Tanzania 2026 bila utekaji bila wasiojulikana. Bila kuwa Wauaji wa watu wetu wenyewe

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

1. Moja ya mambo yaliyonifanya niandamane na kunusurika kuuawa ni pamoja na kupinga Utekaji, mauaji, wasiojulikana na siasa zisizo za haki kwa wapinzani. Ingawaje sina chama lakini mimi ni mdau na mpenda haki.

2. Nakereketwa na kukerwa nikisikia mtu Fulani kapotea katika mazingira ya kisiasa na mwili wake kutopatikana au kupatikana umeuawa kikatili.

3. Sijui nilifikaje huku. Na sina hakika nitatoka kwani nahisi ni wito. Kuna wakati najiuliza ilikuwaje nikajiingiza kwenye mambo haya. Nilikuwa mfuatiliaji WA kimyakimya WA mambo ya siasa tangu nikiwa O level. Lakini sikuwa najihusisha kabisa.

4. Uhusika wangu ulikuwa kwenye DINI na mambo ya masomo, taaluma, falsafa, lakini huko pia nilijikita kwenye mambo ya haki.

5. Mimi ni wale ambao sipendi mtu akionewa hata kama simjui, hatujuani, sihusiani naye. Hata kama ni adui Yangu sipendi aonewe. Napenda Haki.

6. Mara ya Kwanza kuandika mambo ya siasa ni mwaka 2015. Tangu Siku hiyo nimeingia katika shimo lenye kina cha mateso. Pengine nimekuwa mgonjwa. Naugua magonjwa ya HAKI.

7. Haiwezekani Kila ukisikia uonevu popote uumie. Huu ni ugonjwa nawaambia.

8. Wakati mwingine ninajiuliza kwa nini unapigania haki. Kwa nini unazungumzia Haki.

9. Watu Fulani mara kadhaa huwasiliana na mimi. Wakisema, unatetea haki unawajua hao? Mwenyewe najiuliza hivyohivyo lakini mwisho wa Siku moyo unaninyima AMANI. Kwamba usiposemea na kutetea haki na ukweli. Nitakunyima Amani. Hutaishi maisha ya furaha. Kweli inakuwa hivyo.

10. Namshukuru Mungu Kwenye Maisha Yangu sijawahi kuonewa, wala kudhulumiwa. Sijawahi kuumizwa personal lakini naumia kupitia maumivu ya wengine.

11. Dhulma na uonevu havipaswi kuwa sehemu ya jamii na taifa letu.

12. Tunahitaji Haki hata kama hatujawahi kunyimwa. Tunapigania haki na kuitetea sio kwa sababu maslahi yetu yameguswa. Hapana. Tunapigania haki kwa sababu haki ni Amani, furaha na upendo.

13. Mwaka 2026 ni mwaka wa nuru mpya. Mwaka usiokuwa na utekaji, mauaji, na wasiojulikana.

14. Watekaji na wauaji wa ndoto za wanawake na vijana.
15. Wasiojulikana wanaojiingiza kwenye maisha yako na kuyaharibu huku ukidhani unawajua lakini huwajui kwani nje ni kondoo lakini ndani na mbwa mwitu.

16. Watekaji wa akili na mioyo ya watu na kuiua kwa kile kiitwacho mapenzi na ndoa bandia.

17. Wauaji na watekaji na wanaharakati na wanasiasa wenye mawazo kinzani na wao. Wote hao mwaka huu wasiwepo.

18. Watesaji na wanaodhulumu pesa za nauli wote hawa ni wasiojulikana.

19. Nuru mpya iangaze katika mioyo ya watu zenye roho za mauaji. Watu waliogeuza nafsi zao kuwa kuzimu. Na kuua watu wasio na hatia.

20. Wale waliokata tamaa kuwa Wema tena kutokana na maovu walioyafanya huu ni wakati wa kuruhusu nuru ifukuze Giza katika mioyo yao. Mwaka 2026 usikate tamaa. Bado unanafasi ya kuwa Mtu mwema na mwenye kuonyesha Wema wako kwa Watu.

Kufikia hapo sina la ziada. Nawatakia Siku njema.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Tuko wengi kama wewe,mifano michache ni Tundu Lissu,unazani anashindwa kuchukua hera ndefu halafu akahamia CCM na kupewa Uwaziri juu,lakini nafsi yake imesimama kupigania haki na kuwatete Watanganyika na rasilimali zake
 
Back
Top Bottom