KeyserSoze Mkuu nimekusoma ingawa umeleta legitimate queries lakini naona kama vile unayotolea majibu mepesi sana tofauti na uhalisia wake jinsi mambo yanavyofanyika na kutekelezeaka kama unataka kufanya sustainable business. Ingawa nilia ahidi ntarudi jana usiku na maelezo lakini kila nilipo jaribu kutafuta angle ya kuanzia sikuona kwa sababu post ingekuwa ndefu sana ki maelezo na ingechukua a good chunk of my night wakati kulikuwa na kazi nyengine za kufanya kimaandishi na bado zipo zikiwa na deadline ya leo.
Vile vile ningeshauri upitie hii ripoti ya IMF "Tanzania economic update: "
who wants a Job"? ambayo iliwahi wekwa jukwaa la siasa na inapatikana online without fuss. Kwa sababu hoja ulizo ziibua wewe zina ambatana sana na maoni ya waandishi wa ile ripoti kuhusu ufanyaji wa biashara Tanzania na kwanini asilimia kubwa ya wafanya biashara wanabaki wadogo wadogo na mambo luluki kuhusu overall business environment ndani ya Tanzania. Ningependa kujibu kwa kina ile tuwekane sawa kwenye post yako lakini muda na siku avinipi hiyo luxury kutokana na majukumu yaliyo jitokeza kwa hivyo nitaweka tu mawazo yangu kwa kifupi na kama mjadala utakuwa live by next week nta weza kufafanua zaidi.
Mkuu wazalishe zaidi tena wakati mazao yanaoezea kwenye maghala ?, alafu hii issue ilishatokea hata England miaka fulani kulikuwa na supply kubwa sana ya maziwa hivyo yakashuka sana bei, wakulima wakaona afadhali kuyamwaga kuliko kuyauza ili ku-create shortage hence demand..,
Mkuu hapa unachanganya mazingira matatizo ya sera za kutoa subsidies kuwapa wakulima ushindani ndio vitu vinavyosababisha sana europe kuwa na over production in farming; as opposed to our over production problem inayosababishwa na luck of business opportunities.
Ni hivi nchi za EU zinatofautiana kisera, sheria za kazi, mishahara, taxes na kufanya gharama za kuendesha biashara kuwa kubwa, on the other hand kuna nchi nyingine bidhaa zao bado ziko chini kutokana na gharama za uzalishaji. Sasa basi makampuni yanayo tumia hizo bidhaa wanaona kuna faida zaidi iwapo watachukua bidhaa za nchi nyengine kuliko kutumia za kwao. Katika mazingira hayo serikari kwa kushinikizwa mara nyingi na wakulima au their representative groups ujikuta wakitoa subsidies hili gharama za kuzalisha ndani zipungue hili waweze shindana na wazalishaji wa mataifa mengine na kulinda sector ya kilimo. Kinachotokea unakuta ni kwamba even after those subsidies bado wanajikuta wapo juu kwenye gharama na isitoshe wafanya biashara nao wana angalia maslahi ya muda mrefu. Kwa mfano kama wewe ni muuza maziwa fresh utakuwa na option ndogo sana kununua nje, lakini anaetengeza chocolate, cheesse and other dairy product can afford to continue with importation. Kwa hivyo maziwa largely yanabaki kwa sababu ya wanywaji tu lakini matumizi mengine wafanya biashara think they can get a cheaper deal elsewhere. Kwa sababu jamaa wana-subsidies lazima waonyeshe wanaendelea kuzalisha na ndio kinachotokea na kusababisha over production.
On the other hand sisi tunazalisha lakini atujafikia kiwango cha kusema tumezidisha consumption ya soko na kinaoza alikadhalika bado tunauwezo mkubwa sana wakuongeza kilimo, isipokuwa kilimo kunakuwa restricted na uwezo wa wateja wote wanunuzi wakibiashara na walaji wa mwisho. Kwa maana hiyo kwa wazalishaji (wakulima) kilimo kinakuwa kama bahati nasibu hakuna 'production possibility frontier' ya kujua uwezo wa soko, ukijumlisha na changamoto wakulima wenyewe ni wadogo wadogo halafu wapo wengi wakifukuzia wanunuzi wachache wanaokwenda mashambani.
Kwanini unaweza kuona intermediaries wana kila advantage huko mashambani yaani mkulima anaweza shushwa mpaka borderline ya faida na ndio maana wengi bado wana hali ngumu wakati middleman anauwezo wa ku-push mpaka kwenye bei ya juu kabisa ya uwezo wa mlaji.
Na kwa sababu hiyo equilibrium iliyo jitokeza ina maana wakulima wanahitaji more players to if they are to gain advantage kwa sababu huwezo wa soko bado upo especially kama tunaongelea nafaka ambapo ndio lishe kuu kwenye jamii na inatumika kwenye kila nyumba na wengi bado inawasumbua sana kuimudu sanasana mijini kutokana na gharama. Kwa hivyo kuoza kwa chakula ndani ya Tanzania auwezi kulinganisha na kuoza kwa chakula nchi za EU. Anyway kuna details nyingi sana hapa za kuweka especially upande wa Tanzania isipokuwa muda na ukubwa wapost inabidi nizingatie.
Unachosahau ni kwamba ukiona mizigo haifuatwi sana na walanguzi fahamu kwamba margin imeshuka hata mlanguzi haoni faida kwahio anawekeza mtaji wake pengine... tofauti na kama stake holders wenyewe (wakulima) wangekuwa wana-direct link na soko hayo yasingetokea na hata ikiwepo surplus wangeweza kuhifadhi kutokana na uwezo mkubwa na facilities za kutosha (na hicho wasitegemee mfanyabiashara atawasaidia bali ni wenyewe wanaoguswa ndio wajisaidie au serikali ambayo ni kazi yake kuwaangalia wananchi wake)..
Hili nalo ni tatizo lengine kama utasoma hiyo ripoti niliyokwambia utaona waandishi wanalitafsiri vipi jambo kama hili. Mimi nitakupa tu vidokezo vya ripoti na kama nilivyokwambia awali wewe unatoa picha halisi ya argument yao.
Jamaa wanadai asilimia kubwa ya wafanya biashara ni wadogo wadogo na wanamitaji midogo, biashara nyingi azina malengo ya muda mrefu wa kukuwa, wanfanyabiashara mbinu zao ni very predictable na main aim kwa wengi ni ku-sustain life biashara ni kama vile alternative ya kipato cha ajira. Lakini si wafanya biashara wengi wanamalengo ya kuwa akina mengi wala bakhresa.
Hao middle men sum up the argument above that everything is done simply. Mfanyabiashara makini awezi kuchagua route na kusubiri soko lipate nguvu ndio ajishirikishe kama angekuwa na madhumuni ya kutanuka. Huyo anaonekana ni mtu wa kubahatisha na mwoga wa kuongeza risk. Just as unavyo suggest mkulima awe na sehemu ya kuhifadhi mazao, same as distributor anatakiwa awe na warehouse yake yeye mwenyewe kwa sababu za kibiashara, huwezi kuchagua sehemu ya kufuata mzigo kama wewe ni mfanyabiashara makini. Unachofanya ni aggregate cost na kuweka unit cost thats how businesses think kama ikibidi unaweza shusha bei so long bado unabaki na faida ili kuuza haraka. Lakini kwa kushindwa kufikiria faida za muda mrefu na kuja na mikakati ya muda mrefu ya kibiashara ndio maana wenzetu wanona wafanyabiashara wengi wameridhika walipo na wengi hawakui miaka nenda miaka rudi.
Na tatizo sugu litabaki vivo hivyo middleman asilimia kubwa ya wateja wake watakua wafanya biashara wadogo wadogo na awa ndio wanaowafikia walaji wa mwisho. Kwa mlolongo wa chain hiyo advantage ya economies of scale inapotea kwa kila mtu na kusababisha bei ziwe juu pia vilevile kwa mlaji. Kuna mengi hapo ya kufafanuliwa kibiashara na maelezo ya kisera lakini muda ndio tatizo kwa sasa no wonder kilimo akina mchango kwenye GDP yetu.
Jaribu kufuatilia TBL sasa hivi inavyowafaidisha wakulima kutokana na hiyo economies of scale, sasa tanzania kuna masupermarket mangapi, viwanda vingapi na mashirika mengine yenye huwezo wa kudemand large volume au hata wakulima wenye uwezo wa ku-supply large volume if asked. With that nimeifikiria point yako ya ushirika oops it just at the bottom.
Wenzetu huko magharibi hakuna wakulima wadogo wadogo ni corporations kubwa zinatumia machinery na kuhusika na zao tangia lipo shambani mpaka linaingia kwa mlaji sasa sisi badala ya kuleta wawekezaji watunyonye hao hao wakulima wadogo wadogo waungane na kutengeneza corporation yao itakayowasaidia kwenye manunuzi ya mbegu mpaka utafutaji wa soko as well as usafirishaji wa mazao
Mkuu sidhani kama ili swala umelifikiria kwa kina it is one thing kupigania maslahi ya pamoja mfano bei ya pamoja ya soko, sera za kuwasaidia wakulima na mengineo kwenye ya external environmnet yanayo changia kumkandamiza mkulima. However it is also another thing kuweka responsibility za pamoja, wewe umeona hii kama ndio njia ya pekee ya kutatua tatizo lakini mimi naona huu ndio mwanzo wa matatizo.
Maana kwanza apart from mazao mkulima mdogo ana hela yoyote ya mtaji wa kibiashara, sasa unapoenda kukopa benki kufanya unayotaka kuyafanya na business plan yako kama wataikubali si kwa sababu ya wakulima ni kwa sababu it is viable.
Suppose ndio imekubaliwa na wewe umeshirikisha wakulima, kutokana na mikakati yako ya muda mrefu una wa convince watu ambao kwa sasa wanalima wakati mapato ya mavuno ndio akiba ya mwaka mzima halafu wewe unawaambia wa-retain profit kwa sababu za kukuwa au una mbinu gani za kutanuka huko mbele mpaka ufikirie kujenga viwanda maghala , usambazaji na mambo mengine yanayo hitaji hela. (hivi uliona kwenye TV soko la geita lilivyo ungua sio kwamba watu wanalalamika tu, wamama wanalia hapo utadhani wamefiwa au kuna multiple killings, jamani tutakufa, baba raisi tusaidie watoto watakula nini yaani mpaka mimi nikajisikia vibaya wamama wanavyo bubujikwa na machozi kisa soko tu limeungua). Sasa umeshajuwa wakulima kipato chao kwa sasa kikoje, volume wanazozalisha, uhakika wa wewe kuuza bidhaa, faida zao zikoje kushirikiana na wewe, nani atakae control ushirika, maamuzi yakibiashara yana amuliwaje, mgawanyo wa mapato ukoje, mikopo inahudumiwa vipi kuna mlolongo wa mambo mengi ya kujibiwa kuliko kudhani ni swala la kuwaita wakulima mniamini mimi tufanye abc.
Mkuu najaribu kufupisha najikuta maelezo ayatoshi na sehemu zingine ngumu kumeza urekebsihaji unahitajika lakini muda auko upande wangu kama nilivyosema mada ikiendelea nitachangia zaidi yale ambayo sijajibu siku zijazo kwa leo majukumu yanaita sasa also bear with typos for now.