Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,718
- 3,465
Mkuu ni kosa kubwa Sana kutoshiriki, maana ingekuwa hivyo magufuli asingeshiriki kuomba kugombea kipindi kile kupitia Ccm, hata wewe hapo ulipokaa unakumbuka na kufaham kuwa magufuli aliingia kwenye kinyanganyiro akihisi kuwa hawez fanikiwa yeye mwenyewe alihisi hivyo na wewe na Mimi na huyo uliekaaa nae hapo pembeni alijua hivyo, Hakuna aliejua kuwa magufuli angekuwa rais, asilimia Mia waligawanyika Kwa membe na lowasa Lakini hawakupita akaja kuwa magufuli, ninachotaka kukuambia kuwa ajue kesho yako ni MUNGU pekee, lolote linaweza kutokea hapo katikati, MUNGU ni Mkubwa kuliko binadam kwenye dhuluma iliyoko mbele, huwa anaiona mbele kabla Ya wewe, maisha Ya binadam na mfumo wa uongozi MUNGU huwa anaujua kabla na sisi huwa tunaangalia recorded iliyokwisha chezwa Akiwa anaangalia MUNGU
Kutokuwa na uhakika wa kushinda ni kitu kimoja na kujua haki haiwezi kutendeka ni kitu kingine. Kama Magufuli angekuwa na mashaka juu ya haki kutendeka bila shaka asingeshiriki hata kwenye hicho kinyang’anyiro!
Ni Tanzania pekee ambako utakuta mtu anashiriki uchaguzi akijua kwamba asiposhinda yeye, basi uchaguzi haukua huru na wa haki! Huo sio uchaguzi!