Tangu nimeanza kupiga mazoezi badala ya kupungua naongezeka uzito

Tangu nimeanza kupiga mazoezi badala ya kupungua naongezeka uzito

mwenzenu tangu nianze jogging nakimbia km takibani kumi kila week, na push-up 200 kila siku, cha ajabu kilo badala zipungue ndo zinazidi; sielewi nkosea wapi, stumii supu, bia wala soda na chakula changu kikubwa ni ugali Wa dona .
malengo yangu nataka zipungue!
Mkuu 10 km kwa week bado chache sana. Fanya kuongeza juhudi. Mimi binafsi nakimbia mara 3 kwa week na ni 15 km kwa siku.
 
Kunywa maji ya vuguvugu especially morning, usitumie mda mwingi kulala, Epuka kulala ukiwa umeshiba, ruka Kamba sana, pia kuna zoezi kama la kuruka matairi hivi kama utakua unafanya lile within a week utapunguza kgs then pia kata tumbo sana
Push ups & squats piga kawaida tu sababu havipunguzi uzito
sawa mkuu
 
Mtu unapiga mazoezi ikifika jioni unaenda kula nyama choma na kupigilia balimi utapungua wapi, pathetic kabisa nonsense 6.4Kg
Mnahangaika bure na hizo fitness staili zenu,ukishakuwa na uhakika wa msosi tabu za ubonge na nyama uzembe zinaanza.Penda kutembea kwa miguu au kutumia baiskeli mda mwingi la sivyo mtapata tabu sana hapo bado hao watoto wenu wa huko dar wenye vitambi sijui itakuaje
 
Ugali wa dona unanenepesha sana. Fanya mazoezi then, asubuhi pata chai sukari kwa mbali na mayai + mkate vipande 2 ( mimi asubuhi sinywi chai au natafuna tango tu. Mchana kula kidogo sana kutuliza njaa( sio kushiba, mboga mboga zikiwa nyingi sio wanga). Usiku kula matunda tu ( mimi natafuna tango au nalala bila kula) kwa muda wa week 3 nimepungiza kilo 3 kutoka 78 to 75.
duu huu mlo tunaofanya kazi ngumu hautafai yaani ule hivyo halafu kesho ukabebe zege
 
Mnahangaika bure na hizo fitness staili zenu,ukishakuwa na uhakika wa msosi tabu za ubonge na nyama uzembe zinaanza.Penda kutembea kwa miguu au kutumia baiskeli mda mwingi la sivyo mtapata tabu sana hapo bado hao watoto wenu wa huko dar wenye vitambi sijui itakuaje
tukianza Kupishana na baiskeli wote huko mtaani cjui itakuwaje
 
Potezea wali, ugalo, chipsi na vyakula vinginevyo vya wanga badala yake kula matunda, na mboga za majani kwa wingi pamoja na nyama na mayai ..usipopungua nitafute ntakupa millioni 1
 
Push up Hazina msaada kwenye kupunguza uzito angalau jogging, Fanya mazoezi ya aerobics, punguza misosi ya mafuta na wanga, kama utaweza tumia juicy ya limao angalau Mara moja kwa siku na ukisha kunywa tulia walau dakika 5 ndio uanze kunywa maji walau Lita moja na nusu, hiyo no kwa asubuhi, jioni tizi la nguvu usisahau kuruka kamba walau 450 yaani set 3, kila set ruka 150, Fanya mazoezi angalau 4 days kwa siku, siku mbili pumzika, kila mwezi utapungua walau kilo tatu, mazoezi yanasaidia kupunguza mwili kwa 35%, 65% msosi.
Watu wengi hawaelewi kuwa key point ya kupungua uzito kwa 80% ni chakula. Unakuta mtu snajiumiza kwa mazoezi magumu halafu akimaliza anaenda kula sahani ya wali iliyojaa full, kwa staili hii hta ufanye mazoezi kwa miaka 200 hutopungua kamwe !. Ukitaka kupungua na upo serious cha kwanza potezea wanga, ninaposema wanga namaanisha wali, ugali ,chapati, mkate, mandazi , na pia kaa mbali na sukari. .....ukiacha kula wanga sometimes unaweza jihisi km homa hyo ni kawaida. Sasa jikite kwenye kula mayai, nyama, na mboga za majani na kuhusu matunda epuka matunda yenye sukari nyingi kula sana parachichi na tango , tikiti maji n.k fuata hii programm nakupa guarantee utapungua hadi utashangaa!!! na hii ni bila kufanya zoezi hta kidogo
 
Potezea wali, ugalo, chipsi na vyakula vinginevyo vya wanga badala yake kula matunda, na mboga za majani kwa wingi pamoja na nyama na mayai ..usipopungua nitafute ntakupa millioni 1
sawa mkuu nimescreen shot kabisa, lakini kwenye ugolo hapo umebug stumii
 
Back
Top Bottom