The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Kwenye mazungumzo na wanahabari jijini Dar es asalaam Mhandisi Besta amedokeza kuwa mpaka sasa mchakato wa manunuzi kwaajili ya ujenzi wa kipande cha barabara ya Mbagala Rangi tatu - Kongowe 3.8km kwa upanuzi wa njia 4 umeanza na utakamilika ndani ya wiki 4.
Aidha Mhandisi Besta ameongeza kuwa kwa kipindi cha miaka 4 cha Rais Samia hadi kufikia sasa karibu theluthi ya barabara zote nchini zimejengwa kwa kiwango cha lami na kuchochea uchumi kwa jamii zinazopitiwa miradi ya barabara hizo.
==========================
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Mohamed Besta, amesema Barabara zilizopo chini ya TANROADS zenye Kilometa 12,022 zipo kwenye Kiwango cha Lami.
Ameyasema hayo leo tarehe 07 Machi, 2025 wakati akiongea na Wanahabari kuhusu Miradi mbalimbali ambayo inaendelea Nchini ikiwemo ya barabara, Madaraja pamoja na Viwanja vya ndege.
Besta amesema theluthi ya Barabara zilizopo chini ya TANROADS ni za Lami.
"Mpaka sasa katika Nchi yetu tuna Kilometa 37,300 za urefu wa barabara ambazo zimekasimiwa na TANROADS na kati ya hizo Kilometa 12,022 zipo kwenye Kiwango cha Lami. Vilevile TANROADS inasimamia Madaraja 9,563 Nchi nzima ambayo yameshajengwa kwa awamu zote 6. Ndani ya Miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kukamilisha miradi 8 Mikubwa ya Madaraja Nchini na kuna Miradi 10 mingine ya Madaraja inaendelea kujengwa. Amesema Mhandisi Besta.
Mhandisi Besta amesema katika kindi cha miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan TANROADS wameweza kujenga Kilometa 1366 za barabara ambazo ni Wastani wa Kilometa 400 kwa Mwaka.
Mhandisi Besta amesema TANROADS ina Kilometa 15,225 ya Miradi ambayo ipo kwenye hatua mbalimbali ya kujengwa na kufanyiwa Upembuzi yakinifu.
Mhandisi Besta ameongeza kuwa kuna Miradi ya Viwanja vya ndege inaendelea kujengwa na vipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezani na vingine vimekamilika.
"Kiwanja kwa mfano cha Msalato kimefikia katika hatua nzuri na Vilevile na Viwanja vingine vya Mkoa kama vile Shinyanga, Sumbawanga, Musoma, Kigoma na Kwingineko. Na kuna miradi ambayo imekamilika kama Mtwara, Songea pamoja na Songwe". Amesema Mhandisi Besta.
Katika Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Besta amesema Manunuzi ya Barabara ya Kilwa kutoka Mbagala rangi tatu mpaka Mbagala Kongowe Kilometa 3.8 yatakamilika Wiki ya nne ya Mwezi Machi 2025.
Mhandisi Besta amehitimisha kwa kisema kwamba hii barabara itajengwa kwa njia nne kama Rais Samia Suluhu Hassan alivyoagiza kwani hio barabara ina Msongamano sana. Tumeshafanya majadiliano na Mkandarasi ambaye amata mradi huu kuangaalia jinsi ya Kupunguza Msongamano.
=======================
Video ya Khan Mbarouk
Video ya Khan Mbarouk
Pia soma:
~ Barabara ya Mbagala hadi Kongowe ni nyembamba, ina mashimo na inasababisha foleni mara nyingi
~ Meneja TANROADS aelezea ulipofikia mchakato wa Ujenzi wa Barabara ya Mbagala Mzinga - Kongowe - Kisemvule
~ Barabara ya Mbagala hadi Kongowe inatesa wananchi Serikali itupie jicho