Utatokwa na kamasi bure ukizungumzia sykes na mzee wetu hapa Mo said[emoji23]
Nahisi Alipenda sana kuona sykes angekuwa kiongozi wa taifa hili lakini siyo yule
Na kwa upande wangu sykes namuona kama alikuwa na umagharibi zaidi,bepari
Nahsi angetawala tanganyika ingekuwa kama ulaya
Ova
Mrangi,
Abdul Sykes hakuchukulia siasa kama ajira kwa hiyo ashike nafasi ya siasa ili nafasi hiyo imwendeshee maisha yake.
Kwa ajili hii basi si Abdul wala Ally walikuwa na haja ya nafasi za siasa.
Mchango wao mkubwa katika TANU ulikuwa kufadhili harakati za uhuru.
Ukweli ni kuwa hawa ndugu wawili wakipenda sana biashara kama alivyokuwa baba yao.
Mwaka 1953 majina ambayo Abdul Sykes na Hamza Mwapachu walikuwa wakiyajadili kushika uongozi wa TAA na 1954 waunde TANU yalikuwa majina mawili jina la Chief David Kidaha Makwaia na Julius Kambarage Nyerere.
Jina la Abdul Sykes halikuwapo.
Je, mlikuwa mnaijua historia hii bila ya mimi kukuelezeni?
Mnaujua mkutano nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio, UkereWe kati ya Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe ulioamua kuwa Nyerere aingizwe kwenye uongozi wa TAA?
Ndugu zangu isomeni historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika kuna mengi sana hamyajui.
Someni kitabu cha Abdul Sykes.