Tangu Kikwete alipopata Urais, CCM wakafungua geti la viwango duni katika siasa

Tangu Kikwete alipopata Urais, CCM wakafungua geti la viwango duni katika siasa

Kama humtaki rais mkatae kwenye kura au mfanyie motion ya impeachment.

Rais ambaye kazoea kucheza taarab muziki wa kwao kumkataza kucheza taarab kwa sababu ni rais ni kumuonea na kushindwa kuelewa nini kitu cha muhimu.

Taarab ni sehemu ya utamaduni wa Tanzania sehemu za Pwani, au huelewi hilo?

Unataka rais aache utamaduni wa kwao kwa sababu ni rais?
Kwani muziki wa Taarab una ubaya gani?
 
Kwani muziki wa Taarab una ubaya gani?
Basi watu wana matatizo ya kufikiri tu.

Ni tabia za watu wasioweza kujieleza kwa hoja kuchagua vitu irrelevant out of anger, chuki.

It is a failure to articulate their frustrations in a logical way.

Watu wanaona wanaonewa na serikali halafu hawana elimu ya kuchambua matatizo ya serikali kwa hoja. Hawawezi kutofautisha rais na serikali. Hawawezi kutofautisha mtu mmoja na utamaduni mzima wa watu wengi. Hivyo wanaishia kumshambulia rais kwa vitu irrelevant.

Hawawezi kujenga hoja zilizo relevant and logical.

Hapo ndiyo mwisho wa uwezo wao.
 
Tukio la Kikwete kupigiwa simu na kupewa Happy Birthday na watangazaji wa Clouds FM nalikumbuka. Yawezekana ni uelewa wetu au culture yetu, lakini halikustahili na aliyepigiwa alistahili kutokubali jambo hilo. Najua siyo rahisi kwa rais kupigiwa kama hajaulizwa na kukubali.

Nasema hivyo kwa sababu waliopiga wenyewe, walionesha wazi kwamba wako kwenye utani na rais. Rais (president) akaitwa 'Presdaa' (shame!). Ilikuwa ni kutoheshimu nafasi ya urais kwa mazungumzo na watu walioonesha uhuni wa mitaani. Tukumbuke Taifa zima linasikia. Je ni culture yetu? Au ni vizuri kufanya kama Amerika? 'Happy Birthday Mr President -Marlyn Monroe.

Hilo la taarabu nalo tusilitetee. Nini sababu ya kutuonesha rais anacheza Taarabu? Yaani naye anajua kutikisa kiuno? Hii ni Taarabu ya 2000s; Kanga moko, n.k. Mtu asiniambie eti naye ni binadamu bhla-bhla! Huyu ni rais ana majukumu muhimu aliyoomba kwa kupenda kwake, tunampa privileges zote kwa ahadi ya kutumikia majukumu. Kama anatamani kucheza Taarabu kama akina Hadija Kopa, aondoke tusiingie gharama za ulinzi kwa furaha zake.

Mkuu, Samia hajawahi kuomba Urais wala kuomba kugombea. For her everything has been coming with easy.
 
Kwa wahenga tunafahamu matatizo yaliyotokana na uongozi dhaifu wa JK.

Rais Kikwete alipoingia madarakani, alipendwa sana, na wengi wakawa na matumaini ya uongozi bora. Ilitokana na matamshi yake alipoishika wizara ya fedha juu ya Kigoma Malima aliyekuwa mtangulizi wake, na wakati huo alikuwa hapendwi kabisa!

Tatizo ikawa ni aina ya uongozi wa Kikwete. Ilitegemea urafiki, mahusiano yasiyo na mipaka na hata ngono ilionekana ni mtaji. Ni wakati ambapo nafasi za wakuu wa Wilaya ziligeuka ni nafasi za mafunzo, bila kujali umuhimu wa nafasi hiyo ktk jamii.

Wanachama wakaona kumbe U-rais ni nafasi ya kuchezea tu! Akapigiwa simu za kupewa heri ya 'Birth day*, naye akaitika akisikika nchi nzima. Akataniwa na kucheka, n.k. Baada ya hapo watu waliingia kwa makumi kuomba nafasi ya Urais.

Leo hii rais anaonekana akicheza taarabu, anaalikwa na wachekeshaji, anashikwa bega akiombewa kanisani. Kama ni hivyo, hata Ubunge imekuwa ni nafasi ya kila mtu. Mwaka huu wameomba kwa ubora wao wanaoujua, na wanagomba na kusema ni haki yao, ni wanachama. Mmoja hajui hata kazi ya Mbunge, kasema atakuwa chawa wa Serikali, na mwaziri.

Nafasi za uongozi zimepoteza hadhi yake. Ieleweke kwamba, Unapokuwa mwanachama wa chama cha siasa, haina maana kwamba unastahili kugombea uongozi wowote ktk chama au Taifa. Kila mtu ajipime nafasi anayoiweza. Ni aibu kama bunge litakuwa ni sehemu ya wachekeshaji, a.k.a wasanii. Nchi inayojigamba sasa ina vision 2050, yenye Ai ndani yake.
Unaambiwa adui mkubwa wa taifa hili ni Kikwete, jamaa hakufaa kabisa kuwa rais wa hili taifa letu. Kaambukiza kina Mama wengi virusi kwa kuwapa vyeo walivyokuwa hawaviwezi na kuharibu nchi.
 
Unaambiwa adui mkubwa wa taifa hili ni Kikwete, jamaa hakufaa kabisa kuwa rais wa hili taifa letu. Kaambukiza kina Mama wengi virusi kwa kuwapa vyeo walivyokuwa hawaviwezi na kuharibu nchi.
Watanzania wengi wanapenda sana kumtafuta mtu mmoja na kumtwika zigo lote.

Sasa huyo Kikwete alijiweka yeye mwenyewe kuwa rais katika nchi ya mamilioni yote hayo ya watu?

Mbona mnapenda sana kuruka wajibu wenu?

Ulishawahi kujiuliza imekuwaje nchi yenye watu mamilioni yote hayo ikaishia kuwa na rais kama Kikwete in the first place?
 
Alichaguliwa kabla wananchi hawakumgundua uchizi wake.
 
Alichaguliwa kabla wananchi hawakumgundua uchizi wake.
Sasa wewe huoni kuwa hapo wananchi wanaomchagua mtu kuwa rais kabla ya kumchunguza vizuri na kumuelewa vizuri nao ni tatizo?

Huoni kuwa hapo tuna tatizo zaidi ya huyo rais, hata hao wananchi nao ni tatizo?

Kikwete alikuwa na meritorious record gani ya kumfanya apewe urais?
 
Ninaposema wananchi walimchagua bila kujuwa uchizi wake ujuwe kuwa hizo kura si kama alichaguliwa na wananchi kwani CCM ni wezi wa kura zetu. Kwa miaka mingi hakuna mwananchi mwenye akili timamu anaipenda CCM.
 
Kwanza umebadilisha hoja. Kutoka wananchi wamemchagua bila kumjua, unasema wananchi hawajamchagua CCM wameiba kura.

Hizi ni hoja mbili tofauti.

Lakini tuseme kura zimeibiwa na CCM wachache.

Sasa hata hapo huoni kuwa nchi yenye mamilioni ya watu wanaoruhusu kikundi kidogo cha uongozi wa CCM uweze kuiba kura na kuwawekea rais hao mamilioni ya watu na wao wana tatizo, tatizo haliwezi kuwa kwa hao wanaoiba kura tu, hata hao wanaoruhusu kuibiwa kura nao wana tatizo?
 
Km mwalimu nyerere angelikuwa hai JK asingekuwa raisi maana alimkataa kweupe
 
Kwanza umebadilisha hoja. Kutoka wananchi wamemchagua bila kumjua, unasema wananchi hawajamchagua CCM wameiba kura.

Hizi ni hoja mbili tofauti.

Lakini tuseme kura zimeibiwa na CCM wachache.

Sasa hata hapo huoni kuwa nchi yenye mamilioni ya watu wanaoruhusu kikundi kidogo cha uongozi wa CCM uweze kuiba kura na kuwawekea rais hao mamilioni ya watu na wao wana tatizo, tatizo haliwezi kuwa kwa hao wanaoiba kura tu, hata hao wanaoruhusu kuibiwa kura nao wana tatizo?
Wewe mtu naanza kuona ulivyo na matatizo ya kufikiri. Una maana CCM wakiwa wachache, mamilioni waliobaki wana nguvu ya kuwadhibiti? Serikali inalindwa na vyombo vya usalama,nani ana amri juu ya vyombo hivyo? Au nawe unaamini mwananchi ana madaraka juu ya vyombo hivyo? Kweli hapo ndo mwisho wa fikra zako?

Huko kwenye magereza ya mamia ya wafungwa, kuna polisi wangapi wanaowadhibiti.
 
Back
Top Bottom