Kila sehem tunalaani! Tunalaani! Tunalaaani!
Yaani sisi afrika hatujui mambo mengine yanahitaji vitendo!
Yaani utazani hao watekaji ni mashetani siyo watu!
Naomba matamko ambayo hayana mrejesho wa vitendo yasipewe nafasi kwenye media hayana tija!
MATARAJIO YANGU YALIKUWA HIVI
Nilitegemea baada ya hali ya hewa ya utekaji kuongezeka taasisi zinazotuhumiwa kuhusika zingekuja na mkakati na kauli mbiu ya kutufariji!
Mfano! Polisi wangetangaza kauli mbiu na kampeni isambae nchi nzima.. KATAA AFANDE KISHOKA JISALIMISHE POLISI
Kama zamani tuliweza kuhamasisha watu kutumia condom kwa kauli mbiu ya ISHI KAMPENI, au kampeni ya maji salama, Tunashindwaje kuandaa kampeni ya KATAA AFANDE KISHOKA JISALIMISHE POLISI?
Wasanii wapewe magwanda watunge na kurekodi video vya matangazo ya kutokomeza aina ya utekaji!
Jamii ipewe elimu kwamba POLISI ANAPOKUJA KUKAMATA ATAKIWA AWEJE na wale Ili pale inapotokea KINA AFANDE KISHOKA wanareta vurumai katika ukamataji jamii itambue hawa ni watekaji HATA KAMA watakuja na gwanda na mitutu!
Jamiii itambue kama kuna haki hata ya kupiga picha kabla ya kukamatwa na polisi!
PIA turekebisha na sheria za VING'ORA vya magari ...yamekuwa mengi mno huko barabarani na watekaji nao wanaweza kutumia mwanya huohuo wa Ving'ora ili wawahi katika adhima yao ya utekaji!
Kuna sababu gani ya kuwa na utitiri wa ving'ora huko barabarani kila mtu ana masharubu, kila mtu kisa ana kimulimuli huyo anapita hata sehem na kutanua sehemu isiyoruhusiwa mnaona ni sawa?
Kuna sababu gani magari ya polisi mengine kutokuwa na namba za usajili mnataka nani atii sheria?
Mnapolaani mkumbuke na hayo yafanyiwe kazi ili jamii itenganishe polisi na afande kishoka!
Kama watu mashuhuli wanaweza kukamatwa pasipo kufuata sheria, je watu wengine huko inakuwaje?
HIZO GHARAMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MAMLAKA nani awajibishwe KUZILIPA?
Yaani polisi anakama kimakosa halafu mahakamani inakuja kuonekana alikosea katika ukamataji hizo gharama na hasara vyombo vya moto na kesi nani anazilipa? Au ndo matumizi ya kodi zetu?
Kama kodi zetu zinatumiwa pasipo kufuata sheria nani anauchungu wa kusimamia kodi tunazolipa kwa jasho?
HUU ULIPASWA KUWA MJADALA MPANA ILI kutokomeza Hii teka teka kuliko kila mtu kugawa laana!

- Jeshi la polisi linalaani...
- Mashejh wanalaaani...
- Waziri analaaani...
- Wachungaji wanalaani..
- Wananchi wanalaaani..
- Bunge linalaaani...
- Rais analaaani...