TANROADS : Tunaboresha alama za barabarani (Zebra) ambazo zimefifia na kufutika kwenye njia za Dar

TANROADS : Tunaboresha alama za barabarani (Zebra) ambazo zimefifia na kufutika kwenye njia za Dar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
photo_2026-04-15_18-23-42.jpg

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wameeleza kuwa wanakuchukua hatua madhubuti za kuimarisha usalama wa miundombinu ya barabara kwa kupaka rangi mpya kwenye alama mbalimbali za barabarani zilizofifia hususan alama za watembea kwa miguu (zebra crossing) katika Mkoa wa Dar es salaam ili kuhakikisha zinabaki katika hali nzuri na rafiki kwa watumiaji wote.

Taarifa waliyoitoa leo April 15, 2026 imeeleza "TANROADS imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha usalama wa miundombinu ya barabara kwa kufanya ukarabati na upakaji rangi mpya kwenye alama mbalimbali za barabarani, hususan alama za watembea kwa miguu (zebra crossing), kwa lengo la kupunguza ajali.
photo_2026-04-15_18-23-41.jpg
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha barabara zinabaki katika hali nzuri na rafiki kwa watumiaji wote, wakiwemo madereva na watembea kwa miguu ambao ni miongoni mwa makundi hatarishi"

"Katika utekelezaji huo, alama zilizofifia au kufutika zinapakwa rangi upya ili kuongeza uonekano wake, hatua inayowasaidia madereva na watembea kwa miguu kuzitambua kwa urahisi na hivyo kupunguza ajali zisizo za lazima." imeeleza taarifa

Taarifa hiyo imeendelea kueleza "Aidha, maboresho hayo yameongeza mwonekano wa alama hizo hususan nyakati za usiku au wakati wa mvua, hali inayochangia madereva kuchukua tahadhari mapema wanapokaribia maeneo ya kuvuka barabara."

Wameeleza kuwa zoezi la kuboresha alama hizo kwa sasa linaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, likiwemo eneo la makutano ya barabara karibu na ITV, pande zote mbili, pamoja na kituo cha mabasi ya daladala cha ITV Mwenge.

Aidha TANROADS imeeleza kuwa , zoezi hilo ni endelevu na litaendelea kufanyika katika maeneo yote ambayo alama za barabarani zimefifia au hazionekani kwa urahisi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha barabara zinakuwa salama na zenye viwango vinavyokubalika.
photo_2026-04-15_18-23-39.jpg
 
Back
Top Bottom