Tangu utekaji uanze sijawahi kuona mpango kazi wa kuzuia watekaji; Wengi wetu tunalaani badala kuja na suluhisho kama hivi

Tangu utekaji uanze sijawahi kuona mpango kazi wa kuzuia watekaji; Wengi wetu tunalaani badala kuja na suluhisho kama hivi

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Kila sehem tunalaani! Tunalaani! Tunalaaani!

Yaani sisi afrika hatujui mambo mengine yanahitaji vitendo!

  • Jeshi la polisi linalaani...
  • Mashejh wanalaaani...
  • Waziri analaaani...
  • Wachungaji wanalaani..
  • Wananchi wanalaaani..
  • Bunge linalaaani...
  • Rais analaaani...
Yaani watu tunaotegemea mkae chini mje na suluhisho mko busy kulaani!
Yaani utazani hao watekaji ni mashetani siyo watu!

Naomba matamko ambayo hayana mrejesho wa vitendo yasipewe nafasi kwenye media hayana tija!

MATARAJIO YANGU YALIKUWA HIVI

Nilitegemea baada ya hali ya hewa ya utekaji kuongezeka taasisi zinazotuhumiwa kuhusika zingekuja na mkakati na kauli mbiu ya kutufariji!

Mfano! Polisi wangetangaza kauli mbiu na kampeni isambae nchi nzima.. KATAA AFANDE KISHOKA JISALIMISHE POLISI

Kama zamani tuliweza kuhamasisha watu kutumia condom kwa kauli mbiu ya ISHI KAMPENI, au kampeni ya maji salama, Tunashindwaje kuandaa kampeni ya KATAA AFANDE KISHOKA JISALIMISHE POLISI?

Wasanii wapewe magwanda watunge na kurekodi video vya matangazo ya kutokomeza aina ya utekaji!

Jamii ipewe elimu kwamba POLISI ANAPOKUJA KUKAMATA ATAKIWA AWEJE na wale Ili pale inapotokea KINA AFANDE KISHOKA wanareta vurumai katika ukamataji jamii itambue hawa ni watekaji HATA KAMA watakuja na gwanda na mitutu!

Jamiii itambue kama kuna haki hata ya kupiga picha kabla ya kukamatwa na polisi!

PIA turekebisha na sheria za VING'ORA vya magari ...yamekuwa mengi mno huko barabarani na watekaji nao wanaweza kutumia mwanya huohuo wa Ving'ora ili wawahi katika adhima yao ya utekaji!

Kuna sababu gani ya kuwa na utitiri wa ving'ora huko barabarani kila mtu ana masharubu, kila mtu kisa ana kimulimuli huyo anapita hata sehem na kutanua sehemu isiyoruhusiwa mnaona ni sawa?

Kuna sababu gani magari ya polisi mengine kutokuwa na namba za usajili mnataka nani atii sheria?

Mnapolaani mkumbuke na hayo yafanyiwe kazi ili jamii itenganishe polisi na afande kishoka!

Kama watu mashuhuli wanaweza kukamatwa pasipo kufuata sheria, je watu wengine huko inakuwaje?

HIZO GHARAMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MAMLAKA nani awajibishwe KUZILIPA?

Yaani polisi anakama kimakosa halafu mahakamani inakuja kuonekana alikosea katika ukamataji hizo gharama na hasara vyombo vya moto na kesi nani anazilipa? Au ndo matumizi ya kodi zetu?

Kama kodi zetu zinatumiwa pasipo kufuata sheria nani anauchungu wa kusimamia kodi tunazolipa kwa jasho?

HUU ULIPASWA KUWA MJADALA MPANA ILI kutokomeza Hii teka teka kuliko kila mtu kugawa laana!
 
Yaani watu tunaotegemea mkae chini mje na suluhisho mko busy kulaani!
Yaani utazani hao watekaji ni mashetani siyo watu!
Polisi wameshindwa kutulinda.

Soultion: Wakija watekaji na kutaka kumchukua mtu kibabe wananchi wafunge mtaa wasitoke wachomwe moto ndiyo itakuwa solution ,wakichomwa moto nadhani watakuwa wanafata taratibu za ukamataji ,wananchi waki wengi wenyewe wataogopa hata wakiwa na mitutu.
 
Tuanze na kampeni kwanza ya kukataa kina AFANDE VISHOKA kabla ya kujichukulia sheria mkononi!
 
Maana sahv ni rahis sana kumteka mtu na jamij ikaona ni polisi kumbe ni majambazi!
 
Huoni sahivi raia wakiona watu wanakuja kumchukua mtu bila kuonesha vitambulisho au kuvaa sare wanaanza kuwadindia

Ova
 
Huoni sahivi raia wakiona watu wanakuja kumchukua mtu bila kuonesha vitambulisho au kuvaa sare wanaanza kuwadindia

Ova
Mdindaji mkuu boni yai walimchukua akiwa kadinda sembuse walamba rojorojo!
 
Mpango wa kuzuia hautakuwepo Kwa sababu wauaji ni polisi.mpango wa kuumaliza huu utekaji utaanza pale tu wananchi wakianza kuwauwa wanapokuja kuwateka hao policcm.Nguvu ya umma ikiamua haishindwi
 
M
Polisi wameshindwa kutulinda.

Soultion: Wakija watekaji na kutaka kumchukua mtu kibabe wananchi wafunge mtaa wasitoke wachomwe moto ndiyo itakuwa solution ,wakichomwa moto nadhani watakuwa wanafata taratibu za ukamataji ,wananchi waki wengi wenyewe wataogopa hata wakiwa na mitutu.
Mwanza na Dar(Kariakoo)wameanza vizuri,wamekataa Afande Vishoka!
 
Back
Top Bottom