjapan lakini tunajua mchango wa marekani na shirika la SCAP kuifikisha japan hapa ilipo.

Kwanini nasema haya.

Kama kweli virusi vya HIV jamaa walitengeneza makusudi na kama ndivyo naamini viongozi wa juu wa marekani wanajua.

Basi guilt yao ndiyo inayowafanya wafanye wanayo yafanya. Kuanzia kutoa msaada kwa waathirika na vinginevyo.

Department of defense (DOD) ya marekani wana shirika lao la research kuhusu HIV lipo Mbeya.

Nakuhakikishia wanafeel guilt sana kwa sababu ya hivi virusi. Lakini sio kusema havipo.

Sent from my HUAWEI G6-U10 using JamiiForums mobile app
 
Old is gold that's why we need to know history in order to know our current situation and plans for future. We can't keep on holding the past simply because it's gold.
Asante Sky.

Siwadharau na kama sky anavyosema vitu vina evolve.

New medical machines zinakuwa invented. Vitu ambavyo tulikuwa hatuwezi kupprove, sasa tunaweza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…