TANROADS mnatutesa sana barabara ya Mbezi High School kwenda Bunju kupitia Mpigi Magoe

Kwaasenga

Member
Joined
Jan 28, 2023
Posts
74
Reaction score
104
Hii barabara ni kero sana tena sana. Mbunge wetu anaishia kutupanga kila mara. Hii barabara isipotengenezwa mpaka 2025 tutaona hakuna tofauti kati ya mbunge huyu aliyepo na yule aliyekuwepo.

Haiwezekani barabara ikawa mbovu kiasi hiki wakati huo sisi tuna mwakilishi. Mzee Magufuli (RIP) aliagiza hizi barabara kuu moja wapo ikiwa ni hii ya Mbezi high, zifanyiwe ukaguzi kwa ajili ya kuziwekea lami, lakini alivyofariki tu na kila mpango ukafa.

Tanroads, kwani ni nani ambaye huwa anatengeneza bajeti na kuingiza barabara zinazotakiwa kujengwa??
 
Hii barabara ni kero sana tena sana. Mbunge wetu anaishia kutupanga kila mara. Hii barabara isipotengenezwa mpaka 2025 tutaona hakuna tofauti kati ya mbunge huyu aliyepo na yule aliyekuwepo...
Si nilisikia imeanza wekwa lami?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…