Kazi ipo wakuu sasa sisi wenye nchi wazalendoo.....tumebakia hatuna chetu wanatamba wao tu kazi kweli kweli....
Hapo awali niliandika na sasa narudia, dola ya Tanzania 'imetekwa' na mafisadi ndiyo maana wanaweza kufanya lolote na wasichukuliwe hatua. It is state capture in the contemporary political science literature.
Mafisadi wanachojaribu kufanya ni kuimarisha imaya yao, ili waisguswe na mtu yeyote kwa lolote wafanyalo. Tishio la Mengi limewagutua, na dola ikiwa ni mateka tayari, imeahidi na kuwahakikishia ulinzi na usalama wa mali zao. Haya ni maamuzi ya mkutano wa Kamati Kuu ya CCM uliomalizika jana. Watuhumiwa wote watahitisha press conference.
Anachokiita RA kuwa ni ushahidi dhidi ya Mengi na kwamba anaukabidhi katika vyombo vya sheria, ni nyaraka za uongo/kughushi zilizotengenezwa na mawakala wa genge la ufisadi Ikulu kwa lengo la kupata kianzio/kisingizio cha kuanza 'kumshughulikia' Mengi. Vinginevyo, RA hana intelligence machinery ya kukusanya huo 'ushahidi.'
Kama mengi angekuwa amefanya jambo lolote kinume cha sheria, serikali ya Mkapa ingekuwa imemshughulikia siku nyingi. Matamshi ya Mkapa mara baada ya kutinga ikulu mwaka 1996 kuwa alitaka kumfilisi Mengi ndiyo yaliyozaa ugomvi baina ya Jenerali Ulimwengu/HCL na Mengi. hatimaye mpango huo ulikufa mara baada ya kuingiliwa na Mzee Mwinyi, marehemu Ali Juma (RIP), Malecela na Msuya. Mkapa alishinikizwa kuacha mpango huo, na baadaye Mengi kulipa deni 'halali' lililokuwa linadaiwa na NBC. Huo ndio ukweli wa mambo na bila ushabiki nani zaidi kati ya papa na nyangumi.
Serikali (mateka wa mafisadi) itamfungilia Mengi mashitaka 'kifani' mahakamani, lakini yenye lengo la kuhadaa umma kuwa Mengi ndiye mkosaji ili kumwadabisha, kumfilisi na hatimaye kutoa ujumbe kwa watu wengine (umma) wenye nia ya kupambana na ufisadi, kuwa wasithubutu tena kuwagusa mafisadi walioteuliwa na dola. Na hapo ndio utakaokuwan mwisho wa mjadala na harakati zote za kupambana na ufisadi.
Vinginevyo, tusubiri kuona yatakayojiri, muda si mrefu kuanzia sasa.
Njia pekee ya kuendeleza moto wa vita dhidi ya ufisadi na hatimaye kuinusuru Tanzania ni watanzania wote kwa sasa kujitokeza kwa wingi, na kupitia njia mbali mbali, kuungana na harakati za Mengi kupambana na ufisadi. Si Tanzania wala watanzania, isipokuwa mafisadi, watakaopoteza kitu iwapo tutashiriki wote kikamilifu katika vita hii takatifu ya kuikomboa nchi yetu!