Luca Paguro
JF-Expert Member
- Mar 26, 2023
- 502
- 1,141
Ukiachana na mambo ya katiba, uhuru wa kuongea, hiii ndio Tanzania ambayo vijana wengi wanatamani kuiona kipindi hiki cha uhai wao
1. Tanzania yenye viwanda tele ikiwemo viwanda vikubwa vya magari, laptop, simu na pikipiki. Viwanda viajiri watanzania wengi na bidhaa tuuze nchi jirani. Malighafi yote ya msingi kwa ajili ya viwanda yapo nchini
2. Tanzania yenye kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kisichotegemea mvua, na kutumia matrekta makubwa yenye majembe 50+ badala ya jembe la mkono
3. Tanzania yenye vyuo vikuu kila kona, na vyuo vikubwa sana kama UDSM na UDOM viwepo kama 50 hivi huku vikiwekeza zaidi kwenye research na development
4. Hospitali kubwa kama Mloganzila ziwepo hata 30 hivi nchi nzima, ziwe zinatoa huduma bora chini ya madaktari wasomi wa Kitanzania
5. Tanzania yenye makampuni mengi ya serikali na wazawa ya uchimbaji madini ambayo yanamilikiwa na Watanzania, yanatumia mashine za kisasa na mainjinia wa Kitanzania
6. Miji iliyoendelea kwenye fursa za ajira na mikubwa kama Dar es Salaam iwepo walau 20 hivi nchi nzima
7. Vipato vya Watanzania vikue, gharama za usafiri zishuke, huduma ziboreshwe ili Watanzania waongeze kusafiri kwa ndege kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine na shirika letu la ndege likue
8. Treni nzuri za umeme kama SGR ya Dar-Dodoma ziwepo route nyingi hapa Tanzania mfano route za Mtwara-Mbeya, Mbeya-Dar, Dar-Arusha, Arusha to Mwanza, Mtwara to Dar, Kigoma-Mwanza nk
9. Kuwe na mitambo mikubwa ya kupurify maji kutoka Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa, mabomba yawe installed maji yasambazwe nchi nzima yawe yanayoka bila kukatika 24/7
9. Gesi yetu ya Lindi na Mtwara iwe utilised na inufaishe Watanzania na kushusha gharama za gesi ya kupikia nchini ili Watanzania waache kutumia kuni na mkaa
10. Kila mji uwe na dustbin kubwa nyingi za kutosha kila mtaa na kuwe na CCTV camera kuhakikisha watu hawatupi taka chini hovyo badala yake watupe kwenye dustbin
11. Nchi inunue matrekta makubwa mengi ije kukodosha kwa bei kitonga kwa wananchi
12. Tanzania inayozingatia mipango mji na upandaji wa miti na nyasi kwenye neighbourhoods
13. Tanzania ambayo ina fursa tele kama vile ilivyokuwa Marekani. Asilimia kubwa ya watu ambao serikali imetumia mabilioni kuwasomesha wasiishie kuwa mawinga bali yaandaliwe mazingira jinsi watu hawa wataliingizia faida taifa
14. Tanzania ambayo maghorofa yote marefu, madaraja na barabara za lami zinajengwa na mainjinia wa Kitanzania ambao serikali imetumia mabilioni kuwasomesha
15. Tanzania ambayo elimu yetu inapaswa iwe ya mfano Africa nzima
16. Tanzania ambayo ina GDP kubwa na mzunguko mkubwa wa hela ili kuwe na mazingira rahisi kwa wanaojiajiri. Watu wake wapate hela wawe wanajenga nyumba kali hadi vijijini.
17. Tanzania ambayo umeme kukatika inabaki kuwa story tu
Kuna watu mtaona naongea pumba, au ndoto za mchana au labda nina tamaa za ajabu lakini kwa nchi kama Tanzania ikiamua inaweza kwa sababu zaidi ya 66% ya hii nchi ni vijana ambao ndio wana uwezo mkubwa wa kujenga taifa ikiwa kutakuwa na sera nzuri, utekelezaji na uwajibikaji. Pia Tanzania ina resources za kila aina. Zinatungoja siku akili zetu zikiamka tuanze kuzitumia
Binafsi naamini tukiamua tunaweza, kama tu China ilivyopata mabadiliko makubwa kwa miaka 30 tu kutoka 1990 hadi 2020. Maana yake Wachina walioishi kipindi hiki waliishi maisha ya furaha sana kuiona nchi yao ikikua kwa kasi kipindi cha uhai wao. Hata sisi tunaweza siku tukiwa serious
Tunaweza kuwa wa mfano kwa Africa, tusizifanye nchi za Africa zenye hali mbaya kuliko Tanzania kuwa role model wetu, tuige nchi zilizofanikiwa
Kama tukianza sasa kuwa serious basi ndani ya miaka 15 hadi 20 tu miji ya Tanzania itakuwa hivi
(Hizi picha zimetengenezwa na AI ili tu kuexpress mawazo ninayowaza akilini mwangu kila siku)
1. DAR ES SALAAM
2. DODOMA
3. ARUSHA
4. MUSOMA