Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,966
- 11,218
![]()
Babati. Zaidi ya tani 7,400 za zao la mahindi zilizozalishwa na wakulima wadogo wa kata za Galapo na Qash wilayani Babati mkoani Manyara zimekosa soko na kurundikwa katika Soko la Galapo, eneo ambalo zinaweza kuharibika wakati wowote.
Wakizungumza jana na mratibu wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima wa Manyara (Mviwata), Martin Pius alisema wakulima hao waliiomba Serikali kufanya jitihada za haraka kwa kununua mahindi hayo ili kunusuru hasara kwa wakulima wa eneo hilo.
Mkulima wa Kijiji cha Galapo, Dodo Ekwani alisema wakulima wanateseka kwa kukosa fedha za kuwalipia ada watoto wao, kupata huduma za afya na pia kulipa vibarua na wakikosa viongozi wa kuwatetea juu ya hilo.
Mwenyekiti wa soko hilo, Lohay Langai alisema wakulima wa vijiji vya Galapo, Gedamary, Qash na Halu walileta mahindi yao sokoni wakitegemea Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula nchini (NFRA) wangenunua, lakini hali imekuwa tofauti.
Diwani wa Kata ya Galapo, Michael Naas Dil alisema suala hilo limekuwa kero katika kata yake na inampa wakati mgumu akiwa sehemu ya uongozi, hivyo ameiomba Serikali itoe fedha haraka kwa NFRA ili waweze kununua mazao hayo.
Mratibu wa Mviwata wa mkoa huo, Pius alisema soko ni suala muhimu na kichocheo kikubwa kwa uzalishaji na ubora wa mazao ya kilimo na inaweza kuwafanya wakulima wazalishe mazao mengi na kwa ubora unaohitajika.
"Hivi karibuni Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ilisaini mkataba na Kenya ili kununua mahindi ya wakulima, hivyo mchakato huo ufanywe haraka na taarifa ziwekwe wazi ili wakulima wadogo wafaidike," alisema Pius.
Chanzo: Mwananchi
My take;
Hivi katika nchi ambapo ni wengi tu wanaishi kwa mlo mmoja inawezekana vipi mahindi au chakula kikakosa soko, wafanyabiashara wa kitanzania inabidi waongeze ubunifu na serikari inabidi iweke mazingira mazuri ya kibiashara kwa sasa. Si kujenga miundo mbinu tu bali izingatie na majukumu mengine sanasana ya 'fiscal policies' itakayo enda sambasamba na ukuwaji wa microeconomics.
Binafsi bado nakataa sana bei za sokoni kwenye miji bidhaa nyingi za chakula ukichukulia bei za mkulima anazotoa, ni wakati sasa wafanyabiashara waanze ku-lobby ili waweze ku-exploit uwezo wa soko na kuwafikia wengi. Kwa sasa kiualisia itakuwa ngumu kutokana na uhaba wa few participants in the haulage sector akuna bei za ushindani, majukumu ya mikopo ina riba kubwa plus government taxes.
Ni wakati sasa pengine watu kama akina Mengi na wao waongeze jitihada kwenye ku-lobby kama viongozi wa umoja wa wafanyabiashara si kufikiria vitalu tu, wawausishe makundi ya wafanyabiashara wadogo, new enterprenuers kwenye bodi zao, kuwe na ushirikiano na vyombo kama TASO na makundi mengineo bila ya kusahau kutafuta wasomi wa kuwafanyia research na wao ili waweze jibizana na sera za serikari bila ya kuathiri maendeleo na kuongeza pressure yakuwekewa mazingira mazuri ya kibiashara ili bei za soko ziwafikie; ususan kwenye kodi na kwenye interest za mikopo.
Kwa kweli umaskini wetu ni wazi for the large part tunachangia mambo yanavyofanyika na wenzetu mbona maswala yenyewe yapo wazi na na yanataka ku-copy and paste tu, ok with a little bit of imagination required suitable in relation to the stage of our economy.