Tani Milioni 1 za ufuta zanunuliwa mkoa wa LINDI

"Leo (jana) tumeshuhudia Makampuni 3 kati ya 9 yakishinda tenda ya ununuzi wa ufuta wote uliokusanywa na wakulima wa Ruangwa,Nachingwea &Liwale(RUNALI).Mnada umefanyika ktk kijiji cha Mbondo,Bei ya Juu kwa kilo ni Tsh.2860 na wakulima wamekubali kuuza"~Rukia Muwango,DC Nachingwea
 
Kudanganya watu JF inabidi ujipange sana maana waungwana wanachambua hadi nukta.
 
Out of context. Idadi ya tani samahani. Nikusaidie, ni tani 1.88 million? Jibu ndio au hapana .
 
Ikithibitika ni kweli tani hizo zimepatikana Lindi tu.nikatwe masikio
 
Unapata mashaka ya nini,toa transport cost,toa mtaji ,toa ushuru etc.
Kama serikali inakusanya Kodi trillion 1 kwa mwezi unashangaa wafanyabiashara kufanya mauzo ya trillion 100 kwa mwezi,ikiwa tu hiyo Kodi ni asilimia 18 tu!!!
 
Unapata mashaka ya nini,toa transport cost,toa mtaji ,toa ushuru etc.
Kama serikali inakusanya Kodi trillion 1 kwa mwezi unashangaa wafanyabiashara kufanya mauzo ya trillion 100 kwa mwezi,ikiwa tu hiyo Kodi ni asilimia 18 tu!!!
Haiwezekani lindi pekee zipatikane tani mil 1.884!Hizi ni data za kupika!
 
nafikiri ni kilo na sio tani kwakuwa sioni ghala la kuhifadhi mzigo wote huo
 
Zitakuwa 188,400. Siyo milioni zote hizo lkn hilo zao nalo litavurugwa kubali usikubali
 
Ni kg siyo Tani... Mwandishi amenukuu vibayaaa..taharifa yake
 
Jamani wadau hebu tupeni data za kutosha kuhusu ufuta,ni kweli bei yake ni nzuri kiasi hicho?
Maana kama bei inapendeza,bora nipangishe nyumba yangu,nije huko kusini,niingie kwenye kilimo,maana hizi ajira,tumefanya karibu miaka 10,lakini benki hata 10M hakuna,na nje hata kupaki prado,hatuwezi
 


TANZANIA NDIO NAMBA MOJA KWA UFUTA DUNIANI.
 

Just google hiyo bei wakulima wamepigwa bei ya soko unaweza kuta ni mara tatu ya hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…