TANROADS Katavi yalipa fidia ya Tsh. Bilioni 2.4 kupitisha ujenzi wa barabara ya kwenda Bandari ya Karema

TANROADS Katavi yalipa fidia ya Tsh. Bilioni 2.4 kupitisha ujenzi wa barabara ya kwenda Bandari ya Karema

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Zaidi ya fedha Bilioni 2.4 zinatolewa kwa Kaya 435 za Wilaya ya Tanganyika, Mkoa wa Katavi kwa ajili ya kupisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa Kilometa 112 kutoka Kijiji cha Kagwira hadi Bandari ya Karema.

Ujenzi wa barabara hiyo ya lami unatajwa kuwa kichochea cha shughuli za bandari hiyo iliyojengwa kwa fedha zaidi ya Tsh. Bilioni 47.9 huku matarajio ni kuongeza mtandao wa biashara katika nchi za Burundi, Rwanda na DRC Congo.

Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Katavi, Mhandisi Albert Laizer amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo utakwenda kutibu kero ya foleni za magari mengi yanayosafirisha bidhaa kwenda nchi ya Zambia kwa kupitia barabara ya Mbeya - Tunduma.
 
Back
Top Bottom