Uchaguzi 2020 Tangu Tanzania ipate Uhuru, kwa mara ya kwanza CCM inaenda kutumia nguvu nyingi kufanya kampeni


Kutokuwa na uhakika wa kushinda ni kitu kimoja na kujua haki haiwezi kutendeka ni kitu kingine. Kama Magufuli angekuwa na mashaka juu ya haki kutendeka bila shaka asingeshiriki hata kwenye hicho kinyang’anyiro!

Ni Tanzania pekee ambako utakuta mtu anashiriki uchaguzi akijua kwamba asiposhinda yeye, basi uchaguzi haukua huru na wa haki! Huo sio uchaguzi!
 
Hapo wanatengeneza mazingira ya wizi wa kura. Itakapolalamikiwa kuwa wizi mkubwa wa kura umetokea, wao watadai wamepata kura nyingi kihalali ushahidi ikiwa ni kampeni ya nguvu waliyoifanya.
 

Kwani mkuu wewe unaisha wapi? Inaonekana huijui vizuri hali ya democracy ndani ya vyama vya kisiasa vya Tanzania. Kwa ujumla iko chini ya kiwango. Na ndani ya vyama vya upinzani ndiyo kabisaaa (katiba ya chama, miongozo na kanuni zote ni formality ya kisheria na kwamba matakwa ya kiongozi mkuu wa chama ndiyo katiba, miongozo na kanuni zinazoendesha chama)!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…