Tangu hotuba ya Magufuli Chato mbele ya wakuu wa Vyombo vya Dola msitegemee kutangaziwa wagonjwa wapya wa COVID 19

Tangu hotuba ya Magufuli Chato mbele ya wakuu wa Vyombo vya Dola msitegemee kutangaziwa wagonjwa wapya wa COVID 19

Pamoja na hayo yote uliyotaja,Takwimu sahihi ni lazima!Ukweli siku zote ni jibu sahihi!
Ni kweli ulilosema maana kuna watu wenye tabia kama ya Thomas wa Biblia, ambao hawaamini mpaka waneona, ambapo wakati huo wamekuwa wamechelewa kuchukua tahadhari.

Kwa hiyo mtu asisubiri kupewa takwimu ndipo azingatie ushauri wa kiafya au kubadilika kitabia.

Huu siyo wakati wa kwenda kwenye baa, nyumba za starehe au sokoni, kuliko na misongamano ya watu. Ikibidi mtu aende huko awe amejiandaa haswa.
 
Naam,ikiwezekana kimbiza familia mbali kabisa huko kijijini ubaki unapambana mwenyewe mjini!Mimi napenda kuishi kwa vitendo na sio maneno,nimeona mkuu wa nchi kakimbilia kijijini na familia yake nami nimepeleka familia yangu yote kijijini,ikinilazimu nami nitaenda kujumuika nao!
 
Hao wenyewe waliojiwekea lockdown yamewashinda na sasa wameanza kulegeza na kuanza kufungua nchi zao wakati maambukizi na vifo bado viko juu. Baadhi ya majimbo USA wameshaanza kufungua, hali kadhalika Hispania, Italy, India nk.
Ila wanaona aibu kusema yamewashinda!
Hizo nchi ulizozitaja zote walichelewa kuikabili corona kama ambavyo Tanzania imefanya na ikafika wakati raisi wa Italy alikuwa anaongea hadi analia sasa kwa kuwa wao walikosea ndio na sisi tukosee

Nchi zilizowahi kuandaa mikakati ya kuikabili corona ni Uganda na Rwanda angalia wana vifo vingapi na wagonjwa wangapi

Angalia mipango ya Kagame na Museven kama ina fanana na mipango ya huyo wa kwako aliye enda kujificha Chato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam,ikiwezekana kimbiza familia mbali kabisa huko kijijini ubaki unapambana mwenyewe mjini!Mimi napenda kuishi kwa vitendo na sio maneno,nimeona mkuu wa nchi kakimbilia kijijini na familia yake nami nimepeleka familia yangu yote kijijini,ikinilazimu nami nitaenda kujumuika nao!
Ni wazi hata wacha Mungu wakumbuke maneno ya Yesu:-

Mathayo 24:
3 Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?

4 Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.

5 Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.

6 Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.

JILINDE UMLINDE JIRANI
 
Nahisi viongozi wetu nao wamechanganyikiwa hawajui cha kufanya, na msamaha wetu kwao ni kuwapumzisha tuu bongo zao zimechoka na wamezoea kufanya kazi kimazoea. Bahati nzuri au mbaya hili janga japo lilionekana likija na wadau wakaonya wao wakachukulia kimazoea na sasa wanavurugana, anayetaja takwimu za kweli anaonekana mwongo na anayetoa za kupika anaonekana mkweli. Tuwe na msimamo m'moja viumbe hawa wamechoka tuwapige benchi kwa muda usiojulikana, hadi akili zikiwarudi tunaweza kuwafikiria tena!!
 
Kuna siku niliandika Uzi kama Tetesi nikisema kuwa Tanzania hakuna lockdown mkaufuta licha ya kutoa sababu. The same day jioni yake mkuu akasema yale niliyoyasema, sijui aliyefuta alijisikiaje.

Sasa ni wazi kuwa takwimu halisi za wagonjwa wa COVID 19 hamtapewa, mkipewa mjue kuwa zimechakachuliwa.
Sasa ni mwendo wa bata na vifaranga wake, kila mmoja ajilinde.

Ukicheza na ukajawa na amani wakati huu wa hatari ukasahau kujilinda unakwenda
Juzi tumeona "wagonjwa" wamefanyishwa party.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ummy Mwalimu ajiuzuru ili kulinda staha yake na kujiepusha na njama za Meko.

Vinginevyo ajiandae kujibia kwa anayotufanyia sasa.

Kuna mambo ya kuafanyia mchezo ila sio uhai wa watu.
 
16:07 hrs
27/04/2020.
Any update?
Je, tuanze kushangilia kuwa Tanganyika tumeishinda corona?
Je, ilikuwa propaganda za mabeberu kuhusu corona hapa Tanganyika?.
 
Wakuu huu sio utani watu wanakufa sana na corona.
Nina rafiki zangu wengi wanatujuza maswahibu yanayowakuta yatokanayo na corona lakini hakuna wa kutangaza.
Mbunge wa Arumeru mashariki mdogo wake kafariki kwa corona na familia iko karantini.
Arusha central police kuna askari kadondoka kazini kwa matatizo ya corona na sasa usipovaa mask huingii kuhudumiwa, haitangazwi.

Matukio ni mengi mno

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnngu atuponye
 
Dah kweli watz tumepatikana. Nadhan hizi suluba kila mmoja wetu atajua kua siasa inagusa maisha yao. Ccm wanajitahid kuwaaminisha kua siasa ni mbaya na wananchi hawatakiwi kujiingiza au kushiriki kwenye siasa na haiwagusi kwa chochote.

Baada ya hili janga kwa watakaobaki/tutakaobaki ni dhahiri kabisa akili itakua imewakaa/imetukaa sawa.
 
Tatizo wakenya walimcheka jiwe wetu, alipotangaza tutegemee maombi halafu keshokutwa yake wakaripotiwa wagonjwa 84 wakenya walizomea mno. Jiwe akaona dawa yao ni kuwafunikia tu hakuna habari ya mgonjwa hapa ila ubaya wa ugonjwa haufichwagi hata siku moja na ukiuficha utakuumbua tu
 
Kumbe Wakenya ndio wanaofanya watu waambukizane kimyakimya
 
Back
Top Bottom