TANROADS epukeni mfumo wenye traffic lights kwenye barabara kuu zilizo na magari mengi, kwanini mnatuangusha kama hamna utaalamu?

TANROADS epukeni mfumo wenye traffic lights kwenye barabara kuu zilizo na magari mengi, kwanini mnatuangusha kama hamna utaalamu?

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Nimeshindwa na kutoelwewa kwa nini TANROADS wanajenga mifumo ya flyover ambayo inahitaji taa za kuongoza magari (traffic lights) kwenye barabara zilizo busy. Mfano ni flyover za Ubungo, Tazara na junction ya Kilwa road/Mandela road. Ni kwa nini TANROADS wanatumia mifumo ya flyover sehemu kama hizi ambayo haistahili na inawekewa taa za kuongoza magari?

Flyover kwenye barabara busy kama hizi lengo lake ni kufanya kuwe na mtiririko wa magari usiosimama. Lakini sasa TANRAODS wanafanya completely the opposite. Wanaweka flyover ambazo bado zinasababisha follen.

Kwa mfano, flyover ya Ubungo. Ukitoka Mwenge unaenda Mororgoro inabidi upite chini kisha usubiri kwenye trffic light ali kukata kna kulia. Hili ni kosa. Flyover hii ilitakiwa iwe designed kisi kwamba wanaotoka Mwenge kwenda Buguruni na wa Buguruni kwenda Mwenge wanapita moja kwa moja juu kama ilivyo sasa, kisha chini yake wakapita wanaotoka Morogoro, wanakikata kushoto, chini ya njia hii wanaotoka Mwenge kwenda mjini. Kwa hiyo kungekuwa na "ghorofa" mbili za bararaba.

Jambo la msingi ni kwamba TANROADS wanatakiwa wa design flyover ambazo hazitahitaji traffic lights sehemu kama hizi. Nadhani wameona vurugu inayosababishwa pale Ubungo na Tazara, lakini bado wanaendelea na design hizo hizo zenye kasoro.

Halafu pia, limekuwa ni kosa sana barabara ya airport ilikuwakuwa dual caariage way hapo mwanzo bila lanes za Mwendo kasi, kurudishwa tena na kuwekwa four lanes zile zile. Hili ni kosa ambalo halitatatua foleni ya barabara ya Nyerere kwenda airport. Mwendokasi hautapunguza kero ya foleni kwenye barabara hii kama ambavyo tumeona Mwendokasi haujapunguza foleni barabara kati ya Ubungo na Kimara. Hii barabara ya Nyerere kwenda airport ilitakiwa iwe na njia ya Mwendokasi pamoja na three lanes kila upande wa njia ya Mwendokasi.

TANROADS, acheni kufanya mambo kwa mazoea. Think 50 years ahead of now!
 
Kichwa cha habari kilipaswa kuwa

TANROADS epukeni mfumo wenye traffic lights kwenye flyover za barabara kuu zilizo na magari mengi, kwa nini mnatuangusha kama hamna utaalamu?​

 
Back
Top Bottom