Tangu Mwaka 2017 naishi Mkoa tofauti na mke wangu sababu ya kukosa uhamisho kazini, ndoa yangu ipo shakani

Tangu Mwaka 2017 naishi Mkoa tofauti na mke wangu sababu ya kukosa uhamisho kazini, ndoa yangu ipo shakani

Anonymous

Senior Member
Joined
Apr 6, 2006
Posts
131
Reaction score
379
Ndugu zangu JamiiForums Habari zenu! Nimeona chapisho lenu kuhusu uhamisho, limeniumiza sana ndugu zangu.

Kwa nini nimeumia? Napitia changamoto kama hiyo, mimi pia mke wangu ni muajiriwa (Mwalimu), tangu nifunge naye ndoa Mwaka 2017 mpaka leo (Julai 2025) tunakaa mikoa miwili tofauti.

Hili tatizo limesababisha mpaka ndoa yangu kuingia kwenye hali ya sintofahamu, Uhamisho umekuwa kikwazo sana hali inayoniumiza, sasa hivi tuna Watoto wawili, lakini nimepata Mtoto mwingine nje ya ndoa na hili mke wangu hajui😭😭 sijui hata nifanye nini!

Andiko analozungumzia Mdau hili hapa ~ Tuambiwe, Mwalimu kupata uhamisho ni Sh ngapi ili tulipe. Inachosha kusubiri majibu kutoka TAMISEMI bila maelezo yanayoeleweka
 
Hili jambo ni hatari sana! Serikali ingelichukulia kwa uzito sana! Huwa nawaza sana inawezekana mke na mme wanakaa mikoa tofauti wanawezaje kujidhibiti dhidi ya dhambi ya zinaa???? Mungu akusaidie ndugu lakini ukweli uhamisho ungelenga wanandoa zaidi! Kwa mazingira haya watu wengi wataenda motoni kwa dhambi ya uzinzi!
 
Unauhakika gani kama mkewako hajui? labda ilivokuwa huyo alokupigia alitaka kumwaga nje, alivochomoa tu mkeo akawahi kuishika akairudisha wazungu wote ndani.

Halafu unakuja kusema hapa mkeo hajui, hivi unatuchululiaje?
 
Hili jambo ni hatari sana! Serikali ingelichukulia kwa uzito sana! Huwa nawaza sana inawezekana mke na mme wanakaa mikoa tofauti wanawezaje kujidhibiti dhidi ya dhambi ya zinaa???? Mungu akusaidie ndugu lakini ukweli uhamisho ungelenga wanandoa zaidi! Kwa mazingira haya watu wengi wataenda motoni kwa dhambi ya uzinzi!
Serikali inapeleka watumishi kwa mahitaji sio kuangalia familia yake , kuna shule ukifika huko unakuta watu wamehama sana mpaka kuna shida za watumishi ...Ukweli ni kwamba mkubaliane na hali halisi la sivyo mmoja aache kazi.
 
Mkuu pole sana na changamoto unayopitia ila ukweli ni kwamba hiyo changamoto wanapitia watu Wengi sana katika Nchi yetu

Ila ifikie hatua tuujue ukweli kuwa katika Nchi yetu ukitaka vitu muhimu uvipate kwa njia ya Halali utataseka sana

Kama wewe kwako jambo unaliona ni la umuhimu mkubwa fight kwa kutumia njia zingine na utalimaliza kuliko kuendelea kudai haki yako

Kama utaendelea kusubiri mfumo ndio ukuhamishe ili uwe karibu na mkeo basi utakuja kukutana na mkeo kipindi cha kudai taraka, Jiongeze Mkuu
 
Huu ni uzembe na kutojali kwa upande wa serikali. Haiwezekani wanandoa wake mbali mbali miaka yote hiyo na familia inaathirika.
Hapa pia mh waziri Gwajima aangalie hili na asaidie kujadili na utumishi sababu familia inateseka kwa kitu kina suluhisho.
 
Migogoro mingine kwenye Ndoa inasababishwa na serikali
Hivi kwel tunataka kuwa taifa imara lenye maadili alf tunaruhusu Long distance family
 
Serikali inapeleka watumishi kwa mahitaji sio kuangalia familia yake , kuna shule ukifika huko unakuta watu wamehama sana mpaka kuna shida za watumishi ...Ukweli ni kwamba mkubaliane na hali halisi la sivyo mmoja aache kazi.
Sio kweli. Mbona wanaohonga wanahama? Na wengine ni kwa sababu zingine na si ndoa?
 
Ungeomba ushauri mapema, tungeuliza dini yako na maandiko tukufu yanasemaje huko kwenu kabla hujapata mtoto wa nje alafu tungekuambia muachishe mkeo kazi mvute karibu mpe biashara ili wengine wenye sifa waajiriwe maana huwezi mtumikia Mungu na mali ila usimtese mkeo.
 
Ni njia haramu hiyo ,kwenye kazi kunaangalia uhitaji
Mbona Mimi nimeomba sehemu watu wengine wanakimbia lakini nazungushwa? Lakini wengine wakitoa rushwa wanahama. Uzuri watumishi hawana siri, akitoa hela anasema na ukitaka akuunganishe anakuunganisha
 
Hao watoto kapime DNA kama hutaki pressure piga kimnya!
images (3) (5).jpeg
 
Mbona Mimi nimeomba sehemu watu wengine wanakimbia lakini nazungushwa? Lakini wengine wakitoa rushwa wanahama. Uzuri watumishi hawana siri, akitoa hela anasema na ukitaka akuunganishe anakuunganisha
Ishu ya familia na mwenza ni nyeti ila kuna sababu nyingine ,mkikimbia wote huko kwingine atabaki nan? Utakuja kuelewa ..kwanza ,nyie wengine hata mtoke huko bara bado mnataka kuishi Dar sijui mna tatizo gani
 
Back
Top Bottom