mkuu ni kwamba, waalimu ahueni/afadhali wa tz ni wale waliosoma ualimu chuo kikuu nao wameenda kwa kuungauna kwasababu kwa kawaida ya tz mtu aliyefaulu vizuri huwa hadondokei kwenye ualimu. hivyo kumwajiri mtu aliyemaliza chuo kikuu afundishe nursery hautampata hata mmoja pamoja na kwamba mshahara nitakaomlipa ni mkubwa kuliko ule anaopokea serikalini usiozidi hata laki saba kwa mwezi kabla ya makato. unaishia kuwapata ambao hata university hawajafika ambao ni wabovu tu kichwani kiingereza cha kukariri kama wewe.
tukija kwa wakenya, kule wasomi wengi hivyo kuna competition sana ya kupata kazi, kulipwa mshahara mdogo ni kawaida sehemu zenye uhaba wa ajira. hivyo wakija huku wakilipwa more than one million or so, kwao ni hela nyingi, na wanafanya kazi vizuri sana. watoto waliofundishwa na wakenya ambao wametumia kiingereza tangu chekechea hadi chuo wanakuwa vizuri kuliko watoto waliofundishwa na watz waliotumia kiingereza kwa mara ya kwanza form one.acheni kukimbia ukweli.