share
JF-Expert Member
- Nov 22, 2008
- 6,063
- 10,479
Kwanza kabisa heshima kubwa iende kwa Kamanda Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA. Mbowe amefanya kazi kubwa sana kukiweka katika chati chama hiki kwa gharama ya kufilisiwa utajiri wake, kufunguliwa makesi ya hila, na kuumizwa mwili.
Kama kiongozi hajatetereka kabisa. Ni kiongozi bora kabisa wa upinzani ukanda wa Afrika Mashariki. Mwamba tuvushe. Sasa amerudi mwamba mwingine - Mhe. Tundu Lissu. Huyu mwamba tangu arudi hajapumzika.
Ni kazi kwenda mbele mpaka tunamuonea huruma. Hajali Afya yake na hasa mguu wake wa kulia uliochakazwa vibaya kwa risasi za wasiojulikana ambao kwa kweli wanafahamika. Kwake yeye kwanza ni Taifa la Tanzania.
Ujio wake na mikutano yake ya kutafuta wadhamini kugombea URAIS imekuwa na mvuto mkubwa sana, akili nyingi sana, na elimu ya uraia ya kutosha.
Kwa mtindo huu, ameipaisha mno kisiasa CHADEMA. HONGERA SANA Mhe. LISSU.
Wengine mnasemaje?