Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
Nilikuwa nasafiri hivi karibuni nikitoka Shinyanga kwenda Igunga, nikiwa kwenye gari sikuamini macho yangu, kama kilometa mbili kabla ya kufika Stendi kuu ya mabasi Nzega, barabara imeliwa na vile mvua zinanyesha kila wakati kila dereva anapita anakojua.
Kama Barabara itaendelea kuwa vile kuna hatari ya ajali kutokea, maana kama dereva ni mgeni anaweza kujitungua akajikuta mtaroni hivyo Tanroad mkoa wa Tabora hakikisheni ile baranabara hususan kile kipande kinatengenezwa ili kuweka usawa.
Ni kero kuwa na aina ya Barabara kama ile kusema ukweli.