Tanzania 0-3 DR Congo | 2022 FIFA WC Qualifiers | Benjamin Mkapa Stadium

Tanzania 0-3 DR Congo | 2022 FIFA WC Qualifiers | Benjamin Mkapa Stadium

Kufungwa stars huwa najisikia km nimetua mzigo mzito.

Burudani yoyote nikishaona wanasiasa wameingia basi huwa naichukia. Upuuzi kila kitu kinafanywa mtaji wa siasa.

Acha wachezaji wetu watulie kwenye klabu zao ligi iendelee.
 
Kesi haijafika mwisho....

Hapo unayo hukumu yake?!!!!
Beni, Kivu Kaskazini huko ni suala la waasi (ADF, M23, Lord Resistance, nk) dhidi ya wakongo. Wakongomani wako pamoja dhidi yao.

Kwetu ni serikali yaani Sirro, Kingai, Sabaya na binamu zao dhidi yetu.

Siyo siri umoja wetu kama watanzania haupo tena.

Mshikamano haupo tena
 
Faida ya wachezaji kukipiga ligi kubwa na nzuri inaonekana,sisi huku wanasubiri Hadi mtu au watu wapate mafanikio ndo wapongezwe wakati haya Mambo yanaanzia nyuma kabisa huwezi kukimbia wakati hata kutembea huwezi,Yani tunajipa ndoto nzuri wakati hatukuziandaa haiwezekani kabisa ufanikiwe kisoka bila kuwa na mikakati sahihi Kama serikali na mashirikisho yetu ya soka,Bora kabisa hao Kongo wametupiga ili Basi nao wakutane na wa saizi yao sisi hata rwanda Nina wasiwasi kuwa hatumfungi...lakini tunahitaji watu kweli wakufanya vitu vizuri...
 
Wiki nzima kabla ya mechi ya Stars na DRC kulikuwa na pilikapilika za ofisi ya Waziri Mkuu kuhangaika na ahadi kedekede kwa Stars ikiwa watashinda game hii , INAFAHAMIKA MADHARA ya ahadi kama hizi kuelekea kwenye mechi muhimu kama hii , Matokeo yake ni tensheni ya kufa na kupona huku wachezaji wakiwaza ahadi walizopewa tu .

Iko haja sasa kwa TFF kudhibiti wanasiasa uchwara wanaotafuta umaarufu kupitia timu ya Taifa huku wakifahamika kwamba kwenye enzi zao hawakuwahi kupiga danadana hata mbili , wanaua morali ya wachezaji .
@Moderator umewezaje kupata ujasiri wa kuunga uzi huu ?
 
Back
Top Bottom