Tangu mwaka 2000, Japan imepitia AWAMU 11. Tanzania tunajifunza nini katika hili?

Tangu mwaka 2000, Japan imepitia AWAMU 11. Tanzania tunajifunza nini katika hili?

G4N

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
4,283
Reaction score
9,925
Kwa mujibu wa katiba ya Japan kiongozi mkuu wa executive ni waziri mkuu.

Tangu mwaka 2000, Japan imeongozwa na mawaziri wakuu 11, kati ya hao 8 wameongoza chini ya mwaka 1 na nusu.

1. Yoshiro Mori: 5/4/2000 - 25/4/2001
Sawa na mwaka 1 na siku 22
2. Junichiro Koizumi: 26/4/2001 - 26/9/2006
Sawa na miaka 5 na siku 154.
3. Shinzo Abe: 26/9/2006 - 26/9/2007
Sawa na mwaka 1 na siku 1.
4. Yasuo Fukuda: 26/9/2007 - 24/9/2008
Sawa na siku 365
5. Tarao Aso: 24/9/2008 - 16/09/2009
Sawa na siku 358
6. Yukio Hatoyama: 16/09/2009 - 08/06/2010
Sawa na siku 266
7. Naoto Kan: 8/6/2010 - 2/9/2011
Sawa na mwaka 1 na siku 87
8. Yoshihiko Noda: 2/9/2011 - 26/12/2012
Sawa na mwaka 1 na siku 116.
9. Shinzo Abe: 26/12/2012 - 16/9/2020
Alirudi tena kwa mara ya pili akaongoza kwa miaka 7 na siku 266.
10. Yoshihide Suga: 16/9/2020 - 4/10/2021.
Sawa na mwaka 1 na siku 19
11. Fumio Kishida: 4/10/2021 - hadi sasa

Sababu kubwa za awamu kubadilika haraka haraka ni mbili;-
1. Kushuka kwa kukubalika na wananchi (fall of approval ratings). Mjapan akisoma negative comments mitandaoni kuhusu yeye siku 2 tu anajiuzulu.

2. Kushindwa uchaguzi. Mjapan akishindwa uchaguzi, kabla hata ya kumaliza kuhesabu kura anatangaza kushindwa.

My take:
Siyo hapa kwetu Tanzania mtu anakaa madarakani muhula wa kwanza halafu wenyewe kwa ujinga wetu tunaanza kuomba aongezewe muhula mwingine (maarufu kama mitano tena). Halafu anaondoka madarakani anakabidhi nchi kwa jamaa zake.

Ebo! Ikulu kusiwe mahala pa kuishi kwa uhakika wala mazoea.

Kama mtu analitendea haki taifa sawa. Lkn siyo kwasbb za kinafiki na kizandiki
 
Japan Wana roho ndogo mno, sio kila kitu unacopy na kupaste!
 
Wenzenu tayari wana mfumo mahili unao ongoza taifa, nyie mnategemea mtu mmoja anaejiita chief wa machief ndo aamue msitakabali wa taifa.

Africans are poor because they are very poor.
 
FB_IMG_16325697095989360.jpg
 
Hoja fikirishi mkuu, hata ulaya na dunia hatimae ilipata maendeleo kwa watu kuhoji the status quo ndipo yakazaliwa mapinduzi ya kiitikadi, kiimani na baadae ya kisayansi na viwanda. Tusipokaa pembeni na kujihoji desturi zetu hatutabadirika kamwe.
 
Siyo hapa kwetu Tanzania mtu anakaa madarakani muhula wa kwanza halafu wenyewe kwa ujinga wetu tunaanza kuomba aongezewe muhula mwingine (maarufu kama mitano tena). Halafu anaondoka madarakani anakabidhi nchi kwa jamaa zake.
Yanayoomba kuogeza muda niyatukane sijui tusi gani, ngoja nitafute namna ya kuliweka lakini lipo "zuri" tu
 
Kwa mujibu wa katiba ya Japan kiongozi mkuu wa executive ni waziri mkuu.

Tangu mwaka 2000, Japan imeongozwa na mawaziri wakuu 11, kati ya hao 8 wameongoza chini ya mwaka 1 na nusu...
Hayo huwa yanafanyika kwenye jamii ya watu waliostaarabika, na yanafanywa na viongozi waliostaarabika.

Kwetu hapo, unakuta mtu primitive kabisa, ambaye utofauti wake na ng'ombe au nguruwe, zaidi ni kwenye umbo na uwezo wa kuongea, anapewa uongozi. Unategemea nini kutoka kwa mtu kama huyo? Na hao ndio wapo tayari kufanya kila aina ya uchafu including kuua ili tu abakie madarakani.

Hapa kwetu tuna viongozi wengi ambao ni primitive, CCM kimekuwa chama primitive kwa sababu viongozi wake wengi, wanachama wake wengi na wapenzi wake wengi ni primitive. Hawa wapo tayari hata kuua, kujeruhi, kuiba kura, ili tu wabakie madarakani.

Tanzania haitapiga hatua na kubadilisha maisha ya watu kuyapeleka kwenye ubora, mpaka tutakapokuwa na civilized leaders and civilized political party in power.
 
Hayo huwa yanafanyika kwenye jamii ya watu waliostaarabika,
Hapa ndipo kwenye tatizo kubwa Sana. Wakati wa uchaguzi jamii haielewi umuhimu wa kampeni na maana yake.

Wengi wanafata mkumbo bila ya kufanya takafakari yoyote kuhusu madhara ya kuwachagua wahuni.
 
Hayo huwa yanafanyika kwenye jamii ya watu waliostaarabika, na yanafanywa na viongozi waliostaarabika.

Kwetu hapo, unakuta mtu primitive kabisa, ambaye utofauti wake na ng'ombe au nguruwe, zaidi ni kwenye umbo na uwezo wa kuongea, anapewa uongozi. Unategemea nini kutoka kwa mtu kama huyo? Na hao ndio wapo tayari kufanya kila aina ya uchafu including kuua ili tu abakie madarakani.

Hapa kwetu tuna viongozi wengi ambao ni primitive, CCM kimekuwa chama primitive kwa sababu viongozi wake wengi, wanachama wake wengi na wapenzi wake wengi ni primitive. Hawa wapo tayari hata kuua, kujeruhi, kuiba kura, ili tu wabakie madarakani.

Tanzania haitapiga hatua na kubadilisha maisha ya watu kuyapeleka kwenye ubora, mpaka tutakapokuwa na civilized leaders and civilized political party in power.

nafikiri tunahitaji civilized society, unakosea saana unapowanyoshea CCM peke yao kama primitives wakati ukweli ni zaidi ya 70% ya watanzania ni primitive..

tukiendelea kuamini CCM peke yao ndio primitive nakuacha ukweli kwamba we are all uncivilized tutakuwa tumekosea sana..

Tukumbuke pia hawa tunaoona leo hii ni civilized wamepitia hatua nyingi sana miaka mingi nyuma huko kuanzia hiyo primitive stage, ujuaji na kuuana mpaka leo kuwa kama civilized society...hawa tunaoona leo hii civilized kuna watu huko nyuma walisacrifice ili kufika hapo..

Wote au wengi tungekuwa civilized sidhani kama tungeongozwa na hii tunayoita primitive society, naamini wote ni maprimitive ndio maana hata ukitoa mtu upinzani ukapeleka huko CCM ni yaleyale mfano Dr Slaa, Polepole, Kabudi, Msando, Dogo janja wa Arusha, Komu ,Silinde na wengine weeengi....The whole society is primitive, inawezekana ndio stage kuelekea civilization..
 
Chief, Japana ni superpower toka zama hizo kabla hata WW2....Japan anamiliki Aircraft carrier kabla hata 1945 unafananisha na watu waliokuwa utumwani zama hizo na kupata uhuru 1961....wenzetu ni Kenya, Zambia, Malawi, DRC, Msumbiji nk..
 
Back
Top Bottom