TANROADS: Ni kweli Mkandarasi wa Mradi wa Mwendokasi Mwenge - Tegeta anasuasua, Serikali imechukua hatua za Kimkataba

TANROADS: Ni kweli Mkandarasi wa Mradi wa Mwendokasi Mwenge - Tegeta anasuasua, Serikali imechukua hatua za Kimkataba

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Uongozi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) umetoa ufafanuzi kuhusu hoja ya Mdau wa JamiiForums.com aliyeandika Ujenzi wa Mwendokasi Mwenge -Tegeta utakamilika lini? Ni kweli Mkandarasi ana vifaa vichache, wafanyakazi hawatoshi?
IMG-20260604-WA0000.jpg
UFAFANUZI WA TANROADS:
Serikali kupitia TANROADS inatambua umuhimu wa Mradi wa Mwendokasi Awamu ya Nne (BRT Phase IV) kutoka Mwenge hadi Tegeta katika kupunguza msongamano wa magari na kuboresha huduma za usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam.

Mradi huu unatekelezwa na mkandarasi wa Kampuni ya Shandong kutoka China. Hata hivyo, utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kwa muda licha ya juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali kupitia TANROADS kuhakikisha unakamilika kwa wakati.

Mkandarasi alielekezwa kuongeza vifaa, wafanyakazi na kuendesha kazi kwa saa 24 ili kuongeza kasi ya ujenzi, lakini hatua zilizochukuliwa hazikuleta matokeo yaliyotarajiwa.

Kutokana na hali hiyo, na kufuatia maelekezo ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Serikali kupitia TANROADS imechukua hatua kali za kimkataba dhidi ya mkandarasi huyo.

Hatua hizi zinaonesha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika, kwa wakati na kwa kuzingatia thamani ya fedha za umma.

Hatua hii itakuwa fundisho kwa wakandarasi wote wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa mikataba waliyoingia na Serikali, ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati na wananchi wanapata manufaa yaliyokusudiwa.
 
Khaaa.... hadi wakumbushwe ndipo wachukue hatua!!
Huyo mtendaji mkuu wa mradi inatakiwa awajibishwe kwanza kabla ya huyo mkandarasi
 
Kuna top layer ikiongozwa na rais wa kokoto walishagaiwa mapande yao.. Huwezi kuwasikia wakinyanyua midomo
 
Kutokana na hali hiyo, na kufuatia maelekezo ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Serikali kupitia TANROADS imechukua hatua kali za kimkataba dhidi ya mkandarasi huyo.

Hatua hizi zinaonesha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika, kwa wakati na kwa kuzingatia thamani ya fedha za umma.
Hatua gani? Inawezekana serikali imechukua hatua kwenda mbali na mkandarasi
 
Back
Top Bottom