Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Hayo ni maelezo ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) baada ya hoja iliyotolewa na Mwananchi kupitia Jukwaa la JamiiForums.com aliyehoji barabara hiyo kutowekewa sehemu za magari kusimama ikitokea kuna dharura ili kutoziba magari mengine kupita.
Maelezo zaidi ya TANROADS:
Ni muhimu kuelewa kuwa barabara hii imebuniwa kwa viwango vya kisasa vya Expressway (high-speed controlled access road), ambapo lengo kuu ni kuruhusu magari kusafiri kwa kasi na usalama zaidi bila kusimama ovyo barabarani.
Baada ya kukamilika, barabara hii itakuwa na miundombinu muhimu ikiwemo:
Vituo vya mapumziko (Road Side Stations - RSS) kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara.
Sehemu za kugeuzia magari (U-turns) zilizopangwa kitaalamu kila km 3-5.
Barabara za huduma (service roads) kwa ajili ya shughuli za maeneo jirani na biashara.
Hata hivyo, miundombinu hii yote inawekwa kwa umakini mkubwa ili kulinda dhana ya barabara ya mwendo kasi (expressway), ambapo kusimama ovyo barabarani hakuruhusiwi.
Kuondoa miundombinu hiyo kutasababisha magari kuingia ovyo barabarani, kuongeza ajali na kuharibu kingo za barabara na kupunguza ubora na hadhi ya barabara kuwa ya kawaida badala ya expressway.
TANROADS inaendelea kukamilisha kazi zilizobaki, na tunaomba wananchi na watumiaji wa barabara hii wawe na uvumilivu katika kipindi hiki cha mpito.
Lengo letu ni kuhakikisha tunakuwa na barabara salama, ya kisasa na yenye kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya usafiri nchini.
Madai yalivyokuwa: DOKEZO - Responded - Barabara ya kupunguza foleni Dodoma ni mpya lakini imejengwa kizamani, hakuna sehemu ya gari kupaki kwa dharura