Mjuba og
New Member
- Apr 27, 2024
- 3
- 3
Tangu alipofariki aliyekuwa muasisi wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania, Dr. Moses Kulola, uongozi uliopewa dhamana kuliongoza kanisa hilo umeshindwa kuliunganisha kanisa hilo badala yake wamekuwa ni viongozi wanaolisambaratisha kanisa kwa mpasuko, matabaka, ukabila na kwa kuendekeza matumizi mabaya ya madaraka, rushwa, ubinafsi na uzandiki.
Mbali na hivyo kwa sasa watu wengi hawajui kuwa viongozi hawa wanadaiwa kutumia pesa kuwahonga viongozi wa kiserikali ili watumike kuwafukuza wachungaji wenye makanisa yenye hali nzuri kiuchumi ambao uongozi wa juu wa kanisa hauwataki kutokana na misimamo yao kiroho na kiufahamu, na unataka kuweka vibaraka wao wa ndio mzee ili wazidi kujiimarisha kiuchumi kutokana na mapato. Hali ni mbaya