Tani 7,400 za mahindi zakosa soko

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2009
Posts
11,966
Reaction score
11,218

Chanzo: Mwananchi

My take;

Hivi katika nchi ambapo ni wengi tu wanaishi kwa mlo mmoja inawezekana vipi mahindi au chakula kikakosa soko, wafanyabiashara wa kitanzania inabidi waongeze ubunifu na serikari inabidi iweke mazingira mazuri ya kibiashara kwa sasa. Si kujenga miundo mbinu tu bali izingatie na majukumu mengine sanasana ya 'fiscal policies' itakayo enda sambasamba na ukuwaji wa microeconomics.

Binafsi bado nakataa sana bei za sokoni kwenye miji bidhaa nyingi za chakula ukichukulia bei za mkulima anazotoa, ni wakati sasa wafanyabiashara waanze ku-lobby ili waweze ku-exploit uwezo wa soko na kuwafikia wengi. Kwa sasa kiualisia itakuwa ngumu kutokana na uhaba wa few participants in the haulage sector akuna bei za ushindani, majukumu ya mikopo ina riba kubwa plus government taxes.

Ni wakati sasa pengine watu kama akina Mengi na wao waongeze jitihada kwenye ku-lobby kama viongozi wa umoja wa wafanyabiashara si kufikiria vitalu tu, wawausishe makundi ya wafanyabiashara wadogo, new enterprenuers kwenye bodi zao, kuwe na ushirikiano na vyombo kama TASO na makundi mengineo bila ya kusahau kutafuta wasomi wa kuwafanyia research na wao ili waweze jibizana na sera za serikari bila ya kuathiri maendeleo na kuongeza pressure yakuwekewa mazingira mazuri ya kibiashara ili bei za soko ziwafikie; ususan kwenye kodi na kwenye interest za mikopo.

Kwa kweli umaskini wetu ni wazi for the large part tunachangia mambo yanavyofanyika na wenzetu mbona maswala yenyewe yapo wazi na na yanataka ku-copy and paste tu, ok with a little bit of imagination required suitable in relation to the stage of our economy.
 
Kilimo kwa Mtanzania wa Sasa ni kama Kamali/Gambling/Betting.., uhakika wa kwake kupata ni sandakarawe...
 

Mkuu bei kwa mlaji ikishuka ndio mkulima atapa zaidi ?, Bei kwa mlaji ikishuka bado middle man atashusha kile anachompa mkulima..

Cha kufanya ni kujaribu kwa wakulima kutengeneza unions za kuweza kumfikia mlaji moja kwa moja na kuondoa middle man alafu mambo ya kuwakataza wakulima mara wasiuze nje au wasifanye hiki wakati hakuna guarantee ya kununua mazao yao kwa bei wakulima wanayotaka ni Ujambazi wa Serikali dhidi ya watu wake
 
Both Sudan south na north wanahitaji chakula and the prices are good.Huko ndiko wakenya upeleka mahindi yetu.
 
Serikali ifungue mipaka mzigo uende Congo, Rwanda, Burundi, Kenya , Sudan nk halafu uone kama kuna tatizo la soko.
Serikari pekee aiwezi kuona umuhimu wa kila jambo pengine kwa sababu kwa upande wao hakuna hasara.

Mantiki ya kuwa na makundi ya kimasahi na representative ni kupigania upande wa wanakundi, kama kwa sasa hakuna soko la bidhaa kwa sababu zozote zile iwe ugumu wa maisha, uhaba wa kufikisha bidhaa sokoni na sababu zingine za kiuchumi. Ni viongozi wa wakulima walitakiwa kuwa mstari wa mbele na kutoa pressure ya kutosha serikarini ili wabadili tabia kama kuna masoko ya nje, aiwezekani watu wawache jitihada na hela iliyotumika ipotee bure tu something is very with these reps group leaders for that matter.
 
Hiyo ni ya Babati pekee, Dodoma kwa sasa mahindi ni 15,000 mpaka 20,000 kwa Gunia,
Tatizo letu sio wakina Mengi kuweka new entrepreneur kwenye bodi zao, kuna matatizo mengi sana kwenye sekta ya kilimo
1. Kukosa mitaji ya kuwekeza kwenye kilimo,
2. Mkulima kunyonywa na Serekali kwa ushuru wa mazao
3. Mkulima kunyonywa na Madalali ambao ndio wanafaidika 100% kuliko wakulima
4. Wakulima kutokujua Wanalima kwa ajili gani ( vision)
5. Siasa nyingi kuingizwa kwenye kilimo mfano ni mizani ya aina gani itumike kununulia
Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayoikabili sekta ya kilimo, hata kama NFRA watapewa fedha bado mkulima hataona faida ya moja kwa moja, hujawahi sikia viongozi wa serekali " kama umechoka kukaa mjini rudi shamba ukalime?" watu haohao ndio waliopewa dhamana ya kuunda sera za kumsaidi mkulima unadhani tutatoboa???

Mabadiliko ya kweli ni mpaka pale tutakapo funguka akili zetu tujue kuwa serekali ni sisi na sio wao, tuunde umoja na plan namna tutakavyofaidika na kilimo kabla hata hatujachukua jembe na kwenda kulima, tofauti na hapo tutaishia kulalamika na kuwafaidisha madalali
 
Kilimo kwa Mtanzania wa Sasa ni kama Kamali/Gambling/Betting.., uhakika wa kwake kupata ni sandakarawe...
Kwanini ibaki hivyo wakati wote wana mahitaji sawa particularly wakulima wadogo? uoni ni sababu tosha ya wadau wakilimo kupigana hiyo bahati nasibu ifike mwisho. Unajua hakuna tofauti na siasa kwenye kutoa pressure kama UKAWA wanavyofanya kwenye kutoa ikibidi maandamano (hata kama wakati mwengine ukubaliani na hoja zao), nawakulima pia wanaweza kuandamana na kutoa elimu ya uozo wa kisera au swala la kuoza kwa chakula.

Hatuwezi kusema ukulima ni bahati nasibu wakati namna za kuuzika bado azijakuwa exploited zote ni ujinga kulikalia kimya, swala hili ndio maana na wahusika wa serikarini awaoni tatizo wala sababu za kubadilika.
 
Mkuu mipango ya biashara aianzi na bei ya mlaji, mipango ya biashara inaanza na gharama za bidhaa na operation cost yote mpaka unapomfikia mlaji
ndipo unapopanga bei ili urudi na faida.

Kwa hali ya sasa bei za wakulima ni tosha sana kupata gap kwenye soko na kutengeneza faida kwa bei ya chini ya soko, inahitaji strategy nzuri tu na mtaji wa kutosha, kwa sababu hata huyo middle anatokea kutokana na uwezo wa mfanyabiashara kama unaweza negotiate na kumudu gharama za kuwafikia wakulima mwenyewe na una means hizo why do you need the middle man?

Hayo makundi ndio kabisa mimi naona viongozi wao ndio vikwazo ya kwanini sera azibadiliki miaka nenda miaka rudi kila msimu kama mchele auja oza songea, korosho zimekwama mtwara; kila msimu yaleyale ina maana hakuna shinikizo kwa serikari kubadili muono wake na ndio maana na wao hawaoni tija kwa sana.
 
Ukweli mkuu lakini serikari itabadilika vipi bila ya kushinikizwa mbona aikuchukua muda kubadili mtazamo walipotaka wagusa wenye vituo vya mafuta na namna za ulipaji kodi kwenye sector wakafanya u-turn within a short space of time.

Mengi ya hayo unayo yaongelea nimegusia kwenye post yangu namba moja, hizo ni changamoto zilizowazi kwa sasa ukiwasikia wakulima. Ndio sababu ya kumuingiza Dr. Mengi akiwa kama mwenyekiti ya bodi wafanyabiashara binafsi, wao walitakiwa kwa sasa kuwa umbrella ya hivi vijivikundi vilivyo jikita kimaslahi ili waweze fanya lobbying yenye nguvu kutumia uwezo na nguvu za pamoja hivyo ndio serikari zinavyoshikizwa kuangalia tofauti sera.

Vilevile nikaongezea ya kuwa itakuwa kazi bure (indirectly) kwa sababu pia serikari zinamajukumu yake hivyo aziwezi kupunguza kodi kwa kushinikizwa tu, bali inahitajika evidence ya kuwa punguzo la kodi kweli itafanya mazao yawafikie wengi na ukuaji wa sector commercially ambapo situation hiyo itaweza pato la serikari through growth.

Na ili tufikie hali hiyo maana kwa sasa wachezaji wa kati ni wachache kunahitajika sera zingine zitakazo compliment ukuaji wa sector mfano encouragement on more haulage ili kuwe na ushindani wa bei kwenye uchuuzi, kumbuka kushuka kwa bei za uchuuzi kuna acha gap ya muuzaji kuweza na yeye kushusha bei zake ili kuongeza volume ya mauzo (binafsi isabu zangu zilianzia hapa gharama za kutoa mchele Iringa mpaka dar kilo ambazo zinaweza ingia kwenye lorry sikubaliani kabisa na bei za soko, kama lorry langu mimi mwenyewe na nauza mimi mwenyewe sokoni). Kuna mengi hapa ndio maana nikasema kwa ufupi tu inahitajika tathmini independent kutoka kwenye vikundi vya wafanya biashara na serikari kufikiri sera zao za fiscal policies kwa sasa kwenye kilimo.

Sasa hayo mambo hayaji hivi hivi bila ya counter proposal ya sera za serikari zilizopo you can see why makundi yaliyopo kimaslahi yana ajiri ma professor na ndio mizizi za sera nchi za wenzetu, chanzo cha lobbying na mengineo to do with maendeleo na kuwafikia wanamakundi.

Vyakula vinaoza kila mwaka hawa jamaa waliopo wanafanya kazi kweli?
 
Mkuu mipango ya biashara aianzi na bei ya mlaji, mipango ya biashara inaanza na gharama za bidhaa na operation cost yote mpaka unapomfikia mlaji
ndipo unapopanga bei ili urudi na faida.
Mkuu wewe ndio umesema haukubaliana na bei ya bidhaa sokoni kulingana na middle man anavyonunua kwa mkulima.., mimi ndio nikakwambia bei ya mlaji/sokoni ikishuka ndio mkulima atapata kazi zaidi ?


Rudia kusoma nilivyokujibu ...., nimesema kuondokana na hii shida wakulima wenyewe inabidi waform unions ili waweze kuuza sokoni direct (umoja ni nguvu) wakiungana watakuwa na negotiating power na hata uwezo wa kununua au kukodisha magari kupeleka mizigo sokoni na hata kutafuta masoko ya nje (kama serikali itaacha upuuzi wake wa soko likiwa zuri nje kuwabana wasiuze na demand ikiwa ndogo kuwatupa na mizigo yao)

Hayo makundi ndio kabisa mimi naona viongozi wao ndio vikwazo ya kwanini sera azibadiliki miaka nenda miaka rudi kila msimu kama mchele auja oza songea, korosho zimekwama mtwara; kila msimu yaleyale ina maana hakuna shinikizo kwa serikari kubadili muono wake na ndio maana na wao hawaoni tija kwa sana.
 
Mkuu wewe ndio umesema haukubaliana na bei ya bidhaa sokoni kulingana na middle man anavyonunua kwa mkulima.., mimi ndio nikakwambia bei ya mlaji/sokoni ikishuka ndio mkulima atapata kazi zaidi ?
Mkuu

Kwenye mawazo yangu hakuna middle man ndio sababu nikasema inategemea na strategy ya mfanyabiasha na operation zake na uwezo/nguvu yake ya mtaji anayofanyia biashara, kwa maana hiyo unapomwingiza middle man tayari umeshapanga strategy tofauti at times kutokana na uwezo wa mfanyabiashara unaye muongelea wewe na sikatai with those in the middle prices are bound to hike sokoni.

Lakini kama unakuja na strategy nzuri there is aprice gap to be exploited in the market, considering kuna watu wanakula kwa kujinyima kwa sababu ya bei common sense bei zako zikiwa chini utawafikia wengi na kuweza kununua zaidi kutoka kwa mkulima this is why I said this:
mipango ya biashara aianzi na bei ya mlaji, mipango ya biashara inaanza na gharama za bidhaa na operation cost yote mpaka unapomfikia mlaji
ndipo unapopanga bei ili urudi na faida.

Hapa tunaongea kitu kimoja kwa lugha tofouti sijakataa ya kuwa umoja wao utawaongezea bargaining power kwenye soko na kutetea maslahi yao lakini that is not enough kwa nchi zinazoendelea na zenye sera za ubepari au zilizoendelea wengi wanakubalina na bwana Porter na theory yake ya secretarial growth mbali na tools ambazo government can offer there is also the need of five forces in the market.



Na serikari nyingi kwenye sera zao zinalenga kuweka mazingira hayo ambapo soko huwa linaji regulate lenyewe in terms of supply and demand kuna mengi hapo yakufanyika kwenye safari yetu ndefu ya maendeleo kutokana na uchumi wetu ulipo. However kutokana na hali ya sasa kwa Tanzania (bado sana kufikia malengo ya theory) ukiangalia mambo yalivyo na bei za kujiamulia sanasana kama unatumia middle bei zinakuwa juu, ila bado kuna nafasi kubwa sana za faida kama unaingia na strategy sahihi na una mtaji wa heshima kumtoa middle man.

You can see why i thought there is not enough pressure from participating stakeholders to make the government change their views or implement the right policies those that nurture growth si tu kumsaidia mkulima bali kukuza our microeconomies.

Mchana mwema.
 
Eric Cartman

Kwenye maelezo hapo meeengi hapo juu Post No. 13..., sijui unataka kuelezea nini au tunacho-debate ni nini ?

Ili kufatuta solution inabidi ujue tatizo na uli-solve tatizo.., Sasa inabidi ujiulize tatizo kubwa ni nini linalopelekea wakulima wasiendelee hata wakiuza mazao na sometimes hata mazao yao hayauziki kwa zile bei ndogo.... ?, Hapo utagundua yafuatayo
  • Miundo Mbinu mibovu ya kuweza kufikisha mazao sokoni (hii ni kazi ambayo serikali inabidi iwajibike na sio kuweka barabara tu bali vitu kama reli ambayo ni cheapest transport inabidi iwepo
  • Wafanyabiashara wanaochukua fursa kwa kununua kwa wakulima na kuwapunja na kulangua..
  • Kutokuwepo na uwezo kwa wakulima wadogo wadogo kuwa na maghala makubwa na kutunza chakula chao ili kuweza kuuza pale bei inapokuwa nzuri na umasikini unawapelekea kuuza haraka hata kama bei ni mbaya
  • Serikali kuwakataza wakulima sometimes kutafuta soko zuri (hata kama ni nje ya nchi) na kutaka wenyewe wanunue wakati hata bei wanayowapa sio nzuri

Kwahio hapa utagundua kwamba kuna solution mbili.. Kwanza serikali iache wakulima wauze kule wanapoona panafaa wakati wowote ule, na kutengeneza miundo mbinu ili mizigo ifike sokoni kwa bei rahisi.

Pili wakulima wenyewe watengeneze vyama vyao wenyewe vya ushirika hivi vitahakikisha kila mzigo unanunuliwa kwa bei inayomfaa mkulima (yaani mkulima hauzi mazao mmoja mmoja bali anapeleka kwenye ushirika wake, alafu huo ushirika ndio unatafuta soko na kupeleka mzigo sokoni as well as adding value), na kama mazao yakiwa mengi mwaka fulani huo ushirika unakuwa na storage ya kutosha kuhifadhi hayo mazao.., huwezi kutegemea mfanyabiashara amsaidie mkulima wakati yeye anaangalia profit tu..., bali inabidi huo ushirika uwe pale wa wakulima kuwasaidia/kujisaidia wakulima wenyewe
 
Last edited by a moderator:
KeyserSoze

Mkuu soma kwenye porter's theory na majibu ya changamoto zako yapo hapo tunatoka vipi unapoongela miuondo mbinu angalia in terms of supplier na competition, unapoongelea disadvantage za wakulima angalia na wanunuzi wapo wangapi ili waweze kuringa au kuwa na jeuri ya kusubiri bei za soko zipande maana kama kuhifadhi si ndio tunachoongelea hapa mwishowe kinaishia kuoza, isitoshe baada ya mwaka kunakuwa na mavuno tena na kwasasa wakulima wadogo wanazalisha high volume kushinda kipindi chochote cha historia yetu.

Mwsiho unapozungumzia serikari kuacha kudhibiti soko hiyo ndio hoja aliyoileta Maundumula na hapa wote tunakubaliana kuliko vyakula kuoza bora viuzwe nje, sababu zangu mimi ni kuwa changamoto bado ziko nyingi kisera na uchache wa players kwenye soko (mitaji pia inakuwa sababu na vyanzo vyake) na hali hiyo inapelekea walaji kulanguliwa kwa kuwa prices are dictated by the middle man kusawazisha soko ndio nikamleta huyo bwana Porter msome taratibu utapata picha kamili ya angle yangu hapa kama utazingatia na mazingira ya tanzania utaona tu ni wapi pa kuboresha na intervention ipi inatakiwa.

Mchana mwema ntarudi usiku if anything.
 
Last edited by a moderator:
Serikali ifungue mipaka mzigo uende Congo, Rwanda, Burundi, Kenya , Sudan nk halafu uone kama kuna tatizo la soko.
hii ni mbinu chafu ambayo serikali dhaifu. unajua watu wanaoweza pindua serikali na kuleta mabadiliko ya kisiasa ni watu wa mijini na sababu kubwa huwa kupanda bei ya chakula. sasa serikali ili kujjihakikishia kubaki madarakani hufix bei na kufunga mipaka. huu ni unyonyaji mkubwa sana kwa mkulima na hii strategy ina backfire. maana uwekezaji kwenye kilimo utapungua na viijana watakimbia kilimo maana kinakuwa hakina pesa. kwa ardhi tuliyonayo serikali ifungue mipaka ione watu watakavyokimbilia kulima. tatizo viongozi wanataka tu kubaki madarakani
 

Mimi ni mmojawapo ya hao wanataka kuachana na kilimo cha mazao ya chakula mwakani nina target biashara tu!!!

Hadi hapo ambapo wakulima wa kutosha watakapotoka kwenye kilimo na kufanya bei kuwa juu.
 
KeyserSoze

Mkuu soma kwenye porter's theory na majibu ya changamoto zako yapo hapo tunatoka vipi unapoongela miuondo mbinu angalia in terms of supplier na competition,
Mkuu Najua Porters Forces.., na hapa wewe naona unacomplicate issue hadi unafanya issue inakuwa ngumu kuliko ilivyo.., cha maana ni kuangalia tatizo na kutafutia solution Just KISS it ......., Naongelea miundo mbinu ni mibovu hivyo kuna mazao yanaozea mashambani..., au mimi nikichukua gunia moja la mahindi kule mabonde kuinama ili nililete mjini unadhani bei itapanda kiasi gani ?, na hio increase ya bei ni faida ya nani ? utaona kwamba hapa source of production itapungua sana kama miundo mbinu (mfano trains ambayo ni cheaper kuliko magari itatumika) hapu kutaongezeka margin ambayo either atakula mkulima, mfanyabiashara au mlaji kwa bei kupungua...


Sijajua hapa unamaanisha nini ?, always wakati wa mavuno bei huwa zinashuka (kitu ambacho hapa wafanyabiashara ndio huwa wanalima) na baada ya mavuno bei zinapanda.., hapa ndio wafanyabiashara huwa wanauza.., Hivi unajua nafaka ikiwa stored vizuri inaweza ikakaa muda gani ? (hivi unajua zinaweza zikakaa miaka zaidi ya sita ?) ofcourse mtu mmoja mmoja hawezi ndio maana nikasema wakulima wanahitaji kuwa na Umoja ili hata umoja wao uweze kupata storage za kutosha.., alafu unapoongelea soko, sio kwamba soko ni la ndani tu.., unadhani kama wakulima wakiwa na Tons za kutosha zilizohifadhiwa kwa utaaalamu watakosa soko hata nje ya nchi ?, na kama wakulima kwenye stock yao wakiona wana mahindi ya kutosha wanaweza kufanya wengine crop rotation wakaona kwa sasa ni kipi kimepungua kwenye ghala ili tujaribu kulima hicho..,

Alafu unaposema kwamba wakulima hawawezi kusubiri bei zipande ebu jiulize wafanyabiashara huwa wanafanyaje sasa ?, kwahio mimi ninachoshauri badala ya wafanyabiashara kupata hio faida wakulima wenyewe kupia ushirika wao ndio wapate hizo faida.


Mkuu hatumuhiji hapa bwana porter at all it just complicating the issues na tunatoka kwenye mstari.., Bwana Porter anaweza akakusaidia kama wewe ni organization/business / corporation ili uweze kuangalia ushindani

Michael Porter's Five Forces of Competitive Position model provides a simple perspective for assessing and analysing the competitive strength and position of a corporation or business organization

In our case inabidi tuangalie ni vipi mkulima anaweza kufaidika (its by uniting na kuweza kuuza direct sokoni na kuondokana na middle men as well as finding new markets) pia ni vipi bei zinaweza kushuka (one of them is by decreasing cost.., hii itasaidiwa na miundombinu na urahisi wa mzigo kufika sokoni
 
Uzi kama huu, wale jamaa wa buku saba huwaoni hata mmoja, akichangia. Ni Ukweli usio na shaka, mkulima mdogo anaonewa sana, akifurukuta na kuvuna anapangiwa wa kumuuzia, ila wakati anahangaika au kufanya kazi za shamba hapewi msaada wowote, serikali inatakiwa iruhusu, wakulima kuuza kokote hapa duniani, na wachangie kulipa kodi ya mauzo.TUMEINGIZA SIASA KWENYE KILIMO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…