Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

Mi nishakuwaga muwazi, nimemwambia kabisa mtu wangu mimi niko hivyo akiona hawezi Aende atafute mtu mwingine aoe sina cha kupoteza mimi.
Kwa uandishi wako inaonyesha nyuma ya keypad wewe ni mtu wa majuto makubwa ambayo chanzo chake ni mtindo wako wa maisha ujanani..

Olacle anaendelea kusema:- "huna Mme ila una mshakaji/washikaji ambao unajua fika muda wowote wataondoka(kukuacha) kama wale wengine walivyoondoka"...hali hiyo imekufanya uwe MBINAFSI na mtu wa kujihami hasa pindi upatapo mpenzi(hawala) ukimbilia kutapanya mali ZAKE ukijua fika kuwa "hata usipotapanya pesa zake bado Atakuacha tu" .

HATIMA YAKO.
nimechunguza na kuangalia, olacle anasema" huta kuja kuiona amani furaha maishani mwako labda nyuma ya keypads".

THIS IS WHAT I HAVE SEEN
 
mkuu tuliza mshono we ulitakaje aingie kichwa kichwa
 
Hivi hicho Cha Mwanamke ambacho hakitegemewi huwa kinaliwa na nani?
 
Mi nishakuwaga muwazi, nimemwambia kabisa mtu wangu mimi niko hivyo akiona hawezi Aende atafute mtu mwingine aoe sina cha kupoteza mimi.
Inaonekana umetoka kwenye familia masikini sana! pole!!
 
Mungu atuepushe mtu wa aina yako kwenye familia yetu, kwenye ukoo wetu hata kwenye kizazi changu.... Mtu asie kuwa na msaada kwa mumewe hapana kwakweli.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Msaada gani unataka zaidi ya kukuzalia watoto, kuwalea na kukulea wewe mwenyewe na mimeno yako 32?.
Ikitokea siku mwanaume akabeba mimba japo dakika 5 tu (akanisidia hilo) basi nitamsaidia kuhudumia familia.
Vinginevyo apite kushoto.
 
Naona mungu mdogo umefufuka sasa kumuelezea mtu usiyemfahamu hongera sana.
Tafuta pesa Acha kuogopa majukumu.
Wanaume mmeumbwa kupambana OVA.
 

Kubeba Mimba kwa Mwanamke ni swala la kibiologia wala usitake kutisha watu na Mimba, weww ukiaambiwa usimamishe Kama Wanaume tunavyo simamisha utaweza?
 
Hahahaha...hakika
 
Mkuu napitia hali kama yako kikazi ila nashukuru mke wangu ananiheshimu zaid ya awali, ananiseidia hata ki psycholojia
Kwa kweli namshukuru sna .......

Kuna mahali umefanikiwa kumkontro, umepashika sawa sawa na pia inahitaji hekima za ki Mungu.

Niliwahi pitia Hali hiyo miaka mwaka 2014. Tena nikiwa mkoa tofauti na alipo wife, ikabidi nirud nyumbani(aliko wife na watoto)

Wife alikuwa mwelewa Sana, tulikuwa na mashamba tumelima viaz mviringo, tulipovuna na kuuza wife akasema hiyo hela Kaa nayo ikusaidie wakat unaangalia Raman za Kazi, milion 9.5, nikawwka Kwa akaunti.

Nilitumia kuendesha familia na kuangalia Ramani had mambo yalivtokaa POA.
 
Wanawake wa kizazi hichi ni umiza kichwa, hapo anaona hauna future tena alikuolea kazi.
Kuna aina mbili za mke...
1. Mke mke, huyu atakuwa na wewe katika hali zote unazopitia, atakucover kwa vingi ili usiyumbe, msikivu na anakuheshimu.

2. Mke jina, aina hii ya mke ndo Kama mke wa ndugu yetu mleta mada hi, ukiyumba nae hana habar na wewe, kibur kinakuwa dhahiri, hakustiri. Yuko radhi kuwambia mashoga zake na mahawara zake. Hawa wapo wengi Sana.
 
Ahahahaaa..!! Katika ubora wako
 
Mimi hii nadharia siiamini, eti kwa vile msambaa nioe msambaa mwenzangu, au mpare mwenzangu. Kwanza dada zangu siwakubali kabisa when it comes to marriage life..
 
Mkuu Kama una shamba la kulima jikite huko, amka asubh nenda shamba/bustanini piga Kazi jioni au mchana rudi maskani.

Kilimo kinaweka heshima nyumbani, Mimi mpaka leo nalima na Kazi ya ofcn nafanya, tangu niyumbe kilimo kikaniokoa sijaacha
 
nme

nilifikiria hili ila mimi haiba yangu ni ngumu sana kujichanganya na watu na watu niaoweza kujichanganya nao wengi wanakuwa kazi zao mchana
Mzee maisha ni vita weka haiba pembeni. Hiyo haiba haita kuletea mkate kwa meza. Kwa sasa kama unarafiki alie jiajiri mfate na muelekeze hali yako halisi sisi wanaume tunaelewana....kama ni fundi muombe hata uwe saidia fundi uwe unatumwa tumwa kuleta spana hii itakufanya upate na kufanya na kuwa busy huku ukiendelea kusikilizia michongo ya haiba yako.

Trust me mimi mke wangu hata kama nina hela hapendi kuniona ninazagaa nyumbani
 
Pole Mkuu, ndio ukubwa na darasa pia,asante kwa Ku share.

Mimi pia dharau hizo nishaletewa kisa uchumi Wangu mdogo umeporomoka baada ya kupata matatizo na polisi, hakua mke(sijaoa), kimada wala hawara, unadhani Nani? Mama Yangu mzazi, alikua ananiona SHABA TU Sina mipango, goi goi.
 
vumilia kuna kitu Mungu anataka kukuonesha, wewe jitahidi sana kutafuta kipata, fanya kazi yoyote ile mradi upate pesa.
 
Mkuu Kama una shamba la kulima jikite huko...amka asubh nenda shamba/bustanini piga Kaz jion au mchana rud maskan...kilimo kinaweka heshima nyumban..Mimi mpaka leo nalima na Kaz ya ofcn nafanya..tangu niyumbe kilimo kikaniokoa sijaacha
Mkuu wwe haulimi,sema unalimisha, yaani unawalipa vibarua wakufanyie kazi zako za shamba!!
 
Ahahahaha,

Nilishawaambia kuwa musioe wanawake ambao wanashinda maofisini.

Masaa 9 anakodoleana macho na mwanaume mwingine kila siku huku wewe unakutana naye masaa 2 tu nyumbani tena mkiwa mmechoka.
Wanaliwa kweli kweli.

Sasa kwakuwa ameona umeishiwa anakufanyia vitimbwi ili muachane.
Ungemwoa darasa la saba mama wa nyumbani sasa hivi ungeomba kwa washkaji laki 2 ungempa ya mtaji wa genge mngeshinda gengeni kwa furaha zote huku mnamake pesa na kusikilizia michongo mingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…