bahati93
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 1,334
- 2,463
Serikali changa ya mwalimu Julias Kambarage Nyerere ilikabiliwa na changamoto nyingi sana. Mwalimu aliwahi kuainisha mojawapo ya changamoto kuu: Ujinga, Magonjwa, na Umaskini. Hata hivyo mnamo mwaka 1975 serikali ya TANU ilikaa kujadili juu ya kile walichoona kuporomoka kwa maadili.
Vitu vilivyokera kamati ya TANU ni kutokana na wanawake kuvaa vimini na mawigi vitu vilivyoonekana kama utamaduni wa nchi za mabeberu. Hata hivyo sio viongozi tu walikereka bali hata raia hali iliyopelekea kufanya maandamano ya amani jijini dar es salaam waliandamana kupinga mawigi kwa kusema "mywele za maiti"," makatani" na walichukizwa na vimini kwani bibi zao walikuwa wakitinga mabaibui.
Haki ya nani haya maisha yamejaa vituko vingii sana, ni burudani kuangalia ujinga unaofanywa na jamii fulani ambayo jamii yako imeshapita! Wazungu wanatuenjoi sana harakati zetu ambako wao walipitia huko zamani sana. Na kama endapo viongozi wetu na jamii ingefuatilia kwa umakini history kutoka kwa jamii kongwe huenda tungeepuka kurudia mistake walizofanya. Ukija kwa viongozi wa tanu enzi hizo tayari walikuwa wanajua maadui ni kina nani lakini cha ajabu wakaanza kukamata wakina mama na wadada wanaovaa mawigi na vimini.
Chanzo: kumbukizi za mwalimu, TBC,0830Hrs, 14/10/2021