Tangu zamani nilishaapa kuwa nikiolewa siwezi kuishi na Mama mkwe wangu

Tangu zamani nilishaapa kuwa nikiolewa siwezi kuishi na Mama mkwe wangu

NAOMBA UNISAIDIE NAMNA YA KUMFUKUZA MAMA YANGU MZAZI KWANGU NIMECHOKA!

Tangu zamani nilishaapa kuwa nikiolewa siwezi kuishi na Mama mkwe wangu wkani nilikua nafahamu jinsi Mama wakwe walivyo na roho mbaya. Kweli sikuishi naye, Mama mkwe wangu hata hakuwahi kuja mjini kusalimia, ndoa yangu ilikua na amani kwa miaka 12 ya mwanzo. Lakini mwaka jana mwanzoni Baba mkwe wangu alifariki dunia, Mama mkwe ni mtu mzima ana miaka kama 67.

Alibaki kijijini mwenyewe hivyo mume wangu kwakua ndiyo mkubwa kwao aliniambia kuwa anataka kumchukua Mama yake kuja kuishi naye. Nilikataa wkani nilishajiapiza hivyo, lakini mume wangu alisema hawezi kumuacha Mama yake akiteseka kijijini. Nilikubali shingo upande lakini ili kumkomoa mume wangu nilienda kijijini na kumchukua Mama yangu ili tuje tuishi wote.

Mimi Baba yangu yuko hao, lakini nilidanganya kuwa Mama je Dar kuchekiwa kwani mara nyingi alikua analalamika miguu, basi alikuja nikijua kuwa, wakiishi na Mama mkwe wangu watagombana au mume wangua tachukia na kumfukuza Mama yake ili tuishi wenyewe. Mama yangu alikuja mwaka jana na mume wangu alimpokea vizuri, tuna nyumba kubwa tu hivyo hakuna tatizo kwa hilo.

Sababu ya kuja kwako ni hivi, Mama mkwe wangu pamoja na umri wake mkubwa ni mtu poa sana mpaka naona aibu, anamka anafanya usafi nyumba nzima, yaani hata kama nipo anasema hapana nikikaa hivi sifanyi kitu nitakufa kwa uzee, ananisaidia kupika, anapenda watoto, alikua Mwalimu, yaani anafundisha watoto wangu, wananidhamu na wanamuelewa kuliko hata mimi.

Hana kelele na sasa hivi mume wangu alikua mlevi ila kwa Mama yake kaacha pombe kwani Mama alimuambia hawezi kula chakula mtoto wake akiwa nnje hivyo ni kama kamnyoosha, yaani Kaka Mama mkwe wangu hana shida. Shida imekuja kwa Mama yangu, ana visa mpaka naona kama anataka kunivunjia ndoa yangu. Mwanzo nilikua namuona Mama yangu kama mtu wa kawaid, hana maneno na nimu mzuri.

Lakini baada ya kuja Dar, kwanza ni mtu wa majirani, yaani yeye akiamka Mama mkwe kashapika chai anywe aende kwa majirani, tunapokaa si uswahilini sana ila kuna majirani kashazoea nao. Pili anavituko vingi, napenda kugombeza watoto na akigombeza anatukana kabisa, lakini pia mimi na mume wangu tunafanya kazi, tuna utaratibu wa kufanya vitu kwa pamoja.

Mama yangu hivyo hataki, analeta maneno maneno kuwa mume wangu hachangii chochote, mimi ndiyo namlisha na vitu vingi, kisa tu mimi nafanya kazi serikalini na Mume wangu binafsi hivyo anajua mimi nina akili sana na nina pesa nyingi sana hataki nichangie chochote. Anashindwa kujua kuwa msahara wa mume wangu ni zaidi ya mara tano ya mshahara wangu na kila kitu tunaandika majina yetu au ya watoto.

Mama yangu baada ya kuja huku kuna jirani yetu alimshawishi na kuingia kanisa moja hivi, basi baada ya kuingia huko akaambiwa kuachana na Baba kwani yeye hajaokoka, basi sasa hivi ni kwamba wamegombana, yaani hata ukimuambia kuhusu kurudi nyumbani anakataa kwakua kaambiwa haezi kuishi na mtu si wa dhehebu lake. Shida nyingine nikuwa, anasumbua kuhusu fedha za sadaka, yaani hata kama huna ataongea na hapo nyumbani hakutakalika.

Usiku anaweza kufungua Radio, akafungulia nyimbo kwa nguvu vila kujali kama watu wamelala, sasa hivi kaanza kitu kingine, kila siku saa nane usiku huamka na kuanza kukemea mpaka asubuhi. Yaani kaka ni mambo mengi mpaka najuta, mume wangu hajwahi kunilalamikia hata siku moja lakini najua kuwa anaumia na vituko vya Mama yangu an ipo siku atachoka.

Naomba nisaidie Kaka, nifanye nini, nina ndugu zangu hapa Dar nikiwaambia wanisaidie kumchukua wanakataa kwani washamjua tabia zake wananiambia sikutumwa kumchukua kijijini. Yaani nina mdogo wangu yeye hana ndoa anaishi mwenyewe, nimemuambia amchukue Mama kabla hajanivunjia ndoa yangu yeye anasema angalau mimi nina ndoa ya kuvujja yeye akiishi na Mama hata ndoa hataipata, nisaidie, nifanye nini, nimfukuzeje wakati kijijini Baba hamtaki kwasabbau ya dini, nisaidie Kaka?

Mwanakulitafuta
Mwanakulipata
Tulia dawa iingie
 
Kupitia huu mwandiko wako tayari nimeweza kugundua una umbo la namna gani.[/SIZE][/QUOTE]

piga ua atakua kimbaumbau flan hivi
 
Una nia OVU tangia mwanzo na Hili linadhihirika kupitia mama yako.
Tubu
 
Subiri msiba / sherehe utokee kijijini mkienda ukamuache huko
 
Mim nikimskia.or nikihis tuu kuwa mke wangu hampendi mama angu..bas huyo mke ataish kwa tabu sana...tabu snaaaa

Yaan ntampa adhab ambazo atataman asingenijua..kwanza ntazaaa nje kumkera tu.sirud nyumban.michepuko ya kutosha

Yan ni bora u pretend kumpenda maza
 
We always get lesson in a hard way. Nadhani huu msala umejiletea mwenyewe mpaka sebuleni kwako.
 
Mi nimependa jibu la mdogo wako tu "afadhali wewe angalau una hiyo ndoa ya kuvunjwa, nikimchukua mimi hata hiyo ndoa haitapatikana" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]........acha ujinga we dada, huyo ni mama yako unaanzaje kumpangia mikakati ovu ya namna hiyo
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ujue kuishi na mama yako sehemu uliyoolewa ni aibu! Kwani jamaa kaoa mama na mtoto??
 
Vipi kama mama yako ana tabia kama za mama yake huyu binti??? Kuna watu Wana tabia mbaya tu, sio sababu mama yako basi ndio awe malaika hata akikosea basi watu wakae wavumilie, Kuna wamama wengine vichomi kwelikweli tena mpaka unajiuliza huyu binadamu au vipi yaani, ni vile hana roho ya Utu wala huruma... Kabla hujamchukia mkeo kisa mama yako, Anza kutumia Muda wako kumjua mama yako yupoje kwa mkeo.... Hakuna hukumu inayotoka kwa kuangalia upande mmoja.
Mim nikimskia.or nikihis tuu kuwa mke wangu hampendi mama angu..bas huyo mke ataish kwa tabu sana...tabu snaaaa

Yaan ntampa adhab ambazo atataman asingenijua..kwanza ntazaaa nje kumkera tu.sirud nyumban.michepuko ya kutosha

Yan ni bora u pretend kumpenda maza
 
doh pole bidada.je hukujua tabia za mama yako kabla hujamchukua kuja mjini?

kama ulikuwa hujui basi ina maana kwamba hata wewe ni mtoto kama mama alivyo. nakushauri fika kwa viongozi wa dini husika ili ufikishe malalamiko yakonkwa hatma ya ndoa yako
 
Roho mbaya imekuponza....!

Ila tafuta wenye busara wamueleze bi mkubwa hasa kama una mjomba wako ndo itapendeza zaidi.
 
Wewe una roho mbaya mnoo, yaani eti ulikuwa umejiapiza kutoishi na mama mkwe tena mzee wa mungu! Na hizi ndio akili za mabinti wengi wa kileo.

Na hao wanaume suruali mnaowapata eti mie mama yangu nikitaka kuishi nae nikuulize wewe kuwa nimlete au la, hilo haliwezitokea. Nitachofanya ni kukupa taarifa tu sio kukuomba.

Mme wako ni mwanaume wa shoka, sio mwanaume suruali, na ndio maana hakukusikiliza ulipomkatalia mama yake kuja kuishi nae.

Sasa ukatarajia umkomeshe mmeo kwa kumtoa mama yako kwa mmewe (baba yako) kwa hila za kishetani (hiyo nayo ni kumkosea adabu baba yako ), sasa ubaya umekurejea kisha unaanza kulialia humu.

Na tayari umeshamvunjia ndoa baba yako sasa
 
Ita mchungaji akifika mwambie akufafanulie juu ya huu mstari Mwanzo 2:24, Waefeao 5:31 naamini had hapo wataondoka wenyewe
 
Back
Top Bottom