Tangu utekaji uanze sijawahi kuona mpango kazi wa kuzuia watekaji; Wengi wetu tunalaani badala kuja na suluhisho kama hivi

Tangu utekaji uanze sijawahi kuona mpango kazi wa kuzuia watekaji; Wengi wetu tunalaani badala kuja na suluhisho kama hivi

Andiko lako likekuja muda Sahihi,Cha msingi kama serikali imeshindwa kuwalinda raia wake kwa vitendo basi Kila mtu atambue kuwa usalama wa mwili wako ni wewe mwenyewe hivyo basi Anza kujilinda wewe mwenyewe.
 
Mkuu mambo yote n tarehe 23.9.2024 TUTAPIGWA SANAAA hil nakuakikishia
 
Andiko lako likekuja muda Sahihi,Cha msingi kama serikali imeshindwa kuwalinda raia wake kwa vitendo basi Kila mtu atambue kuwa usalama wa mwili wako ni wewe mwenyewe hivyo basi Anza kujilinda wewe mwenyewe.
Serikali imethibitisha watu binafs na majambaz bado yanamiliki silaha waziwazi wanazotumia kutekea!
 
Tusubili utash badala ya sheria kuamua
 
Watu wako busy na umbea ila kujadili mambo ya msingi hamna
 
Utekaji ndiyo njia nyepes ya polisi kumkomoa mtu
 
Hii kamata kamata na utekaji ina baraka kubwa sana kuliko watu wanavyozania!

Kamata na utekaji imeonekana ni mbinu inayolipa haraka zaidi kuliko ile ya ustaarabu!

Hivyo ni vigumu mno sasa hivi kwa raia kutofautisha yupi ni mtekaji na yupi ni askari!

IFAHAMIKE Kuna ile KAULI ya Polisi sheria kwamba UKIMZUIA ASKARI AKIWA ANATEKELEZA MAJUKUMU YAKE NI KOSA, Hili peke yake linaweza kupelekea wewe kufungwa JELA au kuunganishwa na mtuhumiwa!

Polisi Halazimishwi kuvaa sare wakati wowote anapotekeleza majukumu yake, lakini pia polisi kuna kipengele kingine kinaitwa ANAWEZA KUTUMIA NGUVU YA KADRI ili kumdhibiti wanaedai ni mhalifu!

Sasa kwa hayo hapo juu ni RAIA Gani ataweza kutofautisha zoezi hili la utekaji na lile la ukamataji wa polisi kwa nguvu ya kadri?

Ukiwazuia wanakuunganisha kwenye utekaji!

Sioni wa kumzuia mtekaji! Watu pekee ambao huwa angalau na uthubutu kidogo ni kina mama,

kina mama angalau wakiwa wawili watatu huwa hawaogopi sheria na hujikuta wanapiga kelele za ujasiri!

Lakini wanaume wengi huwa wanatafakari kabla ya kuingilia kati, moja ya tafakari huwa ni hii USIMZUIE ASKARI KUTENDA KAZI YAKE.

Hili la ukamataji na utekaji ni vigumu sana kulitenganisha na POLISI kwasababu mbinu ya VIKOSI KAZI vya serikali kuanzia mgambo, polisi, jeshi wooote ili wapate matokeo ya haraka wanatumia mbinu hii!

Kama kweli polisi wanalaani wapige marufuku ukamataji wa hivyo na jamii ifahamishwe kupitia vyombo vya habari kwamba popote watapoona watu wanaojitambulisha kuwa naaskari kwa style hiyo wapigwe mawe!
Lakini kusema tu mkiona tukio pigeni simu polisi mnapaswa kujiuliza mnamshitaki nani polisi wakati ndo huyo yupo doria uraiani akidaka watu!

Yaani ni sawa uwapigie emergency tanesco kwa kukatiwa umeme na mafundi emergency waliokuja kukata umeme bila sare!

Niliwahi pia kushauri haya katika mada hii lakini watu tunapenda zaidi kujadili umbea wa bartazari na si mambo ya msingi.
 
Haki za mtuhumiwa anapokamatwa na askari kisheria zipo.

1. Haki ya kufahamishwa sababu ya kukamatwa


2. Haki ya kukaa kimya


3. Haki ya kupata mwanasheria


4. Haki ya kutopigwa au kuteswa


5. Haki ya kuwasiliana na familia au rafiki


6. Haki ya kufikishwa mahakamani kwa haraka


7. Haki ya kupewa dhamana


8. Haki ya kutopigwa au kuharibiwa mali
 
Watu pekee ambao huwa na uthubutu kidogo ni kina mama, kina mama angalau wakiwa wawili watatu huwa hawaogopi sheria na hujikuta wanapiga kelele za ujasiri!
Naomba unitajie Bank ambayo inalindwa na askari Mwanamke mwenye Silaha, nina jambo nataka nikafanye research hapo
 
Haki za mtuhumiwa anapokamatwa na askari kisheria zipo.

1. Haki ya kufahamishwa sababu ya kukamatwa


2. Haki ya kukaa kimya


3. Haki ya kupata mwanasheria


4. Haki ya kutopigwa au kuteswa


5. Haki ya kuwasiliana na familia au rafiki


6. Haki ya kufikishwa mahakamani kwa haraka


7. Haki ya kupewa dhamana


8. Haki ya kutopigwa au kuharibiwa mali
Ni kweli lakini ile nguvu ya kadri inafunika yote hayo
 
Naomba unitajie umewahi kushuhudia Mtekaji Mwanamke? Ndio maana Bank hazilindwi na Wanawake wenye Silaha
Watekaji ni watu wasiojulikana unataka nikutajie mimi tena ndugu wakati hawajulikan
 
Kama ni watu wasiojulikana hata polisi hawawezi kuwajua
 
Back
Top Bottom