A GIRL OF THE GIRLS
Member
- Jul 21, 2022
- 29
- 163
Mimi nitazungumzia Zaidi ulemavu wa neli ya mgongo kwa ujumla wake. Ulemavu wa neli ya mgongo ni hali ambayo mgongo wa mtoto haufungi vizuri wakati ule wa siku ishirini na nane(28) za kwanza za ukuaji wa fetasi, ambao upelekea uharibifu wa uti wa mgongo na ubongo wa mtoto. Huu Ulemavu wa Neli ya mgongo husababibishwa na mambo mbali mbali kama ifuatavyo;mazingira(pombe, moshi wa tumbaku, viuatilfu vya wadudu, kemikali na mionzi), mabadiliko ya vinasaba kutoka kwa wazazi, magonjwa yanayoambukizwa wakati wa ujauzito kama (MALARIA), Matumizi ya dawa ambazo si Rafiki kwa mtoto aliyeko tumboni zikiwemo( Thalidomide, Methotrexate, carbamazepine, valproic acid na sulfadiazine pyrimethamine), matatizo ya kiafya kwa mama kama akiwa anaumwa Kisukari , unene uliokithiri na maambukizi mengine , historia ya familia kuwa na kizazi cha Watoto njiti, kuzaa ukiwa na umri wa miaka 35 na kuendelea, na upungufu wa vitamini mwilini kama vile (vitamin B2 , B6, B9 na B12)
Kuna aina tano za ulemavu wa neli ya mgongo kwa Watoto wadogo nazo ni; spina bifida ( mgongo wazi), anencephaly, encephalocele ,cranioraschisis na inincephaly. Kati ya hizi tano,tatu tu huwa zinatokea mara kwa mara ambazo ni spina bifida, anencephally na encephalocele.
Mchoro huu huonesha fetasi inavyoanza kukua na jinsi ulemavu wa neli ya mgongo unavyotokea kulingana na sehemu husika.
- Tukianza na aina ya spina bifida imegawanyika katika vipera vitatu ambavyo ni;
- Spina bifida occulta; hii ni aina ya spina bifida ambayo mgongo haufungi kabisa katika eneo moja au Zaidi, lakini uti wa mgogngo hauathiriwi.
- Meningocele; katika aina hii mfuko wa maji hujitokeza kupitia ufunguzi kwenye mgongo, lakini uti wa mgongo unabaki ndani ya mfuko.
- Myelomaningocele; aina hii ni kali Zaidi ambayo mfuko wa maji hujitokeza kupitia ufunguzi kwenye mgongo na uti wa mgongo upo ndani ya mfuko.
- Anencephaly; hii ni kasoro ambayo hutokea wakati ubongo na fuvu la mtoto hazikui vizuri wakati wa ujauzito.
- Encephalocele; ni kasoro ya kuzaliwa ambayo hutokea wakati sehemu ya ubongo na utando unaozunguka ubongo hujitokeza kupitia ufunguzi kwenye fuvu.
- Iniencephaly; ni kasoro ambayo mtoto huzaliwa nayo, huku sehemu ya chini ya ubongo na uti wa mgongo wa mtoto hazikui vizuri wakati wa ujauzito.
- Craniorachisis; ni kasoro ya kuzaliwa ambayo hutokea wakati sehemu ya juu ya ubongo na uti wa mgongo wa mtoto hazikui vizuri wakati wa ujauzito.
- Mchoro ufuatao unaonesha aina zote za neli ya mgongo
- Ili tuwe na taifa lenye vijana wenye maono makubwa na afya njema lazima, familia, balozi za nyumba kumi, Vijiji, wilaya, mikoa mpaka taifa tushikamane bila kujali huyu ni kiongozi au sio kiongozi kutokomeza Ulemavu wa neli ya mgongo. Kwa kuzingatia haya yafuatayo;
- Kubadilisha aina ya mlo au vyakula tunavyokula kila siku ; hili ni suala muhimu sana hasa kwa wanawake na Watoto wakike wote waliofikia umri wa kubalehe. Ni muhimu kula vyakula vyenye madini ya chum ana vitamin B9 . vyakula hivyo ni kama ( mboga za majani, maharage,karanga, paranchichi,njegere, papai, ndizi mbivu, machungwa, mayai na maini ya ngombe. Iwapo jamii yetu tutaacha kukariri kuwa chakula chetu huwa ni ugali na fur una kujua manufaa ya kubadili aina mbali mbali za vyakula , matunda na mboga itasaidia san ahata kama mtu akipata mimba ya kushtukiza kupata mtoto mwenye afya njema.
- Picha inayoonesha aina za vyakula vyenye folic acid
- Utumiaji wa vidonge vya folic acid miezi mitatu kabla ya kubeba ujauzito na kuendelea navyo wakati wa mimba mpaka miezi mitatu baada yakijifungua. Hili ni jukumu la baba na mama au kwa wenza waohitaji kupata Watoto wenye akili timamu na ambao viungo vyao vimekamilika. Miaka iliyopita wazazi wetu walikuwa hawatumii hivi vidonge lakini walikuwa wanakula vyakula vya asili ambayo vilikuwa vina madini na vitamini za kutosha. Wewe baba kuwa kiongozi kumkumbusha mkeo kumeza hizo folic acid isije ikatokea akapata mtoto ambaye ana matatizo mkaanza kuingia kwenye gharma za matibabu au ukaanza kumkana mwanao.
- Picha inayoonesha aina za vidonge vya folic acid(vitamin B9)
- Serikali , viwanda binafsi, wafamasia na watu waliosomea mambo ya chakula kushririki katika kuwezesha na kuchagua idadi ya vyakula mbalimbali vya kuongezewa madini ya chuma na folic acid( Large -scale Food Fortification ). Lengo iwe ni kurahisishia watu wa rika zote wenye uwezo na wasio kuwa na uwezo kuweza kupata virutubisho hivyo popote pale walipo kwa bei Rafiki.
- Kuanzisha kampaini ya kuwapa vidonge vyenye Madini ya chuma na folic acid kila wiki mara moja kwa Watoto wakike wenye umri kuanzia miaka 10-19). Hii kampaini inahitaji moyo wa kujitoa kuanzia serikali , wauguzi na mpaka watu waopatiwa hii huduma. Hii sio kwa ajili ya kuwafanya Watoto wafikiri kuwa wakati wa kuzaa umefika hapana. Hivi vidonge vyenye iron na folic acid vinasaidia sana kupunguza upungufu wa damu kwa Watoto wa kike ambao wameshaanza kuona siku zao za hedhi.lkn hii pia inaweza kusaidia kwa Watoto wakike ambao hawapo mashuleni wanaoolewa kupata folic acid ili kupata Watoto wasio na kasoro.
- Picha inayoonesha vidonge vyenye madini ya chuma na Folic acid (FEFO)
- Serikali kupitia wizara ya afya wazidi kutoa elimu ya kwenda kliniki mapema na haraka sana baada ya kujua wewe ni mjazito. Na pia wamama watanzania tuondokane na ile hamu ya kusubiria miezi mitano ifike tukaangalie jinsia ya mtoto tu. Kupima kipimo cha ultrasound ni kuangalia pia kama mtoto anayo kasoro yoyote ambayo inaweza kurekebishwa mapema kabla ya kuzaliwa.
- MREJELEO;
- Participants Manual for Health Workers.
- Research Gate and PubMED.
Attachments
Upvote
477
