Tangu Soka lianze hadi leo hii, Kuna Mchezaji yeyote aliyefikia kiwango cha Maradona au Messi?

Bora umewachana live,,maan hatuwaelewi wanataka nini,,au wenzetu siyo ridhiki
 
Umeanza kufuatilia mpira juz,,angalia clip za zaman na za sasa utaona magoli yap ni magumu
By ma side ronaldinho,zidane ndo the best player forever
 
Mkuu kuna garrincha, ferenc puskas, Pele nascimento,zico na wengine wengi ...... ukiangalia zile classic videos za mechi zao utaona hawa jamaa hawana mfano mpaka sasa

Mkuu ingia you tube umuone mzee Diego alafu uje na feedback hapa, huyu mshkaji huwa hazinikifu videos zake. Ukija kwa mtaalamu asiyefananishwa na michezaji mingine huyu si mwingine bali ni N0 10 original na ameitendea haki hii namba/ Messi, huyu muungwana kama humfatilii basi nakushauri ingia youtube ujionee hana mfano wake/Na hawana mfano wake wawili hawa.
 
Usichanganye hisia na kazi
 
😛😛Mkuu Watapata wapi facts...ukweli utabaki pale pale,wanajua yupi mkali wa soka ila hawataki kusema tu, maradona na messi kitu ingine hakuna wakuwakamata wafalme hawa
Unachanganya hisia na kazi ww
 
Diego maradona kilichomkosesha heshima yake ni nidhamu

Yeah ni kweli kamanda wangu. Ila nitashangaa mtu anakuja hapa anasema hakuwa bora kwa sababu ya drugs😀😀 na kupelekea kusema wachezaji wake bora wa muda wote fulani na fulani na kumuweka pending huyu jamaa, simuelewi aise.
 
Mimi sijapata ona level za JUAN PABLO ROMANO RIQUELME

Huyu mshikaji alikua mtamu sana enzi zake na alifananishwa sana na Zinedine zizo namna ya ukokotaji, kwakweli alikua ni elegant playmaker,anakokota mabeki na ni mpigaji free-kick mzuri sana, na vitu vingi tu alikua akivifanya ndani ya uwanja, ila hawakumtendea haki ipasavyo, na alistahiki kupewa best player wa mwaka hata mara mbili, ila haikua hivyo..badala yake akawa wa pili enzi hizo, kitu ambacho kinastaajabisha kwakweri.huyu jamaa kanisikitisha muno bac tu.

Mcheki hapa.
https://www.google.com/url?sa=t&source=web&rct=j&url=https://m.youtube.com/watch?v=SteRrVX9gjY&ved=0ahUKEwisnYr2_fPSAhVJuBoKHRq3Dis4ChCjtAEIKjAJ&usg=AFQjCNFw9YofgQnO9P14g9Q6pMt5aJtlzg&sig2=4Fxf6GCKD8492FK4wFGaOQ
 
Wachambuzi wa soko wa kimataifa wengi wanaamini Ronado De Lima alikuwa mtu mwingine kabisa,
 
mkuu chenga sio kila kitu kwenye mpira wote tunajua huyo messi kafika hapo sababu ya wanaomzunguka wakiwemo midfield nzuri sana ya barca na argentina pia imejaa masuperstar...... huyo maradona pia alicheza kipindi wakiwepo malegends kma mario kempes kina ariel ortega sijui redondo.. batistuta etc so sio kweli aliibeba timu yeye binafsi je unawakumbuka kina buruchado na valdano??? by the way alijiunga na argentina ambayo ilikuwa imetoka kuchukua kombe la dunia 1978 so alikuta imejaa majembe kwelikweli hyo hoja haina mashiko

sasa turudi kwa pele huyo jamaa unajua assists alizotoa je huyo maradona au messi wanaweza fikia??? hvi unajua world cup ambayo pele aliumia 1966 si timu iliishia kutolewa je angekuwa anategemea wenzake si wangeendelea hadi kuchukua kombe bila pele??? hivi unajua baada ya pele kustaafu ilipita miaka mingapi hadi wakachukua kombe tena la dunia??? mbona kabla ya pele kuingia timu ya taifa brazil na mastaa wao wote kma didi wa mwaka 50 worldcup hawakuchukua kombe la dunia??? club yake ya santos pia unajua tofauti ya kabla hajajiunga na baada ya kujiunga??? kma nao alikuwa anategemea supportive players kma ambavyo messi aliwategemea kina xavi na iniesta au maradona ambaye alijiunga na argentina ikiwa tayari bingwa mtetezi wa world cup hivyo ilikuwa na superstars pekee????

MKUU HAO MESI NA MARADONA WALIKUTA TIMU ZAO ZIPO ON TOP OF THE WORLD ILA PELE ALIPOINGIA NDIO ILIKUWA MWANZO WA SUCCESS WA TIMU ZAKE BOTH SANTOS NA BRAZIL
 
mkuu nimeshuhudia clip za pele..... kumbuka hata clip za Didi wa brazil 1950 world cup zipo sana na zinaonyeshwa sana ESPN Classics na hta kwa statistics huyo messi ni sh**t kwa pele..... kumbuka pele ana magoli zaidi ya 1350 ambapo messi hajafkia hata nusu ssa how dare umlinganishe na pele..... pia pele ametoa assists nyingi kuliko mchezaji yoyote kwenye historia ya mpira..... pia pele kumbuka alicheza kipindi ambacho mpira haukuwa publicised sana kma ssa yaani matuzo sijui pesa nyingi hivyo naamini angecheza miaka hii angechukua tuzo kuliko hata huyo dogo wenu.....pele ndio mtu aliyeshinda zaidi tuzo ya juu zaidi kwenye mpira inaitwa FIFA ORDER OF MERIT AWARD na pia kumbuka kwa kura za karatasi ndio Alishinda PLAYER OF THE 20TH CENTURY ssa ina maana hao waliompigia kura walidanganya??? au hawamjui kuliko sisi tunavyomjua???? embu tuweni serious

unajua hata alexander the great ndio best ever general in the history of warfare ila je nani kati yetu alishawahi muona??? kwani ili kitu kiwe better lazma ukione?? ila ushahidi wa watu waliomuona wakati ule inatosha kutuaminisha how influencial he was kwenye uwanja wa soka!!!

PELE HAJAPATA MPINZANI BADO hizo highest stats bado hakuna aliyezifikia so kutoa mifano ya la liga haina mantiki
 
Dinho ni soccer megician hajawahi tokea duniani mwingine kama huyu.
 
Dah mkuu umeongea asee,binafsi namkubali De lima kwasabb ni mchezaji alokua amekamilika kila idara,mshambuliaji asiyeogopa mabeki anawapeleka anakotaka
 
Mesi kachezea kikosi bora, mess bila iniesta hakuna viwango! Yupo kwenye class A lakini siyo best player of all times!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…