Cha msingi siku zote babako akiwa na ugomvi na jirani, wewe kama mtoto utakua na mtazamo wa kumtetea babako bila kutaka kujua kama yeye kachokoza, labda hata amekojoa na kuharisha kwenye mlango wa jirani lakini hayo yote hutayaona. Utakua ukisema nyie ndio mnachokozwa.
Kwa ufupi ni kwamba nyie manafahamika kuwa na migogoro na majirani zenu, huwa hamuendani na yeyote, nakumbuka kipindi mlimsumua sana Kagame hadi nursa iishie kwenye vita. Leo hii mnachokoza Malawi, mumewakuta wameishi kwa amani tayari mnawachokonoa, ipo siku nilisoma hata Wazambia mumewazingua sana kwenye ile reli ya TAZARA.
soko bora ni la ndani hata china walianza hivyo,tuzalishe tunavyovitumia na baadae tuzalishe tusivyovitumia.
kuhusu EAC tuliwekeza kwa Gharama mno yaani damu na nyama tuliamini sisi ni wamoja,kenya walichotufanya watanzania shetani na mungu wanajua na hapo ndio tz ikajua malengo ya wakoloni kupitia kenya.
kagame tumemlea na sasa kakua na akaona tz si bora bora kenya kwa kua staili za maisha wanaendana tukasema nenda ila alitaka ajaribu mtiti wa jwtz na km kawaida tukiingia lazima tuweke kiongozi wa muda na kwa gharama yeyote tungeshinda.
malawi hakuanza leo na kuna enzi za mwl alipelekewa tu ka bataliani kamoja akafuta usemi na analijua hilo suala la ziwa linaibuka wakati wa uchaguzi wao sisi huwa hatubadili msimamo ila tunabadili namna ya kuendeleza msimamo.
tuna soko visiwani komoro madagaska na SAdcc kuanzia mazao na wataalamu wetu.
zambia anajua mziki wetu kwenye tazara na hapendi kuligusia maana anajua tukiamua huwa hatugeuzi macho.
wale waliokuwa wanajiita umoja wa walio tayari kwenye EAC wamejua umuhimu wa tanzania km shock absorber ya shida zao na tukijitoa hawako salama.
kupitwa na uganda sio mbaya cha msingi wananchi wana amani,ww ukipitwa na ndg yako unamuwekea bifu?
sasa tunasoko kubwa la asali asia wala hatuhitaji soko la ulaya kwa kupitia kenya.
korea kaskazini wana vikwazo ila mbona wako mbele kimaendeleo kuliko hata nchi nyingi za afrika ?ambazo zimefungua milango kwa mabeberu na vibaraka wa wazungu?shida huleta maarifa mlipoombwa kwenye kikao chaEAC mlisema mekubali kufungua mpaka,wanatu wanapeleka unga nyinyi mnawakatalia mnasema ilikua maneno ya kikao bado aproval ya utekelezaji,na sisi kuwakubalia kikao tunasubili utekelezaji mnaona tunachelewesha.
tanzania tunafuga mifugo mingi hivyo maziwa na nyama si kitu ambacho adimu mpaka tupate hayo ya pakti yenye kemikali. ila kunywa ya pakti ni maamuzi.
soko la kongo ni kubwa kuliko watu wanavyofikiri.hata ivyo hatukubali kutolewa kafara kwa manufaa ya siasa zenu.
ndoa ni hiyari,kuwa jirani isiwe sababu ya kebehi,mahindi hampimi viwango ila unga mnapima.sasa na maziwa nayo yapimwe.