Tanker ya Mafuta yageuka isri ya Pombe haramu - Lita 10,000 za Ethanol zanaswa Kiambu

Tanker ya Mafuta yageuka isri ya Pombe haramu - Lita 10,000 za Ethanol zanaswa Kiambu

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
95
Reaction score
38

​
Polisi wamenasa tanker iliyokuwa ikisafirisha takribani lita 10,000 za ethanol inayoshukiwa kuwa ya viwandani katika eneo la Lari, kaunti ya Kiambu, kwenye Barabara Kuu ya Nairobi kuelekea Nakuru. Watu 3 waliokuwa ndani ya tanker hiyo wamekamatwa na wanasaidia uchunguzi.

Kilichozua maswali zaidi ni kwamba kwa mujibu wa polisi, tanker hiyo ilikuwa imefichwa kama gari la kusafirisha mafuta ya petroli. Mamlaka zinashuku mzigo huo ulikuwa ukielekea katika operesheni ya kutengeneza pombe haramu Nairobi.

Lakini kuna jambo moja muhimu: ethanol hiyo bado haijathibitishwa rasmi kuwa ni ' industrial ethanol' lakini sampuli zimepelekwa kwenye maabara ya Serikali huku uchunguzi ukiendelea. Kwa hiyo, kwa sasa kinachojulikana ni kwamba ni ethanol inayoshukiwa na uchunguzi bado unaendelea.

Lakini, kwa nini lita 10,000 ni habari kubwa? Kwa makadirio yaliyotolewa na Kamishna wa Kaunti ya Kiambu George Matundura, iwapo mzigo huo ungefika ulikokuwa ukienda na kutumika kutengeneza pombe, ungeweza kuzalisha bidhaa yenye thamani ya takribani shilingi milioni 28 kwa bei ya mtaani. Na hapa ndipo tukio hili linapoingia kwenye mjadala mpana unaoendelea nchini kuhusu pombe haramu na msako dhidi ya uzalishaji na usambazaji wake.

Kwa wiki za hivi karibuni, mjadala mkubwa umejikita zaidi kwenye bidhaa inayopatikana kwa mlaji wa mwisho, pombe inayouzwa mitaani, viwanda visivyoidhinishwa na biashara zinazokiuka sheria. Lakini tukio la Lari linaibua upande mwingine wa suala hilo: nao ni mtandao wa usambazaji wa malighafi.

Ikiwa tuhuma za mamlaka zitathibitishwa, swali si tu nani alikuwa akisafirisha hiyo tanker, bali pia:

Mzigo ulitoka wapi? Ulikuwa unaenda kwa nani? Na ni nani alikuwa nyuma ya mpango huo?

Soma pia
 
Back
Top Bottom